http://kariakoodsm.blogspot.com
KARIAKOO BLOG:Kwa Habari Kali Za Mjini | SIASA | BURUDANI | UCHUMI | FASHION | BLOGGER TRICKS | UDAKU | MICHEZO | WASILIANA NA MIMI|0713305567 |urassaombeni@yahoo.com|KWA| MATANGAZO| BABARI| USISITE PIA KUCOMMENT KWENYE HABARI ZETU | <div style='background-color: #de24de;'><a href='http://www.ikiloop.com/' title='link'></a></div>

Sunday, 30 June 2013

LOWASA AMPA MWONGOZO KIKWETE JUU YA USHOGA IF OBAMA ATARUDIA KAULI YA SENEGALI



Mwenyekiti wa Kamati ya Mambo yaNje na Ushirikiano wa Kimataifa, Edward Lowassa, amemtahadhalisha kujiepusha na kauli za kuunga mkono ushoga.

Lowassa ambaye pia ni Mbunge wa Monduli, ameliambia NIPASHE Jumapili ofisini kwake jijini hapa jana kuwa ushoga na hai za ndoa kwa watu wa jinsia moja vinaweza `kuiharibu’ ziara yake hapa nchini.

Mapema wiki hii, Rais Obama alikaririwa akizungumzia masuala hayo yanayotajwa kuwa ni moja ya haki za msingi za binadamu, alipokuwa Senegal, lakini akapingwa.

“Watanzania hawatalikubali na wataendelea kushikilia uhuru na heshima walizojengewa tangu awali, kwamba ushoga na ndoa za jinsia moja havikubaliki,” alisema.

Akiwa Senegal, Rais Obama alitaka serikali za Afrika kutoa haki kwa mashoga kama inavyotoa kwa raia wengine.

"Ninachotegemea, I pray and hope (ninasali na kutegemea) kwamba kuhusu mashoga na ndoa za jinsia moja, Rais Obama hatarudia kauli aliyoitoa kule Senegal,” alisema.

Aliongeza, "ninasema hivi kwa sababu Tanzania hatuamini katika ushoga, na endapo utawalazimisha Watanzania, watakukatalia na kushikilia uhuru na heshima waliyojengewa toka awali."

AHIMIZA MAPOKEZI MAZURI
Hata hivyo, Lowassa aliwataka Watanzania kuiheshimu na kuitumiavema fursa ya kutembelewa na Rais Obama, hivyo wajitokeze kumlaki kwa wingi.

"Tutambue mataifa makubwa yanakimbilia maslahi ya karne inayofuata, kwa mfano Rais wa China, Xi Jiping siku moja baada ya kuapishwa kwake alikuja hapa nchini, " alisema.

Hivyo, alitoa wito kwa Watanzania kuhakikisha maslahi na fursa za kiuchumi zinakuwa za kwanza kulindwa, kwa kuwa ziara hiyo itafungua milango zaidi kwa wawekezaji kuja nchini.

Pia, Lowassa alisema ziara ya Rais Obama ni kielelezo cha amani na usalama uliopo, na kwamba itasaidia kuwavutia watalii na wadau wa sekta nyingine za maendeleo kuitembelea Tanzania.

KITUO CHA KIJESHI
Kuhusu hofu na tetesi kuwa ziara hiyo imelenga taifa hilo kuja hapa nchini kufungua kituo cha kujiimarisha kiulinzi, Lowassa alisema Watanzania wanapaswa kufahamu kuwa tayari nchi hiyo ina kituo cha kijeshi nchini Kenya.

"Tuangalie maslahi yetu tuachane na mitazamo hasi, kama ni kituo cha kijeshi tayari kipo Kenya, tujiulize kwa nini marais wa Marekani Bill Clinton na George Bush walivyofanyaziara zao hapa nchini hawakwenda Kenya," alisema.

WALINZI WA NDANI KUWEKWA KANDO
Kuhusu ziara hiyo kutumia ulinzi wa kimataifa huku majeshi ya Tanzania yakiwekwa kando kwa ushiriki wa moja kwa moja, Lowassa alisema Rais wa Marekani ana kiwango cha juu cha ulinzi unaosimamiwa na nchiyake pekee.

