http://kariakoodsm.blogspot.com
KARIAKOO BLOG:Kwa Habari Kali Za Mjini | SIASA | BURUDANI | UCHUMI | FASHION | BLOGGER TRICKS | UDAKU | MICHEZO | WASILIANA NA MIMI|0713305567 |urassaombeni@yahoo.com|KWA| MATANGAZO| BABARI| USISITE PIA KUCOMMENT KWENYE HABARI ZETU | <div style='background-color: #de24de;'><a href='http://www.ikiloop.com/' title='link'></a></div>

Saturday, 31 August 2013

CHADEMA YAWAILISHA MAONI YA KATIBA MPYA KWA TUME


TUME ya kukusanya maoni ya Katiba mpya inayoongozwa na Jaji mstaafu, Joseph Warioba, jana imegoma kupokea maboksi 17 ya maoni yaliyokusanywa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na badala yake ikapokea vitabu viwili vya randama kwa ajili ya maoni hayo.

Kutokana na tume hiyo kukataa kupokea ushahidi wa kile kilichoandikwa katika randama mbili zilizowasilishwa na CHADEMA, chama hicho kupitia kwa Katibu Mkuu wake, Dk. Willibrod Slaa, kimesema mpango huo unaashiria dhamira ya tume hiyo kuvibeba vyama ambavyo havina ushahidi wa ukusanyaji wa maoni kutoka kwa wananchi.

Maoni hayo ya wananchi kuhusu rasimu ya Katiba, yamekusanywa kupitia mikutano mbali mbali iliyofanywa na CHADEMA yalifikishwa katika ofisi za tume jana majira ya saa 5:56 asubuhi yakiwa katika gari aina ya Range Rover yenye namba T 162 CDA, ambapo ndani ya gari hilo alikuwamo Dk. Slaa, huku maofisa wengine wa CHADEMA wakiwa katika magari tofauti.

Mara baada ya kukabidhi maoni hayo ya wananchi, Dk. Slaa alisema amesikitishwa na hatua ya tume hiyo kushindwa kubaki na maoni yaliyokusanywa kupitia taasisi zinazoeleweka kwa kile alichoeleza kuwa kuna uwezekano mkubwa wa tume hiyo kupokea maoni ya watu waliojifungia ndani na kusema maoni hayo yametoka kwa wananchi.

Alisema tume inaweza kuibua maswali kutoka kwa taasisi na wananchi namna inavyoweza kujiridhisha na maoni yanayofikishwa kwao kwa kile alichoeleza kushindwa kupokea maoni ya awali kutoka kwa wananchi.

Aidha, Dk. Slaa alisikitishwa na utaratibu wa tume hiyo kushindwa kuwa na mpango maalumu wa kupokea maoni na kuweka kumbukumbu ya upokeaji huo.

“Sijui kama hawa watu walijipanga juu ya upokeaji wa maoni, angalia sisi kama tusingelazimisha watugongee muhuri kwa ajili ya uthibitisho wa upokeaji tungeondoka hivi hivi, sasa hali hii wamefanyiwa watu wangapi ambao hawana kitabu cha kusaini?” alihoji Dk. Slaa.

Aliongeza kuwa katika randama walizowasilisha kwa tume, wameweka hoja 66 baada ya kujiridhisha na hoja nyingine zilizoko katika rasimu ya Katiba yenye hoja 240.

Alisema hoja ambazo hazijaguswa katika randama waliyowasilisha ni zile ambazo zinakubaliwa na CHADEMA pamoja na wananchi waliotoa maoni kupitia mikutano ya CHADEMA.

Namna walivyopata maoni

Kuhusu idadi ya watu waliotoa maoni yaliyowasilishwa jana, Dk. Slaa alisema hadi juzi walipokuwa wakifunga randama, kulikuwa na watu zaidi ya milioni 3.4 waliotoa maoni kwa njia mbalimbali.

Alitaja njia hizo kuwa ni mabaraza ya wazi ambapo walikusanya maoni ya watu 3,200,889 kutoka katika majimbo 81 waliyoyafikia, katika mabaraza ya ndani walifika kata 586 na kukusanya maoni 11,7274.

Njia nyingine zilizotajwa na Dk. Slaa ni ngazi ya majimbo ambapo walifanya mikutano ya ndani katika majimbo 189 ya Tanzania Bara na kukusanya maoni 130,000, kwa njia ya barua pepe walipata watu 612 waliotoa maoni huku kukiwa na ujumbe mfupi wa simu kutoka kwa watu 12,345 pamoja na mitandao ya kijamii na kufanya jumla ya watu waliotoa maoni kuwa 3,462,805.

Dk. Slaa alisema ushahidi wa maoni hayo upo wazi kwao na kuwataka tume ijiridhishe kwa vyama vingine vinavyosema wameshakusanya maoni ya watu zaidi ya milioni mbili.

“Sisi tumefanya haya na wenzetu walete ushahidi kama huu badala ya kukaa vyumbani na kuwatengenezea Watanzania maoni na vitu vya kuingizwa katika Katiba. Hapa tunaililia Tanzania tuitakayo na si kwa masilahi ya chama chochote,” alisema Dk. Slaa.

Aliongeza kuwa mazingira na matamko yanayotolewa na Chama Cha Mapinduzi kuwa wamekusanya maoni ya wananchi wengi na hayawezi kufikiwa na vyama vingine yana nia mbaya kwa nchi na hayaleti taswira nzuri kwa tume.

Usiri wa Tume kwa waandishi

Dk. Slaa pia alisema licha ya tume kuweka suala la uwazi kuwa ni moja ya tunu za taifa, bado imeshindwa kudhihirisha uwazi huo kwa kuwazuia waandishi wa habari kuingia na kushuhudia makabidhiano yanayofanywa katika ofisi za tume.

Alisema suala la Katiba ni la Watanzania wote na vyombo vya habari ni mhimili mkubwa wa serikali usio rasmi wenye kutegemewa kwa kiasi kikubwa na wananchi kutoa taarifa sahihi, lakini vinapozuiwa kushuhudia matukio hayo kwa uwazi ni kuwanyima fursa Watanzania kupata habari sahihi.

Aliongeza kuwa kama tume ya Katiba inafanya usiri katika kupokea maoni ya wananchi, wanaweza vipi kuwaridhisha Watanzania kuwa maoni waliyotoa ndiyo yaliyofanyiwa kazi.

Kuhusu Kingunge

Akizungumzia kauli ya Kingunge Ngombale- Mwiru, aliyoitoa juzi kuhusu umuhimu wa serikali mbili, Dk. Slaa alisema Watanzania wanapaswa kumsamehe mzee Kingunge kwa kuwa sasa amechoka.

