http://kariakoodsm.blogspot.com
KARIAKOO BLOG:Kwa Habari Kali Za Mjini | SIASA | BURUDANI | UCHUMI | FASHION | BLOGGER TRICKS | UDAKU | MICHEZO | WASILIANA NA MIMI|0713305567 |urassaombeni@yahoo.com|KWA| MATANGAZO| BABARI| USISITE PIA KUCOMMENT KWENYE HABARI ZETU | <div style='background-color: #de24de;'><a href='http://www.ikiloop.com/' title='link'></a></div>
Showing posts with label SIASA. Show all posts
Showing posts with label SIASA. Show all posts

Friday, 9 August 2013

SOMA JINSI MAKAMANDA WA CHADEMA WALIVYOTESWA KABLA YA KUACHIWA HURU

.
HATIMAYE makada watano wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wanaokabiliwa na shtaka la kummwagia tindikali kada wa Chama cha Mapinduzi (CCM), wameachiwa kwa dhamana na Mahakama ya Hakimu Mfawidhi Wilaya ya Igunga.

Makada hao ambao wanatetewa na mawakili Prof. Abdallah Safari na Peter Kibatala ni pamoja na Avodius Justinian (Bukoba), Oscar Kaijage (Shinyanga), Rajabu Daniel (Dodoma), Seif Magesa (Mwanza) na Henry Kileo (Dar es Salaam).

Muda mfupi baada ya kuachiwa, vijana hao walifichua jinsi walivyopata mateso makali kutoka kwa maofisa wa jeshi la polisi wakilazimishwa kuwataja viongozi wa juu wa CHADEMA, Mwenyekiti Freeman Mbowe, Katibu Mkuu, Dk. Willibrod Slaa, John Mnyika na Tundu Lissu kuwa wanahusika na ugaidi.

Bila kumung’unya maneno waliwataja vigogo kadhaa wa serikali, CCM na mbunge mmoja wa CHADEMA kuwa ndiyo waratibu wa mikakati hiyo ya kuwabambika CHADEMA kesi za ugaidi.

Vijana hao waliowasili mjini Igunga 12:45 jioni juzi na kupandishwa kizimbani katika mahakama hiyo saa 1:20 usiku na kusomewa shtaka lao la kufanya kitendo kilicholenga madhara mwilini.

Mapema hati ya mashtaka iliyowasilishwa mahakani hapo na Mwendesha Mashtaka wa Polisi, Mrakibu Msaidizi, Cosmas Mboya, makada hao walidaiwa kutenda kosa la kummwagia tindikali kada wa CCM, Mussa Tesha, usiku wa Septemba 9, 2011, katika msitu wa Hanihani, Igunga.

Mbela ya Hakimu Mfawidhi wa mahakama hiyo, Ajali Milanzi, ilidaiwa na mwendesha mashtaka kuwa washtakiwa hao kwa pamoja walimmwagia kada huyo tindikali sehemu za uso, puani, mdomoni na kwenye bega la kulia.

Mwendesha mashtaka alidai kuwa shauri hilo limekwenda wilayani Igunga baada ya Mahakama Kuu, Kanda ya Tabora, kuwafutia shtaka la ugaidi na kuamuru kwamba warejeshwe Igunga na kushtakiwa kwa kosa la kumwagia tindikali kisha wapatiwe dhamana.

“Masharti ya dhamana yaliyowekwa na mahakama ni kila mshtakiwa kuwa na mdhamini mmoja atakayesaini dhamana kwa ahadi ya sh milioni 10 za maandishi kila mmoja.

Washtakiwa wote walikana shtaka hilo na kutimiza masharti ya dhamana kisha hakimu akaiahirisha kesi Septemba 10 mwaka huu itakapotajwa tena.

Katika hatua nyingine, vifijo, nderemo, vilio vya furaha na shangwe vilitawala mahakamani hapo baada ya makada hao kuachiwa kwa dhamana.