"Ni sahihi walinzi wetu kukaa pembeni, huyu ni kama Rais wa dunia, lakini hata majeshi yetu yanafanya kazi ya ulinzi lakini sio kwamba yatakaa nyuma tu," alisema.

SUMAYE: TUMKARIBISHE
Naye, Waziri Mkuu mstaafu, Fredrick Sumaye, alisema ziara ya Rais Obama haina ujumbe zaidi ya kuhimiza watu wajitokeze kumpokea.

Hata hivyo, Sumaye alikwepa kuzungumzia kwa undani hatua ya kuwafukuza wafanyabiashara kutoka kandoni mwa barabara, ili kupisha mapokezi ya Rais Obama.

“Ninachokielewa ni kuwa barabara ambazo wanapita viongozi kama Rais Obama zinatakiwa kuwa katikahali ya usalama na hivyo kutakiwa kuboreshwa,” alisema.

LIPUMBA: MAFANIKIO NI MADOGO KIUCHUMI
Mwenyekiti wa Chama Cha Wananchi (CUF) Profesa Ibrahim Lipumba, alisema mafanikio ya ziaraya Rais Obama yapo katika kujitangaza kimataifa kuliko kiuchumi.

Profesa Lipumba ambaye ni mchumi aliyebobea, alisema changamoto iliyopo ni kwamba bado biashara kati ya nchi mbili hizo siyo kubwa kama ilivyo kwa nchi kama China na Tanzania.

Alitolea mfano, mwaka 2012 bidhaa za hapa nchini zilizouzwa Marekani zilikuwa na thamani ya Dola milioni 66 ikilinganishwa na zile zilizouzwa China ambapo zilikuwa ni zaidi ya Dola milioni 500.

Alisema bidhaa zilizoagizwa kutoka Marekani zilikuwa na thamani ya Dola milioni 230 huku za kutoka China zikiwa na thamani ya zaidi ya Dola milioni 1,100.

"Utakubaliana nami kuwa mahusiano yetu na China ni makubwa kuliko Marekani licha ya nchi hii kutoa fursa kwetu ambazo hatujazitumia ipasavyo," alisema

Profesa Lipumba alisema Marekani kupitia mpango wake wa kusaidia Maendeleo ya Afrika (AGOA), ulitoa fursa kwa bidhaa za Afrika kuuzwa nchini humo bila ushuru, lakini Tanzania haikuitumia.

Pia alisema utawala wa George Bush, uliisaidia Tanzania kupitia Mfuko wa Changamoto za Milenia (Millenium Challenge Compact (MCC) kupewa Dola milioni 700 kwa ajili ya kusaidia miundombinu na ujenzi wa nyaya za umeme kutoka bandarini hadi Zanzibar.

"Pana uwezekano wa mpango wa pili wa MCC, Tanzania ikapata msaada wa kuimarisha miundombinu ya umeme, lakini pia kampuni za Marekani kuja kuwekeza hapa kwetu," alisema.

Alisema uwekezaji wa kampuni hizoutategemeana na wafanyabiashara wa hapa nchini pamoja na serikali kutumia fursa mbalimbali za nchi hiyo.

Katika hatua nyingine, Profesa Lipumba alisema ili nchi iweze kujikwamua na umasikini itatokana na jinsi itakavyotumia sera na juhudina siyo kutegemea msaada kutoka nje.

HOTELI ZIMEJAA
Wingi wa wageni wakiwamo watakaofika kwa ajili ya ziara ya Rais Obama, umesababisha hoteli nyingi za jijini Dar es Salaam `kujaa’.

Uchunguzi wa NIPASHE Jumapili ulibaini kwamba kwa zaidi ya wiki sasa, hoteli nyingi hazikupokea wageni kutokana na kile kilichoelezwa kuwa, nyingine zililipiwa ingawa vyumba havikutumika kwa wakati.

POLISI: WASIO NA KAZI WASIJE MJINI
Kamanda wa Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani, Mohammed Mpinga, amewataka wananchi ambao hawatakuwa na mambo muhimu ya kufanya katikati ya jiji, wasifike huko kupunguza msongamano wa watu na magari baada ya kuwasili kwa Rais Obama.