Alisema katika vitu alivyopaswa kuvifanya Kingunge katika muda wake wa utumishi serikalini ni pamoja na kusimamia kero mbali mbali zinazolalamikiwa leo, hivyo kuendelea kuwaambia wananchi wasifikirie juu ya muundo wa Muuungano ni kuwakosea heshima.

“Mimi ninamsamehe mzee wangu huyu ila atambue muungano ulio bora ni ule unaoridhiwa kwa hiari na si kulazimisha mfumo unaoonekana una matatizo,” alisema Dk. Slaa

HIVYI NDIVYO FRANCIS CHEKA ALIVYO MGARAGAZA MMAREKANI

Mgeni Rasmi katika Mpambano wa Kimataifa wa kuwani Mkanda wa Ubingwa wa Dunia wa WBU,kati ya Mabondia Francis Cheka wa Tanzania na Phil Williams wa Marekani,Waziri wa Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo,Mh. Dkt. Fenella Mukangala (mwenye koti jeupe) akimvisha Mkanda wa Ubingwa huo,Bondia Francis Cheka baada ya kumshinda kwa Point Mpinzani wake,katika Mchezo uliomalizika usiku huu kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee,Jijini Dar es Salaam.Kulia ni Bingwa wa Zamani wa Masumbwi,Fransous Bhotha.
Bondia Francis Cheka wa Tanzania (kushoto) akimrushia makonde makali mpinzani wake,Phil Williams kutoka nchini Marekani wakati wa mpambano wao wa Kimataifa kuwania Mkanda wa Ubingwa wa Dunia wa WBU,uliofanyika usiku huu kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee,Jijini Dar es Salaam.Bondia Francis Cheka ameibuka kidedea baada ya kumchapa mpinzani wake huyo kwa Point.
Bondia Phil Williams kutoka nchini Marekani (kulia) nae alikuwa akijibu mashambulizi kwa mpinzani wake,Francis Cheka.hadi mwisho wa mchezo uliokuwa wa raundi 12,Francis Cheka aliweza kuibuka Kidedea kwa kumchapa mpinzani wake huyo kwa point na kufanikiwa kumnyang’anya mkanda wa Ubingwa wa Dunia wa WBU.
Chukua hiyoooooo…
Hapa lazima ukae,mie ndio kisiki cha mpingo:hivyo ndivyo Bondia Francis Cheka alivyoonekana kuifanya kazi yake vilivyo.
Refa wa Mchezo huo akimzuia Bondia Francis Cheka baada ya kumkoleza makonde kisawasawa mpinzani wake,yaliyompelekea kwenda chini.
Mpambano ukiendelea.


Wanahabari wakipata taswira za mpambano huo

WATANZANIA WANAPATA MSUKOSUKO CHINA NI KUTOKANA NA KASHFA YA UNGA(MADAWA)

Stori: Na Mwandishi Wetu
Taifa la China halina mzaha mbele ya biashara haramu ya madawa ya kulevya na kwa kutambua kwamba wanaohusika zaidi ni Waafrika, sasa hivi kila mja mwenye ngozi nyeusi aliyepo nchini humo, anapewa msoto wa nguvu.


Wabongo wanaoishi China, kwa sasa wanahenyeshwa isivyo kawaida katika msako uliopewa jina
na Watanzania kwamba ni Oparesheni Safisha Wauza Unga.
Katika hoteli wanazofikia, vijiwe vyao, barabarani na kadhalika, kote huko wanapewa msoto wa guvu kwa kile kinachoelezwa kuwa Wachina hawana imani tena na Watanzania na Waafrika kwa jumla ama wanaoishi nchini humo au hata wale wanaoingia na kutoka.


“Wazungu wa unga (wafanyabiashara wa madawa ya kulevya) wanatuharibia starehe hapa China, hatuishi kwa amani tena. Mtu unaweza kukaguliwa siku nzima kisa eti wanawatafuta wanaouza unga,” alisema Artides Kimota ambaye ni Mtanzania anayeishi China kwa sasa.


Aliongeza: “Unajua sasa hivi China imekuwa na uingizwaji mkubwa wa madawa ya kulevya. Kwa Serikali ya China hii ni kashfa nzito. Kwa vile wanajua Waafrika ndiyo sababu kuu, sasa hivi kila Mwafrika anapewa msukosuko.


“Kwa kweli ukiwa Mwafrika hapa China ni mateso makubwa sana kwa sasa. Kuna agizo la serikali ambalo limelitaka jeshi la polisi hapa China kuhakikisha madawa ya kulevya yanatokomezwa na wahusika wanakamatwa.

“Kila anayekamatwa na madawa ya kulevya au na kitu chochote ambacho siyo halali, anafunguliwa mashtaka. Mimi naishi kwenye Jiji la Qingyuan, nimeshahuhudia Mtanzania mmoja, Wanigeria wawili na Waghana watatu wakikamatwa.
“Kote hakuna kupumua, hata huko Guangzhou, Beijing na kwingineko kunatisha kwa msako. Nasikia kwenye Mji wa Shanwei alikamatwa Mtanzania mwingine, akakutwa na ungaunga wa marumaru ambao alikuwa nao kama sampuli kwa ajili ya biashara zake, alikamatwa lakini aliachiwa baada ya kupimwa na kugundulika siyo madawa ya kulevya.”
Habari zaidi zinasema kuwa pamoja na sifa mbaya ya Watanzania nchini humo lakini imebainishwa kwamba Wanigeria ndiyo kundi hatari na wanawindwa zaidi kwa sababu raia wa nchi hiyo wameshachafuka sana. 
Imebainishwa zaidi kuwa kwa vile siyo rahisi kumtofautisha Mnigeria na Waafrika wengine kwa haraka, ndiyo maana kila Mwafrika anapoonekana ni lazima ale msoto wa kukaguliwa ili kuhakikisha kama ana ‘mzigo’ au hana.
Risasi Jumamosi linamiliki picha zinazowaonesha baadhi ya Waafrika wakiwa chini ya ulinzi, wakitembezwa vifua wazi, kueleka vituo vya polisi kufunguliwa mashtaka ya uhalifu mbalimbali ikiwemo madawa ya kulevya.