CLICK READ MORE KUSOMA ZAIDI

Wafuasi wa CHADEMA walifanya maandamano yaliyoongozwa na msururu wa magari, pikipiki na baiskeli wakitembea umbali wa takriban kilomita tano kutoka mjini Igunga kwa lengo la kuwapokea makada hao.

Akizungumza kwa kifupi, wakili wao Peter Kibatala, aliendelea kuishukuru Mahakama Kuu Kanda ya Tabora kwa kuonyesha ujasiri wake na kutimiza majukumu yake ya kutoa haki.

“Namshukuru Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Tabora, Simon Likelerwa, kwa weledi wake wa kutoa uamuzi ulio sahihi kisheria na ulioshiba.

“Pia naipongeza mahakama ya Igunga kwa kuwapatia dhamana washtakiwa kwa masharti yanayoendana na uzito wa jambo lenyewe kwani dhamana ni haki ya msingi kwa mshtakiwa yeyote,” alisema.

Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Tabora, Kansa Mbaruku, alisema kuwa pamoja na kuridhishwa na hukumu iliyotolewa na Mahakama Kuu Kanda ya Tabora, pia hiyo ni ishara kuwa haki imezingatiwa kisheria.

Awali makada hao walifutiwa mashtaka na mahakama ya wilaya ya Igunga kisha kukamatwa tena na kupelekwa katika Mahakama Kuu Kanda ya Tabora kusomewa shtaka la ugaidi ambalo hata hivyo lilifutwa na mahakama hiyo.

Mikakati ya hujuma 

Wakisimulia kile kilichowapata tangu kukamatwa kwao hadi kufikishwa mahakamani, makada hao walisema kuwa walipata mateso makubwa huku wakilaghaiwa kupewa vyeo serikalini na fedha ili mradi wawahusishe viongozi wa CHADEMA na ugaidi.

Evodius Justinian (Bukoba)

Alisema kuwa alikamatwa Bukoba: “Nikakaa rumande siku tatu kabla ya kusafisirishwa hadi Mwanza. Nikiwa huko niliteswa sana ili nikubali kuwa ninajua ule mkanda wa Wilfred Lwakatare uliokuwa kwenye mitandao.

“Nilikataa, niliteswa sana nikahojiwa kama nilimmwagia Musa Tesha tindikali nilikataa. Nilisafirishwa kwa ndege kuja Dar es Salaam ambako nilipokelewa na polisi.

“Nikiwa uwanja wa ndege niliomba ruhusa kwenda chooni, askari walinifuata huko wakanitesa sana. Nilifanyiwa mahojiano na Advocate Nyombi na afande Pasua. Walinilazimisha nikubali kuwa viongozi wetu huwa wanafanya vitendo vya kigaidi,” alisema.

Alisema kuwa akiwa makao makuu ya jeshi la polisi, aliteswa sana kwa maelekezo ya Afande Pasua na Nyombi katika ghorofa ya nane, jengo la makao makuu ya polisi.

“Niliambiwa nieleze siri za Dk. Slaa, Mbowe, Mnyika na Lissu na niseme kuwa walihusika na vitendo vya utekaji na utesaji, nilipokataa nilipigwa shoti za umeme ili nikubali kusema.

“Walikuwa wametafuta hata waandishi wa habari wakisubiri nikubali ili wanirekodi. Nilitoa maelezo kwa kulazimishwa huku nikiteswa. Nilipata nafuu baada ya wakili wangu, Nyaronyo Kicheere, kuja ndipo nikaeleza nilivyofanyiwa ukatili,” alisema.

Alisema kuwa alisafirishwa toka Dar es Salaam hadi Igunga na kwamba kila walipopita alitambulishwa kwa makamanda wa polisi kuwa ni mtu hatari sana.

Seif Magesa (Mwanza)

Alisema kuwa alikamatwa Mwanza na mabaunsa wa Meya wa Manispaa ya Ilemela, Henry Matata, aliyefukuzwa CHADEMA, wakiambatana na Adam Chagulani ambaye pia alifukuzwa pamoja na baadhi ya maafisa wa Usalama wa Taifa.