Alisema, baadhi ya barabara zitafungwa kwa muda kwa ajili ya viongozi kuzitumia, hivyo kusababisha msongamano.

Hekaheka zimetanda jijini Dar es Salaam, ikiwa ni zaidi ya saa 24 kabla ya kuwasili kwa Rais Barack Obama.

Rais Obama, atawasili nchini kesho akitokea Afrika Kusini, ambapo pamoja na mambo mengine, alizungumza katika mkutano wa ‘viongozi vijana wa Afrika’ na kujibu maswali kutoka nchi tofauti.

Mkutano huo ulifanyika jana jioni huko Soweto nchini Afrika Kusini, ambapo alipokewaa na kujibu maswali kutoka Kenya, Uganda, Nigeria na Afrika Kusini kwenyewe.

Jijini Dar es Salaam, shughuli kadhaazikiwamo za ulinzi na usalama, zinafanyika kwa kasi na umakini kuhakikisha ziara ya Rais Obama inafanyika pasipo bughudha. kujibu maswali kutoka Kenya, Uganda, Nigeria na Afrika Kusini kwenyewe.

Jijini Dar es Salaam, shughuli kadhaazikiwamo za ulinzi na usalama, zinafanyika kwa kasi na umakini kuhakikisha ziara ya Rais Obama inafanyika pasipo bughudha.

Hata hivyo, sehemu kubwa inayohusu masuala ya itifaki, ulinzi na usalama yanafanywa na taasisi za Marekani, kwa kuzishirikisha taasisi za ndani kwa kiwango kidogo.

“Hawa jamaa (Wamarekani) wanapoingia nchi yeyote wakiwa naRais wao, shughuli nyingi na uamuzi wanafanya wao, sisi wa ndani inakuwa kushirikishwa kwa kiasi kidogo,” kilieleza chanzo cha NIPASHE Jumapili kutoka moja ya taasisi zinahusika katika ziara hiyo.

Maeneo kadhaa ya jijini humo, yaliendelea kudhibitiwa kwa ulinzi mkali na doria za mara kwa mara, huku kandoni mwa baadhi ya barabara wakionekana askari wa Jeshi la Wananchi (JWTZ).

Mathalani, kandoni mwa barabara ya Morogoro, eneo la Ubungo, walionekana askari wa JWTZ maarufu kama MP.

Shughuli nyingine zimehusisha pia operesheni zinazofanywa na polisi kwa kusaidiana na mgambo wa jiji, kuhakikisha watu na bidhaa zilizopokandoni mwa barabara zitakazotumika kwa ziara ya Rais Obama, vinaondolewa.

Magari yaliyowabeba polisi wenye silaha za moto na mabomu ya machozi, yalionekana katika mitaa kadhaa jijini humu, wakihakikisha operesheni hiyo inafanyika pasipo kikwazo kutoka kwa wahusika.

Kila palipofanyika operesheni hiyo, baadhi ya askari walifanya doria zamu kwa zamu, kuhakikisha kuwa bidhaa na watu walioondolewa, hawarejei.

Hata hivyo, waathirika katika operesheni hiyo walieleza kutofurahia, huku wakihoji ni kwa nini serikali haikuwaandalia mazingira mbadala kabla ya utekelezaji wake. 

Walisema miongoni mwao, wamekopa mitaji kutoka kwenye taasisi za kifedha, hivyo kusimamisha biashara zao ili kupisha ujio wa Rais Obama, kutawaweka katika hali ngumu kiuchumi.

“Ikiwa ujio wa Rais Obama unatutesa wafanyabiashara kiasi hiki, ni vigumu kuhimili maisha yetu, kwa sababu hatujui hatma yetu baada ya yeye kuondoka,” alisema mfanyabiashara Zena Rashidi wa Kariakoo.

Hata hivyo, wamachinga walionekana jana katika kituo cha mabasi cha Mwenge walipofukuzwa, wakiwa wanaendelea na biashara zao.