KINACHOWAPONZA NI HIKI
Kwa mujibu wa taarifa kutoka China, taifa hilo limeshtukia kwamba pamoja na sheria kali za udhibiti wa madawa ya kulevya zilizopo na adhabu kali ikiwemo ile ya juu kabisa ya kunyongwa hadi kufa kwa mtu anayekutwa na hatia ya kujihusisha na biashara hiyo, polisi wameendelea kupigwa bao la kisigino.
Imeelezwa kwamba watu wanaosafiri na madawa ya kulevya tumboni, maarufu kama punda ndiyo wanaofanya madawa yazagae nchini humo.
“Punda ndiyo wanatuponza, Serikali ya China imeshtukia kuona kwamba madawa yapo sana mitaani, kwa hiyo kukomesha kabisa hilo, wanafanya msako hatari sana. Wakifika chumbani kwako utajuta, wanapekua kila upande wa chumba.
“Vilevile ikitokea mtu anawasili uwanja wa ndege akiwa dhaifu, anafuatiliwa sana. Asikwambie mtu, hakuna Mwafrika aliyepo China anayeishi kwa raha, iwe unauza au huuzi lazima uhenyeshwe,” alisema Dominick Rafiki anayeishi Guangzhou, China.

CHINA YASISITIZA KUENDELEA KUNYONGA
Ripoti ya Shirika la Haki za Binadamu la Amnesty International mwaka 2012, iliitaja China kama taifa kinara kwa kunyonga watu wenye makosa mbalimbali na kuitaja nchi hiyo kama katili zaidi duniani.
Amnesty International inapingana na adhabu ya kifo, kwa hiyo imekuwa ikitumia jitihada mbalimbali kuhakikisha linaishawishi China iachane na hukumu za kunyonga watu bila mafanikio.
Shirika hilo lilieleza kwamba China imeendelea kuweka msisitizo wa kunyonga watu, huku ikiwa na rekodi ya kunyonga maelfu ya watu kila mwaka.

BALOZI AKIRI HALI NI MBAYA
Balozi mpya wa Tanzania nchini China, Luteni Jenerali Mstaafu, Abdulrahman Shimbo amekiri kwamba hali ni mbaya kutokana na wimbi kubwa la Watanzania kukumbwa na kashfa ya madawa ya kulevya, huku wengine wakiwa wameshahukumiwa kunyongwa.
“Ni kweli hali ni mbaya, kuna vijana wetu wengi wanaipa sifa mbaya nchi yetu hapa. Kama inavyofahamika, mimi bado mgeni lakini nikipewa muda kidogo nitakuwa na ripoti kamili ya jinsi Watanzania wanavyohusishwa na hii biashara haramu ya madawa ya kulevya,” alisema Balozi Shimbo ambaye alikuwa Mnadhimu wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ)


Source:GPL

NANDO ATIWA MBARONI KWA KASHFA YA KUIBA CAMERA NDANI YA JUMBA LA BBA...!



Nando ameendelea kuitia aibu Tanzania baada ya kukumbwa na kashfa mpya ya wizi wa kamera ndani ya jumba la big brother.

Wizi huo unadaiwa kutendeka baada ya Nando kualikwa kushiriki fainali za Big brother ambapo Dillish aliibuka mshindi wa shindano hilo.....

Baada ya wizi huo, kamera za jumba hilo zilimuumbua.Nando alikamatwa na kuamriwa airejeshe camera hiyo

MONUSCO LAFANIKIWA KUITEKA NGOME KUU YA WAASI WA M23


ASKARI wa Umoja wa Mataifa wanaolinda amani nchini DR Congo (MUNUSCO), wakiongozwa na vikosi vya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) vimefanya shambulizi la nguvu katika eneo la Kibati (Nyirangongo Territory, Goma, Eastern DRC), eneo hilo ndiyo iliyokuwa ngome kuu ya waasi wa M23 

Shambulio hilo kubwa na la kwanza kufanywa na vikosi vya Umoja wa Mataifa limekuja siku moja, baada ya Askari wa JWTZ kuuawa na waasi wa M23 katika shambulio lao la juzi wakati vikosi vya UN vilipokuwa katika ukaguzi wa maeneo yenye usalama katika mji wa Goma.

Askari huyo wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania, JWTZ Khatibu Mshindo aliuawa kwa kupigwa bomu juzi na waasi wa M23 kwenye Mji wa Goma ulioko Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo baada ya kuzuka mapigano makali.

Mshindo aliuawa baada ya mapigano makali yanayoendelea katika Mji wa Goma, ambapo ilielezwa kwamba Askari wa M23 waliwazidi ujanja majeshi ya Umoja wa Mataifa wanaolinda amani nchini Congo.Wakati Mshindo ambaye alikuwa miongoni mwa askari wa Tanzania wanaounda Jeshi la Umoja wa Mataifa akifikwa na mauti, wapiganaji wengine 10 walijeruhiwa. 

Waasi wa M23 waliokuwa Mashariki mwa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo wamesema kuwa watasitisha mapigano, kufuatia makabiliano makali na wanajeshi wa serikali wanaoungwa mkono na wanajeshi wa Umoja wa Mataifa.

Wakati M23 wakidai kwamba watasitisha mapigano hayo, taarifa zaidi zinaeleza kwamba Majeshi ya UN yanayo ongozwa na majeshi ya Tanzania yamefanya mashambulizi makali ya mizinga pamoja na Askari wa Miguu wakipanda milima na kuwasambaratisha waasi wa M23 na kuteka ngome yao. 

ALIYEFUKUZWA UANACHAMA CCM ZANZIBAR AFUNGUKA YA MOYONI


HATIMAYE Mwakilishi wa Kiembesamaki, Mansour Yussuf Himid, aliyevuliwa uanachama na vikao vya juu vya Chama Cha Mapinduzi (CCM) mjini Dodoma, ameibuka na kutoa kauli nzito dhidi ya chama hicho huku akitoa siri ya kutimuliwa kwake.

Akizungumza kwa mara ya kwanza tangu alipotimuliwa katika kongamano la wazi lililofanyika kwenye Ukumbi wa Bwawani mjini hapa jana, Mansour alisema licha ya kuvuliwa uanachama hataacha kutetea masilahi ya Zanzibar bila woga.

Waziri huyo wa zamani na aliyekuwa Mwakilishi wa Kiembesamaki, alifichua siri kuwa alianza kujengewa chuki, fitina na viongozi wenzake baada ya kuonekana mtetezi na mpigania masilahi ya Zanzibar, ukiwamo msimamo wake wa kutaka suala la mafuta na gesi asilia liondoshwe kwenye orodha ya mambo ya muungano.

Mwanasiasa huyo mwenye ushawishi mkubwa katika siasa za Zanzibar, alisema amepokea uamuzi huo kwa moyo mweupe na hatarajii kwenda mahakamani au kuwania tena uwakilishi wa jimbo hilo kupitia chama chochote.