“Nilipelekwa ofisi za Usalama wa Taifa. Nilihojiwa nikiulizwa mimi ni nani katika CHADEMA na kwa nini huwa nawasiliana na Mbowe, Dk. Slaa, Lissu au Mnyika,” alisema.

Alisema kuwa aliuzwa kama viongozi hao wanahusika na utekaji wa watu mbalimbali unaotokea nchini na alipokataa aliteswa sana kuanzia saa 3 hadi 7 usiku.

“Nilipigwa shoti za umeme kwa maelekezo ya afande Pasua. Yeye alikuwa anakuja kuniaga kuwa anaenda kunywa pombe, vijana watafanya kazi yao. Waliniambia kuwa Lwakatare alikuwa amenitaja kuwa mimi nafanya vitendo vya kigaidi. Nilikataa kata kata,” alisema.

Aliongeza kuwa Aprili 23, mwaka huu, waliwaleta mama yake mzazi, mama mkwe na mkewe huku wakimdhalilisha mbele yao lakini alikataa kubadili maelezo yake.

“Siku moja nikiwa nahojiwa simu ya afande aliyekuwa ananihoji ilikuwa karibu; kiongozi mmoja wa CCM (anamtaja) alipiga simu akisema kama nimekataa kusema lolote nipelekwe Igunga ambako nilipelekwa nikasomewa shtaka la kummwagia tindikali Musa Tesha,” alisema.

Oscar Kaijage (Shinyanga)

“Mimi nilikamatwa, nikaambiwa niwasaidie askari kufahamu wizi wa milioni 100 uliokuwa umefanyika kwa njia ya mtandao kwa kuwa mimi ni wakala wa Airtel.

“Lakini nilipokubali kwenda na askari kituoni nikawekwa chini ya ulinzi. Ghafla nikapelekwa kwa mkuu wa upelelezi akanielekeza kuwa nikapekuliwe nyumbani kwangu kama kuna silaha ya aina yoyote au chupa zenye majimaji. Nilipekuliwa hawakupata kitu. Ilikuwa yapata saa 5 mchana,” alisema.

Aliongeza kuwa ilipofika saa 12 jioni, alipelekwa tena kwenye ofisi ya mkuu wa upelelezi, akakutana na askari alioambiwa wanatoka Dar es Salaam.

“Hapo nikamkuta afande ninayemfahamu, anaitwa Pasua kwa kuwa aliwahi kufanya kazi Shinyanga na Simiyu. Walinihoji kwa nini nina namba za viongozi wa CHADEMA. Nikawaabia, ‘mbona hamuulizi za wale wa CCM?’,” alisema.

Alisema kuwa alijibiwa kuwa wanajua hana kosa ila wanataka ushirikiano aseme kuwa Mbowe, Slaa, Mnyika na Lissu wanahusika na utekaji unaotokea nchini.

“Nilikataa. Afande Pasua nikamwambia anajua kazi yangu na mimi namjua yeye ndipo wakasema sasa kwa kuwa sitoi ushirikiano nitaunganishwa kwenye kesi ya kummwagia Musa Tesha tindikali huko Igunga,” alisema.

Aliongeza kuwa alipelekwa Igunga na wakati wanahojiwa na askari wa kutoka makao makuu, walikuwa wanafanya siri hata OCD wa pale alikuwa haruhusiwi kusikia.

Rajabu Kihawa (Dodoma)

Alidai kuwa alichukuliwa Dodoma baada ya kupigiwa simu na msichana mmoja aliyedai kuwa na maagizo kutoka kwa kaka yake anayesoma naye Chuo Kikuu cha Dodoma.

“Nilikataa lakini alikuwa anapiga simu kila mara, nikaona ngoja nikamsikilize. Nilipofika kabla sijaongea naye nilikamatwa na maafisa sita wa polisi waliojitambulisha, wakaninyang’anya simu zote na kunipeleka polisi.

“Walinihoji kama najua mkanda wa Lwakatare, nikasema sijui. wakanihoji kama viongozi wa CHADEMA wanahusika na utekaji unaoendelea nchini, nako nikasema sijui,” alisema.