Lakini walifanya hivyo kwa tahadhali ikiwamo kushika bidhaa chache mikononi, huku wakitumia 'janja' ya kupiga kelele za 'kumsifia' Rais Obama.

Walisikika miongoni mwao wakisema, 'praise to Obama' na wengine wakaitikia 'aaamen'. Walifanya hivyo zamu kwa zamu, lakini haikujulisha waliashiria nini.


BARABARA ZAPAMBWA
Aidha, barabara zote atakazopita Obama wakati wa ziara yake zimepambwa kwa bendera za Marekani na Tanzania; huku zikinakshiwa kwa picha yake ambayo imeandikwa 'President Barack Obama' karibu Tanzania.

Barabara hizo ni ile ya Nyerere kuanzia uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius K. Nyerere, Ali Hassan Mwinyi, Mwai Kibaki na Bagamoyo.

NIPASHE Jumapili imeshuhudia pichana bendera hizo zikiwa zimewekwa kwenye mabango yote yaliyo barabarani kuanzia Ikulu hadi kwenye barabara hizo huku usafi wa jiji ukionekana kuimarika zaidi.

Jana gazeti hili lilishuhudia karibu barabara zote, vijana wanaofanyakazi ya kuweka bendera na picha ya Obama wakifanyakazi hiyo.
CHANZO: NIPASHE JUMAPILI

BADO MAMBO SIYO MAMBO ZIARA YA OBAMA AFRIKA KUSINI

image

T
Ndege aina ya MARINE ONE, Ikiwa na Raisi Obama na Mkwewe Michelle ikiruka juu ya anga ya Pretoria wakati alipowasili kukutana na Raisi wa Afrika kusini Jacob Zuma
Helcopters ikiwepo Marine One zikiwa zimetua mbele Ya Jengo la Union(Union Building) Pretoria South Africa 

Kijana akiwa ndani ya Tshet yenye Picha ya Obama nje ya Hospital Ya  Medi-Clinic Heart  alipolazwa raisi wa zamani wa Africa Kusini Nelson Mandela Pretoria
Obama akijibu Maswali from kupitia "Video Mtukano" wakati alipokutana na Viongozi vijana Afrika University of Johannesburg  Soweto
MAANDAMANO BADO YANAENDELEA KUPINGA UJIO WAKE
WAANDAMANAJI WAKIKWARUZANA NA POLICE HUKO AFRKA KUSINI KUPINGA UJIO WA OBAMA
PICHA YA PAMOJA MTU NA MKEWE     MTU NA MKEWE
NA HAWA NAO WALIAMUA KUANDAMANA NYUMA YA CHUO ALICHOTEMBELEA OBAMA KUNA VICHAKA VYA KUTOSHA


US President Barack Obama and South African President Jacob Zuma give a press conference at the Union Building in Pretoria, South Africa. Zuma welcomed Barack Obama to South Africa, saying the first black US president carried with him the dreams of millions of Africans. During a landmark visit which has been overshadowed by Nelson Mandela's failing health, Zuma said Mandela and Obama were 'bound by history' as the first black leaders of their respective nations

Police use stun grenades in an attempt to disperse protesters outside the University of Johannesburg in Soweto, ahead of a visit by US President Barack Obama

A young man shows his excitement as Obama calls on him for a question

Sasha Obama and her cousin Leslie Robinson sit and listen to Michelle Obama speak at a youth event

First lady Michelle Obama waves to participants after a virtual discussion event with young people at the Sci-Bono Discovery Centre in Johannesburg

Michelle Obama hugs Tebogo Tenyan, 16, during a youth event
Obama answers questions from the audience and from people in Nigeria, Uganda and Kenya via live video link during a meeting with the young African leaders at the University of Johannesburg in Soweto

Obama toasts with his wife Michelle during an official dinner hosted by South African president Jacob Zuma at the Presidential Guest House in Pretoria

OBAMA APOKELEWA AFRIKA KUSINI NA MABANGO: KESHO ZAMU YETU TUTAMPOKEA KWA NGOMA NA VIGELEGELE

HIVI NDIVYO MAMBO YALIVYOKUWA KATIKA VIUNGA VYA MKI WA CAPE TOWN.
Waandamanaji wakiwa tayali kuanza maandamano ya Amani
Akiwa na mwenyeji wake Rais Jacob Zuma kulia kwao ni wake zao.
Moja la bango la waandamanaji likiwa chini.