“Nimekubali kufukuzwa uanachama na NEC ya CCM, wenzako kama hawakutaki huna njia ya kujipendekeza kwao, sitakwenda kortini wala sihitaji kugombea kwa chama chochote cha siasa,” alisema Mansoor.

Hata hivyo alisisitiza kuwa licha ya kufukuzwa, ataendelea kutetea masilahi ya Zanzibar bila woga na hatanyamazishwa kwa vile hiyo ni haki yake kikatiba kama raia huru, pia kadi yake ya CCM haikuwa kimeo kama inavyodaiwa na baadhi ya watu.

Mansoor alisema lengo la Mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka 1964 ilikuwa kutafuta ukombozi na uhuru wa kifikra, kiuchumi na kidemokrasia na si kufunga au kuzuia mawazo na maoni ya watu.

Mwanasiasa huyo mwenye ushawishi katika siasa za Zanzibar, alisema kuwa alianza kujengewa kinyongo na viongozi wenzake baada ya kuonekana kuwa ni mtetezi na mpigania masilahi ya Zanzibar, ukiwamo msimamo wake wa kutaka suala la mafuta na gesi asilia liondoshwe kwenye orodha ya mambo ya muungano.

“Hapa ndipo nilipoanza kuonekana mnoko, nikapewa majina mengi na kupigwa. Kwa taarifa yao, sitaacha kupigania ninachokiamini, nitabaki kuwa mtetezi wa haki na usawa hadi nitakapokufa, ila sihitaji kuwa mwakilishi wa mahakamani, sina pesa ya kulipa wanasheria, mshahara wenyewe umekatwa miguu,” alisema Mansoor huku nyimbo za kimapinduzi zikiimbwa ukumbini.

Alisema kitendo cha CCM kumpima na kumuona hafai ni haki yao na ataendelea kuheshimu maamuzi hayo, kwa sababu ndiyo yaliyotolewa na kufikiwa na chama kwa kufuata taratibu zao.

Alisema malengo yake mengi ya kisiasa akayaweka wazi ifikapo mwaka 2015 kama ataona kuna haja ya kufanya hivyo, lakini alisisitiza kuwa hataiacha au kuitupa Zanzibar katika maisha yake akiwa ndani au nje ya chama chochote.

Akizungumzia muungano, mwanasiasa huyo alisema yeye ni muumini wa muungano wa Tanganyika na Zanzibar lakini alisema kuwa angependa kuona muungano wenye usawa, haki na heshima na si upande mmoja kuutafuna mwingine.

Kwa upande mwingine alisema kuna baadhi ya vyama vya siasa vimeanza kumfuata na kumtaka awe mwenyekiti wa taifa na wengine wakitaka achukue fomu ya kuwania kiti cha Kiembesamaki.

Alilaumu tabia na hulka ya baadhi ya wanasiasa wa Zanzibar kupenda kubaguana kwa rangi na uzawa na kuongeza kuwa mambo hayo si mazuri kuyakumbatia kwani hayana mwisho mwema.

Wakati huo huo, Kamati ya Maridhiano Zanzibar imekiri kuwa haina tena uwakilishi wa vyama vya siasa vya CCM na CUF.

Msimamo huo kwa mara ya kwanza umewekwa wazi jana na Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Hassan Nassor Moyo.

Moyo alisema kuwa kamati yake ni ya utetezi na kupigania masilahi ya Zanzibar na kazi yake kubwa ni kudai hadhi na tunu ya Zanzibar kama nchi na taifa lenye mamlaka na uwakilishi katika Umoja wa Mataifa.

Msimamo huo umekuja baada ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein, kuikana hadharani kamati hiyo na kusema haitambui na wala haina baraka za CCM wala serikali yake.

Katika kuonesha kuwa kamati hiyo ni ya wananchi, hata Mratibu wa kongamano hilo ambaye pia ni Mwakilishi wa Mji Mkongwe, Ismail Jussa Ladhu, alipokuwa akimkaribisha Waziri wa Katiba na Sheria wa SMZ, Aboubakari Khamis Bakari, alisisitiza kuwa anasimama kuchangia na kutoa maoni yake kama mwananchi na si kwa kofia ya dhamana yake.

Akizungumza katika kongamano hilo, Waziri wa Katiba na Sheria Zanzibar, Aboubakar Khamis Bakari, alisema rasimu ya mabadiliko ya katiba haifai kwa vile inainyima Zanzibar mambo mengi ya msingi na kuikandamiza kiuchumi.

Aboubakary alisema muungano wa Tanganyika na Zanzibar ni wa mataifa mawili yaliyokuwa na uwakilishi sawa kama dola, hivyo si haki upande mmoja kuonekana mgeni mwalikwa katika ushiriki wake.

Aliwataka wananchi kuacha hofu ya kuwapo kwa muungano wa serikali tatu na kusema jambo hilo halitavunja muungano au kutokea machafuko.

Mmoja wa wajumbe wa Kamati ya Maridhiano, Eddy Riyami, alitangaza kuhama rasmi CCM na kusema ataamua baadaye atajiunga na chama gani kama ataona kuna haja ya kufanya hivyo.

Riyami alichukua mjadala mkubwa wakati wa sakata la kutoweka na kujiuzulu kwa aliyewahi kuwa Mwakilishi wa Jimbo la Mkunazini, Salum Msabaha Mbarouk, ambaye sasa amehamia CCM.

Source:Tanzania Daima

Thursday, 29 August 2013

ASKOFU KULOA AFARIKI DUNIA




Taarifa ambazo zimetufikia hivi punde zinasema kuwa Askofu Mkuu wa Evangelistic Assemblies God Tanzania, Moses Kulola amefariki dunia takriban dakika 25 zilizopita.
Kwa mujibu wa taarifa za kuaminika  kutoka kwa watu wa ndani wa familia hiyo, zinaeleza kuwa Askofu Kulola amefariki katika hospitali ya AMI (African Medical Investments) iliyopo Slipway jijini Dar es Salaam.

Askofu Kulola, ambaye amezaliwa mwaka 1928, amekuwa akisumbuliwa na maradhi kwa muda mrefu na hata kufikia hatua ya kupelekwa nchini India kwa matibabu.
Katika uhai wake, amepata watoto wengi wa kiroho ikiwemo Dr Daniel Kulola, Mchungaji Florian Katunzi, Zakaria Kakobe, Mzee wa Upako, Maboya, Mwasota na wengineo wengi.
BWANA ametoa na BWANA ametwaa, jina la BWANA lihimidiwe. 
MJUE ASKOFU MOSES KULOLA

Moses Kulola, alizaliwa mwezi Juni 1928, katika familia ya watoto kumi, na watano kati yao bado ni hai. alisajiliwa katika shule ya kwanza mwaka 1939 iitwayo Ligsha Sukuma shule ya misheni baada ya Ligsha, alijiunga na taasisi ya usanifu mwaka 1949. Alibatizwa mwaka 1950 katika Kanisa la AIC Makongoro.