Alisema kuwa baada ya hapo alipelekwa na kufungiwa Chamwino siku mbili bila kupewa chakula kisha askari wakaja wakamuuliza kama amebadili msimamo.

Alitolewa akapelekwa hoteli ya Nam, ambapo aliwakuta vijana waliofukuzwa kwenye uongozi wa Bavicha (anawataja) meya mmoja wa Mwanza na diwani aliyefukuzwa CHADEMA na kijana mwingine wa chama hicho mkoa wa Pwani aliyevuliwa uongozi wa Bavicha.

“Niliombwa nikubali kupewa sh milioni 30 ili nikubali kurekodiwa nikisema kuwa Mbowe, Dk Slaa, Lissu na Mnyika wanahusika na vitendo vya kigaidi na utekaji.

“Nilikataa. Baadaye niliingizwa katika chumba kimoja cha hoteli hiyo nikakuta mbunge mmoja wa CHADEMA kutoka Kanda ya Ziwa (anamtaja) akaniambia, ‘angalia huku’ akinionyesha simu yake kuwa alikuwa akiwasiliana na Rais,” alisema.

Kihawa aliongeza kuwa aliahidiwa kupewa cheo kizuri serikalini na fedha ili mradi akubali kuwa viongozi hao wa CHADEMA wanafanya vitendo vya kigaidi.

“Nilimuuliza kwa nini alikuwa ananishauri hivi wakati yeye ni mbunge wa chama chetu. Akasema mimi nilishinda ubunge sio kwa sababu nipo CHADEMA, bali ni muhimu hata akiondoka CHADEMA.

“Nilikataa kukubali ushauri wao ndio niliambiwa napelekwa Igunga kuunganishwa kwenye kesi ya Musa Tesha,” alisema.

Henry Kileo (Dar)

Alisema kuwa alipigiwa simu na maafisa wa polisi makao makuu Juni 17, mwaka huu, wakimwarifu kuwa wanataka kufanya mahojiano naye lakini hawakusema ni kuhusu nini.

“Juni 21, mwaka huu, wakili wangu Peter Kibatala na John Mnyika (mbunge wa Ubungo) tulienda polisi makao makuu, nilihojiwa mambo mbalimbali likiwemo tukio la kummwagiwa tindikali Musa Tesha.

“Nilicheka sana kwa kuwa kabla ya kuitwa nilipata taarifa za kikao kilichofanyika Dodoma ili kuniunganisha na kesi ya ugaidi. Mahojiano yalifanyika wakati tayari kuna kesi iliyokuwa inaendelea huko Igunga,” alisema.

Kileo alisema kuwa baada ya mahojiano hayo na kuandikisha maelezo saa 11.30 jioni, polisi walimnyima dhamana na kumpeleka rumande ya kituo kikuu cha polisi alikolala.

“Jumamosi ya Juni 22, familia yangu ilikuja kunitembelea ikakatazwa lakini baadaye wakili wangu aliwasiliana na makao makuu ya polisi ndipo wakaruhusiwa kuniona.

“Juni 22, mwaka huu, nilisafirishwa kwa ndege nikapelekwa Igunga kuunganishwa kwenye kesi ya kummwagia tindikali Musa Tesha baada ya kukataa kujibu maswali ya kuwahusisha viongozi wa CHADEMA na vitendo vya utekaji vinavyotokea nchini,” alisema.

MAPYA ZAODI: KUMWAGIWA TINDIKALI WATALII ZANZIBAR


Wakati walimu wawili wa kujitolea, raia wa Uingereza, wakijeruhiwa kwa kumwagiwa tindikali, katika maeneo ya Mji Mkongwe, Shangani, Zanzibar, mapya yameibuka kuhusu walimu hao.

Kate Gee (18) na Kristie Trup (18), walivamiwa na kujeruhiwa juzi saa moja usiku, wakienda kupata chakula cha jioni.

Habari za kuaminika zilizopatikana jana jioni zinadai kuwa mmoja wa walimu hao alishawahi kushambuliwa wakati akiwa kisiwani humo wiki mbili zilizopita.