Kama unavyojionea mwenyewe.
kazi kweli kweli.
Wakiyaandaa mabango .

Uku ikiwa wanakumbuka kwamba kiongozi wao wa kwanza Mweusi Mzee Nelson Mandela yuko Hospitali akiendelea kupata matibabu kutokana na hali yake kuwa mbaya Baadhi ya wananchi wa Afrika kusini walijitokeza nje ya ukumbi wa Bunge mjini Cape Town kuandamana kupinga ziara ya Rais wa Marekeni Obama,uku wakiwa na Mabango yenye kuonyesha ujumbe mbalimbali kwa rais huyo

Friday, 28 June 2013

Ujio wa Obama wazidi kutesa wakazi Dar



UJIO wa Rais wa Marekani, Barack Obama na viongozi wengine umezidi kuwa shubiri miongoni mwa wakazi wa Jiji la Dar es Salaam.

Uchunguzi wa Tanzania Daima Jumamosi umeonesha kwamba kwa siku kadhaa wananchi wamekuwa wakisumbuka kwenda makazini au kwenye shughuli zao nyingine kutokana na foleni kubwa wanazokumbana nazo barabarani, hivyo kuwalazimu baadhi yao kutembea kwa miguu.

Hali hiyo imesababisha adha kubwa pia kwa watu wenye magari binafsi, wanaolazimika kukaa muda mwingi njiani, hivyo kukwamisha shughuli zao.

Kumekuwa na msururu mrefu wa magari katika barabara nyingi ikiwemo ile ya Kilwa kutoka eneo la Bandari hadi Stesheni.

Mkazi mmoja, Onesmo Peter alisema ujio huo umeleta hasara kwa sababu umewafanya wakazi wengi kuchelewa kazini ama katika biashara zao.

“Nimetoka nyumbani eneo la Mtoni Mtongani majira ya saa 1.15 asubuhi na cha ajabu nikakwama katika eneo la Bandari kwa zaidi ya saa moja na nusu,” alisema Peter.

Dereva Juma Mtanda alilalamikia hali hiyo na kueleza kwamba kuwepo kwa foleni hizo kunatokana na miundombinu hafifu iliyopo na kuhoji sababu ya serikali kutotumia mbinu mbadala ya kuuwezesha ugeni huo kufika nchini bila kuathiri shughuli za wananchi wengine.

Neema Samora ambaye alishuka kwenye daladala akiwa na wenzake na kutembea kwa miguu ili kuwahi shughuli zake, alisema ujio wa Obama na viongozi wengine unawaweka katika wakati mgumu wa kuweza kukosa kazi kwani wengi wao hufanya kazi kama vibarua hivyo kuamua kushuka kwenye daladala na kutembea.

“Mimi binafsi leo nimeacha gari nyumbani na kulazimika kukodi pikipiki bila kupenda ili iniwahishe mjini kwani machungu niliyoyapata jana yametosha,” alisema Hadija Saidi mkazi wa Ukonga.

Amosi Petro alisema ikiwa kuna ugeni wowote unataka kuja nchini ni vyema serikali ikajipanga vizuri kuliko ilivyofanya sasa kwani kwa kiasi kikubwa imeathiri shughuli za wengine.

SUGU AMBWAGA PINDA

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Dodoma imetupilia mbali mashitaka yaliyokuwa yamefunguliwa na serikali dhidi ya Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi (CHADEMA) kwa madai ya kumtukana Waziri Mkuu Mizengo Pinda.

Akitoa hukumu hiyo, Hakimu Mfawidhi wa mahakama hiyo, Eliezel Luvanda alitupilia mbali mashitaka hayo kutokana na hati ya mashitaka dhidi ya mbunge huyo kuwa na upungufu.