Ni mume wa Elizabeth na wamezaa watoto10 ambapo saba bado hai.alianza kazi za kimisionari mwaka1950 japokuwa aliitwa mwaka 1949 mara tu baada ya kubatizwa.

Mwaka 1959 alianza kufanya kazi serikalini, wakati huo huo akihubiri Injili katika miji na vijiji. Utumishi wake mkubwa kwa nchi ulifika mwisho mwaka 1962, ambapo aliamua kujitolea moja kwa moja nguvu zake zote, mwili na nafsi. Mwaka 1964 alijiunga na chuo cha kiteolojia na 1966 alitunukiwa stashahada.

Hakuacha elimu pale tu, aliendelea na masomo mbalimbali ambapo alitunukiwa vyeti mbalimbali katika mataifa mbalimbali.

Alihudumu kikazi kwa miaka miwili kama Mchungaji kabla ya kuwa mpentekoste mnamo 1961-1962, alifanya kazi katika kanisa la TAG 1966 mpaka 1991 ambapo aliamua kuanzishaa makanisa Evangelistic Assemblies God (EAGT), ambapo yalifanikiwa kukua kwa kasi kubwa katika nchi za Tanzania, Zambia , Malawi na kwa ujumla kuna makanisa yapatayo 4000 katika nchi mbalimbali yakiwemo makubwa na madogo Askofu Moses Kulola anayeongoza makanisa elfu nne, Askofu Msaidizi wake ni Mwaisabila.
Askofu Kulola aliyeketi akiwa na waimbaji wa injili nchini Mwinjilisti Faustin Munishi mkono wa kushoto pamoja na Emmanuel Mwasota. mwanzoni mwa mwaka 1970
Mchakato wa kuongoza makanisa elfu nne si rahisi na kwamba kumefanyika mgawanyiko wa majimbo yasiyopungua 34 ya kazi na kanda tano kwa ajili ya kurahisisha kazi na kila kanda na jimbo lina mwangalizi wake. 
Nampenda sana Askofu Moses Kulola maana anafanya kazi ya MUNGU kwa moyo na kwa mujibu wa kitabu cha historia yake Askofu Kulola amezunguka Tanzania nzima tena wakati mwingine kwa kutembea kwa miguu na kwenye mazingira magumu sana kiasi kwamba ni wito mkuu wa MUNGU mkuu alionao Askofu Kulola na kwa miaka zaidi ya 60 amekuwa akihubiri neno la MUNGU na hadi sasa MUNGU anamtumia sana, katika mkutano uliopita wa askofu Kulola pale viwanja vya jangwani jijini Dar es salaam maelfu ya watu walihudhulia na wengi sana kufunguliwa na injili anayohubiri askofu Kulola ni injili iliyonyooka na akiwataka wanadamu kumpa YESU KRISTO maisha yao ili wapate uzima wa milele bure.

Ukiacha mengi ambayo Mungu anaendelea kumtumia mtumishi wake huyu, kuna suala la nywele zake, askofu Kulola kama tulivyowahi kuandika siku zilizopita, hajanyoa nywele zake kwa takribani miaka 47 sasa, kwakuwa hakupendezwa na suala la kwenda salon kunyoa nywele zake hivyo akamwambia Mungu nywele alizokuwa nazo kwa wakati huo zisikue zaidi au kupungua, na ndivyo ilivyo mpaka sasa wembe haujapita kichwani mwake.
Askofu Kulola akipeana mkono na mwanae Daniel Kulola ambaye ni mchungaji. 



WEZI WALIOVALIA KAMA POLICE WAVAMIA HABIB AFRICAN BANK NA KUIBA MAMILIONI


Watu wanaodhaniwa kuwa ni Majambazi ambao wamevalia sare za Jeshi la Polisi wamevamia Habib Afriican Bank Kariakoo DSM na kupora kiasi kikubwa cha Fedha.


Jeshi la polisi kanda maalum wamethibitisha kutokea kwa tukio hilo.

Monday, 26 August 2013

SAKATA LA OFISA USALAMA:SIRI NZITO YAFICHUKA...

SIKU chache baada ya Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam kumnasa Bw. Alquine Masubo (42), akidaiwa kujifanya Ofisa Usalama wa Taifa, siri nzito juu ya vitendo vinavyodaiwa kufanywa na mtuhumiwa huyo, sasa zimeanza kufichuka. Habari na picha zilizochapishwa na gazeti hili juu ya tukio la kukamatwa Bw. Masubo, ziliibua maswali mengi kwa baadhi ya wasomaji ambao baadhi yao walipiga simu katika chumba cha habari na kudai wao ni miongoni mwa waliotapeliwa na mtuhumiwa huyo. Mkazi mmoja wa Dar es Salaam (jina tunalihifadhi), alisema mtuhumiwa ambaye huwa na kawaida ya kushirikiana na mke wa kigogo mmoja wa Jeshi la Polisi, amewahi kumbambikia kesi ya utapeli na kujitambulisha kwake kuwa yeye ni Ofisa wa Idara ya Usalama wa Taifa. Alisema, baada ya kukamatwa na kufikishwa kituo kimoja cha polisi Dar es Salaam, mtuhumiwa alitoa agizo kwa Kamishna Msaidizi wa jeshi hilo (sasa ni mstaafu), atoe amri kwa RCO (Mkuu wa Upepelezi), aweze kukaguliwa nyumbani kwake "Walipokwenda nyumbani kwangu na kukosa nyaraka ambazo walikuwa wakizitafuta, walichukua vitu mbalimbali ndani kwangu ambavyo ni pamoja na kitanda, godoro, sofa, kabati, friji, DVD, televisheni, redio kubwa na vingine vingi. "Kabla hawajachukua vitu hivyo, alimwambia mdogo wangu ampe sh. milioni tatu ili nisichukuliwe vitu vyangu, alipewa sh. milioni moja, lakini bado alitoa amri vitu vyangu vibebwe licha ya kutoa risiti ya kila kitu walichochukua. "Pia alimtaka mdogo wangu ampe pesa ili niweze kupewa dhamana mahakamani, kesi niliyobambikiwa dhamana yake ilikuwa wazi... aliwaambia waendesha mashtaka kuwa yeye ni Ofisa Usalama kutoka Ikulu, ambayo imemtuma ili nisipewe dhamana," alidai mkazi huyo. Aliongeza kuwa, kutokana na agizo hilo alikaa gerezani miezi mitatu, lakini alisaidiwa kupewa dhamana kutokana na juhudi za dada yake ambaye ni karani wa mahakama (bila kumtaja jina wala mahakama anayoifanyia kazi jijini humo). Mkazi huyo aliongeza kuwa, wakati akiwa mahabusu katika kituo kimoja cha polisi Dar es Salaam, mtuhumiwa (Masubo) alikwenda kituoni hapo na kumtaka atoe maelezo anayotaka yeye na asipofanya hivyo, atambambikia kesi kubwa zaidi. "Nilikataa kuandika maelezo anayotaka yeye, wakati huo ndugu zangu walikuwa nje, mtuhumiwa aliwafuata na kuwaambia sitaki Akizungumza na gazeti hili kwa njia ya simu Dar es Salaam jana, Kamanda wa kanda hiyo, Kamishna Suleiman Kova, alisema mbali ya tukio hilo, jeshi hilo pia litazungumzia mambo mengine makubwa waliyoyabaini. "Mkutano wangu wa kesho (leo) na waandishi wa habari, nitazungumzia tukio hilo, pia kuna mambo mengine makubwa ambayo tunatarajia kuyazungumzia si hilo tu," alisema. Aliongeza kuwa, tayari kuna kikosi maalumu cha polisi ambacho kinaendelea na uchunguzi wa tukio hilo. Mlipuko huo ulitokea juzi ambapo bomu hilo linadaiwa kutengenezwa kwa chupa na kujazwa petroli ambapo madhabahu, gari la mchungaji vinadaiwa kuungua. Mchungaji wa usharika huo, Noah Kipungu juzi alisema chupa za bia zilizojazwa mafuta hayo zikiwa zimezibwa na mifuniko iliyotobolewa tundu, ziliwashwa moto ili kuchochea mlipuko huo. Alisema katika tukio hilo, hakuna mtu aliyekufa wala kujeruhiwa zaidi ya watu kukumbwa na taharuki. kutoa maelezo hivyo atanipoteza na sitaonekana tena uraiani. "Nd u g u z a n g u wa l i k u j a kunibembeleza nibadilishe maelezo na kuandika aliyotaka mtuhumiwa, lakini nilikataa....baada ya kusoma habari za mtuhumiwa katika gazeti lenu (Majira), Ofisa mmoja wa polisi ambaye alihusika kumkamata Bw. Masubo, alinipigia simu na kunieleza usumbufu aliopata akitakiwa kumuachia mtuhumiwa. Aliongeza kuwa, inawezekana mtuhumiwa amewatapeli watu wengi hivyo, Agosti 28, mwaka huu atakwenda Kituo cha Polisi Kati ili aweze kufikisha malalamiko yake. "Kwa sasa nipo Tanga.. kwa shughuli zangu za kibiashara, narudi Dar es Salaam keshokutwa (kesho), Jumatano nakwenda kutoa malalamiko yangu dhidi ya huyo jamaa Kituo cha Polisi Kati," alidai. Kamanda Kova Kutokana na tuhuma hizo, gazeti hili lilimtafuta Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kamishna Suleiman Kova, kama kuna baadhi ya watu waliojitokeza kulalamikia utapeli wowote waliofanyiwa na mtuhumiwa. Katika majibu yake, Kamishna Ko v a a l i s ema j e s h i h i l o litazungumzia sakata la ofisa huyo leo saa saba mchana na kama kuna maswali yaulizwe katika mkutano huo. "Wiki iliyopita nilizungumzia suala hili, katika kituo kimoja cha redio, lakini kama kuna maswali yoyote, mje kesho saa saba (leo) katika mkutano wangu na waandishi wa habari, nitazungumzia sakata zima la huyo Ofisa Usalama feki," alisema. Akizungumzia juu ya mtuhumiwa kudaiwa kushirikiana na baadhi ya vigogo ndani ya jeshi hilo alisema; "Sifahamu lolote kuhusu hilo ila nalipokea, tutaanza kulifanyia kazi," alisema

BIG BROTHER WINNER: DALISH MATHEW-NAMIBIAN

Mshindi wa Big Brother The Chase 2013, Dillish Matthews. MWANADADA Dillish Matthews kutoka nchini Namibia amejishindia zaidi ya shilingi milioni 480 (300,000 usd) baada ya kuibuka mshindi wa Big Brother The Chase 2013. Dillish amewabwaga washiriki wenzake wanne Beverly, Melvin, Cleo na Elikem alioingia nao tano bora. Wa kwanza kutolewa tano bora alikuwa Beverly akifuatiwa na Melvin baadaye akafuata Elikem na kuwaacha Dillish na Cleo wakichuana kutafuta mshindi wa dola 300,000 za Kimarekani. Hatimaye Cleo naye aliondolewa katika kinyang'anyiro hicho na kumuacha Mnamibia Dillish akiondoka na kitita cha zaidi ya milioni 480 na kuwa mshindi wa Big Brother Season 8 The Chase 2013

Sunday, 25 August 2013

CHEKI PICHA FIESTA SINGIDA 2013

Msanii machachari wa muziki wa bongofleva/filamu Shilole akiimba huku akiwa amebebwa na shabiki wake,huku shangwe na miluzi za mashabiki zikiwa zimetawala kila kona.
Baadhi ya mashabiki waliojitokeza kucheza jukwaani,wakionesha umahiri wao wa kukata nyonga mbele ya umati wa wakazi wa mji wa Tabora na vitongoji vyake,waliojitokeza kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2013 ndani ya uwanja wa Al-Hassan Mwinyi usiku huu.

Anajiita Raisi wa Manzese,kutoka kundi la Tip Top Connections,atambulikae kwa jina la Madee akiwaimbisha mashabiki wake wimbo wake wa NANI KAIBA POMBE YANGU,usiku huu kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2013.