Luvanda alisema kwa mujibu wa kifungu cha sheria cha 132 (20) hati hiyo haikuwa na maelezo ya kutosheleza kuonesha ni lugha gani iliyodaiwa kuwa ni ya matusi aliyotumia mshitakiwa huyo dhidi ya Pinda.

Awali akisoma hati hiyo, Mwendesha Mashitaka, Hariet Lopa alidai kuwa Juni 24 mwaka huu akiwa katika Manispaa ya Dodoma, Mbilinyi aliweka ujumbe wenye lugha ya matusi dhidi ya Waziri Mkuu Pinda kinyume cha sheria.

Kabla ya hakimu kutoa hukumu hiyo, wakili na mwanasheria wa CHADEMA, Tundu Lisu, aliwasilisha utetezi wake mbele ya mahakama hiyo akiitaka kuitupilia mbali kesi hiyo kwa vile hakuna matusi yanayotajwa yakidaiwa kutolewa na mbunge huyo dhidi ya Pinda.

Lissu alisema kuwa kwa mujibu wa kifungu cha sheria cha 132 (20), hati hiyo haikuwa na maelezo ya kutosheleza kuonesha ni lugha gani iliyotumika na ni matusi gani, hivyo haiwezi kuwa kesi ambayo inaweza kuendelea kusikilizwa.

Lissu alidai kuwa maneno yanayodaiwa yangesababisha uvunjifu wa amani hayakutajwa katika hati hiyo huku akihoji upande wa mashitaka unataka Sugu ajitetee kwa shitaka lipi.

Aliendelea kuieleza mahakama hiyo kuwa kama hati hiyo ya mashitaka iliyopelekwa mahakamani hapo itaendelea kutumika, itakuwa imekiuka sheria, hivyo akaitaka mahakama hiyo kuifuta kesi hiyo.

Hakimu Luvanda alipomtaka mwendesha mashitaka wa serikali kujibu hoja ya Lissu, alishikilia msimamo wake na kuiomba mahakama kuendelea kuisikiliza kesi hiyo kwa madai kuwa ni mpya, hivyo makosa ambayo yapo yatafanyiwa marekebisho wakati shauri likiendelea.

Hata hivyo Lissu alipinga kauli ya mwanasheria wa serikali kwa madai kuwa hati ya mashitaka ni chafu na imeandaliwa ovyo, hivyo mahakama kukubali kuendelea kusikiliza kesi hiyo ni kosa na hivyo ni vyema ikatupiliwa mbali.

“Mheshimiwa hakimu naomba kesi hii itupiliwe mbali kwa kuwa hati ya mashitaka ni chafu na ni ya ovyo. Naomba itupiliwe mbali na mtuhumiwa aachiwe huru,” alisema Lissu na kuongeza kuwa wapo tayari hata kesho kuendelea na kesi hiyo ikiwa serikali itaandaa hati sahihi.

Hata hivyo, baada ya hakimu huyo kutoa hukumu hiyo, mwendesha mashitaka alidai wataendelea na upelelezi na ukikamilika wataandaa hati mpya.

Akizungumza mara baada ya hukumu hiyo, Lissu alisema mahakama hiyo imetenda haki na kama upande wa mashitaka haukuwa umeridhika na hukumu hiyo, ujipange upya na kupeleka hati ya mashitaka.

Lissu ambaye pia ni Mbunge wa Singida Mashariki (CHADEMA) alisema hata hivyo kufutwa kwa kesi hiyo hakumaanishi mteja wake hawezi kushitakiwa tena, kwani bado Waziri Mkuu Pinda anaweza kwenda polisi kutoa maelezo kama anaona kweli ametendewa kosa hilo.

Kwa upande wake, Sugu baada ya kuachiwa huru alisema kuwa anachoshauri ni Pinda kujitafakari upya juu ya kauli zake anazozitoa hasa kuhamasisha watu kupigwa.

Awali, Sugu alikamatwa na Jeshi la Polisi mkoani hapa kwa tuhuma kuwa aliweka ujumbe mfupi katika mtandao wa kijamii ambao ulikuwa unamtusi Waziri Mkuu Pinda.