Mashabiki wakiitikia kwa pamoja huku mikono yao wakipunga hewani.
Mmoja wakali wa hip hop,Stamina akikamua jukwaani vilivyo usiku huu mbele ya umati wa wakazi wa mji wa Tabora na vitongoji vyake waliojitokeza kushuhudia makamuzi ya wasanii mbalimbali wa tamasha la Serengeti Fiesta 2013

PICHA: FIESTA HAKIKA NI TWENZETU: PICHA MBALIMBALI ZICHEKI HAPA

Mmmh... Linah umetisha wawili double .....?
Recho ..... utamtaja tu wewe jishebedue!!!!
Haaaaa... Shilole unamkonyeza huyo hapo ama nini.....??
Shilole hizo ndiyo pamba za America au??
Nay vipi tena hicho kibinti au ndiyo baridi la Serengeti Fiesta 2013 .....??
Msechu tumekuona ....
Zirro,Muli B, mnatisha hata bila pozi.....
Aaah Shafii umekutana na mdau mwenzako wa soka nini mbona unatabasamu sanaaa????
Nani anadowea kwa mwenzake sasa.... nawauliza nyie hapo B12 & Shetta????
Recho,Nalee... pozi hilo mnapendana kweli au ndio urafiki wa msimu wa Serengeti Fiesta 2013???
Shetta si unamke na mtoto wewe eeeh???
Mmesomeka...,Msechu,Mchomvu,G Walawala & B12 !!!
Basi sawa mrembo!

KANISA LACHOMWA MOTO DAR ES SALAAM


Dar es Salaam. Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Jimbo la Kati, Usharika wa Segerea Wilaya ya Ilala, limechomwa moto na watu wasiojulikana usiku wa kuamkia jana.


Tukio hilo lilitokea saa saba usiku, wakati waumini wa kanisa hilo wakiwa katika mkesha wa maombi ya maandalizi ya mkutano wa injili unaoanza leo.


Mchungaji wa kanisa hilo, Noah Kipingu alisema wakati wakiwa katika maombi ghafla walisikia sauti ya kitu kilichorushwa kutoka nje ya kanisa kikiambatana na moto, ambapo kilianguka madhabahuni na kuanza kuunguza baadhi ya vifaa vya kanisa.


“Tukiwa tumesimama mbele ya madhabahu kwa njia ya mduara ndipo nyuma ya madhabahu ukatokea mlipuko mkubwa kwa sauti ya kishindo, na moto ukatanda madhabahu,” alisema Kipingu na kuongeza kuwa:


“Katika namna ya kibinadamu hakuna aliyeweza kuvumilia, kila mtu alikimbia akitafuta namna ya kujiokoa.”


Kipingu alisema kuwa alipobaini kuwa ulikuwa ni moto wa mafuta aliwaambia waumini wake waingie ndani kwa ajili ya kuuzima, wakati wakiuzima moto huo walipata taarifa kuwa gari la Mchungaji, Toyota Cresta lenye namba za usajili T 482BAF lililokuwa nje ya kanisa lilikuwa likiwaka moto. “Baadhi ya waumini waliokuwa ndani walikwenda nje kushirikiana na mlinzi kuuzima moto huo, tunamshukuru Mungu kwamba matukio yote mawili tumeyashinda kwa uwezo wake,” alisema.


Kipingu alisema kuwa shambulizi hilo lilizua taharuki kubwa kwa waumini wake, na kwamba baadhi ya watu waliwaona watu wanne wakikimbia kutoka eneo la kanisa baada ya kutukio hilo.


Shukuru Thobias mmoja wa waumini waliokuwepo kanisani wakati tukio hilo likitokea, anasema aliona vitu kama mshale vikianguka madhabahuni na vilipodondoka vililipuka kama moto.


“Moto ulianza kuunguza Biblia na makapeti, ndipo tukaanza kukimbia kwenda nje kuchukua mchanga na kuanza kuuzima. Baada ya hapo tulianza kukimbia huku wengine wakidondoka na kujeruhiwa kidogo miguuni. Niliporudi baadaye niligundua zilikuwa ni chupa tatu za bia zilizokuwa zimetengenezwa bomu la petroli,” alisema Thobias.


Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kamishna Suleiman Kova alithibitisha kutokea kwa tukio hilo ambalo hakuna mtu aliyepoteza maisha na kulitaja kuwa ni jaribio la kiharifu lililoshindwa.


“Hakuna mtu aliyepoteza maisha, lilikuwa jaribio ambalo halikufanikiwa. Wakati tukio linatokea waumini walikuwa kanisani kwa hiyo waliwahi kuuzima moto kabla haujaleta madhara,” alisema Kova.


Matukio ya makanisa kuchomwa moto Mei 26, 2012, Kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG) lililopo Mtaa wa Kariakoo mjini Unguja, lilichomwa moto usiku na watu wasiofahamika

Kamati Kuu ya CCM yamzuia Kagasheki kushiriki siasa mkoani Kagera


Dodoma. Suala la kutimuliwa kwa madiwani wanane wa CCM katika Manispaa ya Bukoba limeingia sura mpya baada ya Kamati Kuu kuwazuia Meya, Dk Anatory Amani na Mbunge wa Bukoba Mjini, Balozi Khamis Kagasheki kushiriki katika siasa mkoani humo hadi mwaka 2015.


Habari zilizopatikana kutoka ndani ya kikao hicho zinaeleza kuwa uamuzi huo umefikiwa baada ya kubainika mgogoro wa viongozi hao, unakiumiza chama katika jimbo hilo.


Taarifa zilidai chanzo cha ugomvi kati ya Balozi Kagasheki na Dk Amani, ni kwa kila mmoja kutaka kugombea nafasi ya ubunge Jimbo la Bukoba mjini katika uchaguzi ujao. Na kwa uamuzi huo, Kagasheki na Dk Amani hawatashiriki uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.


Hata hivyo, akitangaza uamuzi huo jana, Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye alisema viongozi hao watakutana na Kamati Kuu leo na baada ya hapo utatangazwa uamuzi uliofikiwa.


Mbali na meya na mbunge huyo ambaye pia ni Waziri wa Maliasili na Utalii, wengine walioitwa katika kikao hicho cha leo ni Mwenyekiti wa CCM mkoani humo, Costansia Buhinye, katibu wake, Averin Mushi pamoja na mwenyekiti wa chama Wilaya ya Bukoba, Yusuph Ngaiza na katibu wake, Janath Kayanda.


Kutokana na uamuzi huo, Kamati Kuu ambayo ilimaliza kikao chake saa 8:30 usiku wa kuamkia jana italazimika kukaa tena leo kuwaelezea uamuzi uliofikia.


Kumekuwapo na mgogoro mkubwa katika Baraza la Madiwani wa Manispaa ya Bukoba, ukimuhusisha Kagasheki na baadhi ya madiwani kwa upande mmoja; na Dk Amani na kundi jingine la madiwani kwa upande mwingine.


Wakati wa mgogoro huo madiwani wamekuwa wakituhumiana ufisadi, na CCM imekwishawatuma viongozi wake wa juu kuingilia kati mgogoro huo akiwamo mwenyekiti wake, Rais Jakaya Kikwete, lakini hakuna mafanikio yaliyopatikana.


Kufikishwa kwenye Kamati Kuu kwa suala hilo kumekuja baada ya uongozi wa CCM Mkoa wa Kagera kuamua kuwatimua uanachama madiwani hao, hatua ambayo ilikuwa inahatarisha nafasi zao na hivyo kukiingiza chama hicho kwenye uchaguzi mdogo.


Habari kutoka ndani ya vikao hivyo zinasema kuwa kuna uwezekano mkubwa kwa viongozi hao kuwajibishwa kwa kukiuka kanuni, kwa kuwa upo uamuzi wa chama unaokataza viongozi waliochaguliwa katika vyombo vya dola kuwajibishwa kwa staili hiyo.


Madiwani waliovuliwa uanachama na kata zao katika mabano ni pamoja na Richard Gaspar (Miembeni ), Murungi Kichwabuta (Viti Maalumu), Alexander Ngalinda ambaye pia ni Naibu Meya (Buhembe) na Yusuf Ngaiza ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM wa Wilaya (Kashai).


Wengine ni Deusdedit Mutakyahwa (Nyanga), Robert Katunzi (Hamugembe), Samwel Ruhangisa (Kitendaguro) na Dauda Kalumuna (Ijuganyondo)


Baada ya kutimuliwa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye alisema chama Mkoa wa Kagera hawana uwezo wa kuvua uanachama na kwamba wenye uwezo huo ni ngazi ya taifa.


Nape alisema kwa mujibu wa taratibu za CCM, Mkoa wa Kagera walitakiwa kuwasilisha tuhuma hizo ngazi za juu ili zijadiliwe na kuamuliwa na Kamati Kuu (CC).


Aliongeza kuwa kwa mujibu wa taratibu, viongozi wa kuchaguliwa na wananchi kama wabunge na madiwani, hawawezi kuvuliwa uanachama na vikao vya chini bali chombo chenye mamlaka hayo ni Kamati Kuu.


Hata hivyo, siku moja baada ya tamko hilo la Nape, CCM mkoani Kagera kilisisitiza kuwa uamuzi wa kuwafukuza madiwani hao ni halali, kwa kuwa ulifanywa na kikao halali kwa mujibu wa katiba na kanuni za chama hicho.


Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Kagera, Costansia Buhiye, alisema kwa mujibu wa katiba na kanuni za chama hicho, hakuna kikao chochote ndani ya chama kinachoweza kukinzana na kikao kingine kwa hivyo, bado madiwani hao wamefutiwa dhamana ya uanachama kama mkoa ulivyoamua.


Buhiye alisema kikao cha Halmashauri Kuu ya Mkoa ndicho kikao kikuu chenye uamuzi wa kumwajibisha mwanachama yeyote, iwapo atabainika kwenda kinyume cha taratibu na kanuni za chama, kwa mujibu wa katiba ya CCM.


Suala la Mansour


Katika hatua nyingine, Kamati Kuu imelipeleka suala la kutimuliwa uanachama kwa Mwakilishi wa Kiembesamaki Zanzibar, Mansour Yusuf Himid kwenye Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ambako litajadiliwa leo na kutolewa uamuzi.


Nape alisema mamlaka ya mwisho ya kumteua mwakilishi ni NEC, hivyo lisingeweza kujadiliwa na Kamati Kuu.

Saturday, 24 August 2013

Taswira Kutoka Mkutano wa Hadhara wa Mabaraza ya Wazi ya Chadema:Mwenyekiti wa Chadema na Mbunge wa Hai Freeman Mbowe na Mkurugenzi wa Sheria na Haki za Binadamu wa Chadema na Mbunge wa Singida Mashariki Waung'uruma Mjini Songea

Mkurugenzi wa Sheria na Haki za Binadamu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)na Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu, akiwahutubia wananchi wa mji wa Songea, katika mkutano wa hadhara wa Mabaraza ya Wazi ya chama hicho, kujadili rasimu ya katiba mpya, uliofanyika mjini Songea.
Mmoja wa wakazi wa mji wa Ludewa, Thadey Ngairo, akitoa maoni yake kuhusu katiba mpya, mbele ya Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, wakati wa mkutano wa hadhara wa Mabaraza ya Wazi ya chama hicho wa kujadili katiba mpya mjini Ludewa

Monday, 12 August 2013

VIDEO:SHEIKH PONDA ALIPOPELEKWA MUHIMBILI PAMOJA NA PICHA ZA MAJERAHA YAKE

PICHA: HENRY KILEWO ALIPOINGIA DAR ES SALAAM KUELEKEA NYUMBANI KWA FAMILIA YAKE

M4C ikiingia Dar kutokea Tabora kupitia Igunga...
Pella Ngunangwa dereva makini wa CHADEMA (papaa Pella mutu ya watu imechoka sana jicho nyanya) kaendesha usiku kucha jumlisha jana yake tulikuwa na pilikapilika za kuhakikisha watu wetu wanapelekwa Igunga
Hellen Baja, mfanyakazi mwenzangu alikuja kutupokea maeneo ya Mbezi
Papaa Pella na Wakili msomi PK, tumeingia Dar 
Booooooom. tukafika nyumbani....
Naomba uweke maneno kwenye hizi picha maana?? Noma...
Oh My God...
I dont Believe ...
Thank you God. you are so wonderful
Welcome back sweet heart
Kila mtu anataka kum'beba baba Lincon
Ngoja niwaone wanangu..
Hongera sana Wakili msomi PK, wewe ni noumaaaaaaaaaa
Karibu mume wangu, watoto wako hawa hapa
KILEWO: Oh God, asante kwa kuitunza familia yangu 
Wakili msomi PK: Watoto wazuri nimewaletea baba yenu kama nilivyomwahidi mama yenu na watanzania na wapenda haki
weka maneno 
Wakili: Ni faraja sana kwangu ninapoona Mungu ameniongoza kuleta furaha tena kwenye familia kama hivi
Oh my God, we are so much Happy
My chif cameraman Prospa Njau na Wakili Msomi PK
Final i have my kids, niliwamiss sana wanangu , namshukuru sana Mungu kwa kusimamia Haki
Tumaini Makene afisa habari wa CHADEMA akiwa na mfanyakazi mwenzangu Hellen Baja
Namshukuru Mungu kwa watoto hawa wazuri pamoja na mama yao ambae alijitahidi sana kuangalia familia nilipokuwa Jela
Baada ya mapokezi, Hellen akafanya jambo moja kubwa sana ambalo lilifanyika jioni... naona kaamua kupiga Pipooooooooz.... pawaaaaaaaaaaaa... any way nitakuwekea picha za jioni endelea ku visit


Source:Joyce Kiria