Hata hivyo, alikuwa akipelekwa katika kituo cha polisi cha kati kwa mahojiano na jana ilikuwa ni mara ya kwanza kufikishwa mahakamani

AFRIKA KUSINI:MAMIA YA WATU WAANDAMANA KUPINGA UJIO WA OBAMA

Waandamaji Nchini Afrika Kusini wakiwa wamebeba mabango yanayopinga kuja Kwa Raisi Obama nchini Humo wakati wa maandamano ya Amani ya Kupinga Kuja Kwa Obama Katika Jiji la Pretoria Nchini Afrika Jioni ya leo wakati Raisi Obama alipotua Katika Jiji Hilo leo Jioni Juni 28
Waandamaji Nchini Afrika Kusini Wakisali mbele ya Bango linalopinga Kuja kwa Raisi Obama Nchini Humo wakati Raisi Obama alipotua Nchini Afrika Kusini Jioni ya Leo Juni 28
Waandamaji wa Nchini Afrika Kusini wakiwa wanasali mbele ya Ubalozi wa Marekani wakati wa maandamano ya kupinga kuja kwa Raisi Obama Nchini Humo Mapema leo wakati Raisi Obama alipotua Nchini Humo Kwa Ziara ya Siku 2 ametokea Nchini Senegali na Kutua Nchini Afrika Kusini huku Akihitisha Ziara Yake Nchini Tanzania wiki ijayo.
Mmoja wa waandamaji nchini Afrika Kusini ambaye jina lake halikuweza kupatikana mara moja akiwa amebeba moja ya Bango ambalo Linamwita Raisi OBAMA kuwa ni Mpishi wa Ikulu ya Marekani kama linavyosomekana na kuendelea kuelezea kuwa sera za Marekani ni tatizo.Mwandamaji huyu amebeba bango leo Juni 28 wakati wa maandamo ya amani kuelekea mbele ya Ubalozi wa Marekani NChini humo kwa kupinga Kuja Kwa OBAMA Nchini Mwao.

PICHA ZA RAIS OBAMA ALIPOTEMBELEA BANDARI YA ZAMANI ILIYOKUWA IKITUMIKA KUSAFIRISHIA WATUMWA

Obamas at the 'Door of No Return': First Family makes emotional trip to former slaving port in Senegal from where captives were shipped to America 
President Obama said that the visit to the former slave trade hub was important to him as an African American and an African American President tasked with protecting human right.
The Obamas visited Goree Island's Door of No Return where the slaves would embark on their journeys across the Atlantic Ocean
Facing history: President Obama took a tour of Goree Island outside of Dakar, Senegal where slaves used to be depart on boats bound for America in the late 18th century
President Obama was accompanied to Goree Island by his wife Michelle, their eldest daughter Malia, Michelle's mother Marian Robinson and their niece Leslie
Obama peered out at the crashing waves through the island's 'Door of No Return,' at first by himself


Though the Maison des Esclaves has become a popular tourist destination, it was one of the more minor slave shipping ports in

Mrs Obama joined him at the poignant doorway, and he said that the visit helped remind them of the importance of protecting civil rights
President Obama has a sombre moment at the Door of No Return



JE UNAFAHAMU GARI YA OBAMA????ICHEKI HAPA NI HATAREEEE.










PICHA ZA MATUKIO YA KUSHANGAZA UJIO WA OBAMA TANZANIA:


BARABARA YA MOROGORO UBUNGO IKIWA INAPIGWA DEKI
Mgambo wa Jiji wakinyanganyana bidhaa na Wamachinga maeneo Ya Mwenge katika Operation ya Kuwahamisha kufuatia ujio wa Obama Tanzania

Baadhi ya wakazi na wafanyakazi wa  halmashauri wakifanya usafi wa motaro ya maji chafu.
[clip_image001%255B7%255D.jpg]
Akina mama wakifanya usafi wa kufagia barabara maeneo ya changombe.
[clip_image001%255B7%255D.jpg]

MAONI YANGU:
Kwanini usafi mpaka aje obama????
Wamachinga wamekuwapo mwenge, Ubungo, Kariakoo na maeneo mengine miaka na miaka kwanini Obama aje ndo waondolewe????