Kwa mujibu wa mmoja wa marafiki zao, Oli Cohen, mwenye miaka 21, alisema: "Katie alishambuliwa wiki mbili zilizopita na mwanamke mmoja wa Kiislamu kwa kuimba wakati wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

"Alishitushwa mno na tukio hilo - lakini hakupatwa na hofu kiasi cha kufikiria kurejea nyumbani. Akaendelea kuishi hapo kumalizia safari yake na kazi yake ya kujitolea."

Akizungumza nje ya hekalu ambalo Kirstie anaishi na baba yake Marc na mama Rochelle, rafiki mwingine aliongeza: "Wamemaliza mchezo kwa sasa, inatia wasiwasi kiasi kuhusiana na kampuni ya bima na balozi mdogo.

Naibu Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai (DCI), Yusuf Ilembo, alithibitisha jana wasichana hao kujeruhiwa kwa tindikali hiyo, na kusema ni sehemu ya vitendo vya aina hiyo ya uhalifu vinavyoendelea Zanzibar.

"Tulipata taarifa ya tukio hilo jioni baada ya watu kumaliza kufuturu eneo la Shangani mjini hapa," alisema Kamanda Ilembo.

Taarifa zilizotufikia jana baada ya kufikishwa katika Hospitali ya Aga Khan, Dar es Salaam, zilieleza kuwa wasichana hao walikwenda Zanzibar kujitolea kufundisha kwa wiki tatu na juzi walikuwa katika wiki ya pili.

Kwa mujibu wa taarifa hizo, wakati walimu hao wakienda kupata chakula cha jioni, pikipiki aina ya Vespa, ilisimama mbele yao ikiwa na vijana wawili, mmoja wao aliwamwagia tindikali walimu hao.

Mwalimu Kate kwa mujibu wa taarifa hizo, alimwagiwa kifuani na mkononi huku Mwalimu Kristie akimwagiwa usoni na hali yake ilielezwa kuwa mbaya.

Kristie anatokea Hampstead na Kate ni mwanafunzi wa zamani wa Shule ya Francis Holland mjini Chelsea.

Mama wa Kate, Nicky alisema familia hizo zinapambana kuwarejesha wanawake hao wawili nyumbani haraka iwezekanavyo.

Wachunguzi wanasema kundi la Waislamu ambao wanataka Zanzibar ijitenge kutoka Tanzania wanawezekana kuhusika na shambulio hilo lakini hakuna yeyote mpaka sasa aliyedai kuhusika na shambulio hilo.

Polisi imeanza uchunguzi wa tukio hilo, kwa nia ya kuwatia mikononi wahusika na kufikishwa katika vyombo vya sheria.

Matukio ya watu kumwagiwa tindikali ambayo sasa yanaonekana kuelekezwa kwa wageni, yanaweza kuathiri sekta ya utalii na sasa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) imepanga kujitanua zaidi kupitia masoko ya Asia na Ulaya.

Wiki iliyopita, wakati Kamishna Mkuu wa Polisi Zanzibar, Mussa Ali Mussa, alipozungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Ziwani, alisema watuhumiwa wa shambulio la tindikali kama hilo dhidi ya Katibu wa Mufti, Shekhe Fadhil Soraga na Sheha wa Tomondo, Omar Mohamed Kidevu hadi sasa hawajakamatwa.

Mwenyekiti wa Chama cha Wawekezaji kwenye Utalii Zanzibar (ZATI), Abdul Samad, aliliambia Shirika la Habari la Ufaransa (AFP), kwamba shambulio hilo linaweza kuathiri sekta hiyo Zanzibar.

Sekta ya utalii Zanzibar huchangia pato la Taifa kwa asilimia 50, huku ikichangia ajira kwa wananchi kwa asilimia 45.

Watalii kutoka Uingereza wanashika nafasi ya tatu kwa wingi Zanzibar kwa asilimia 20, wakiongozwa na Italia na Afrika Kusini.

Eneo la Mji Mkongwe linaongoza kwa kutembelewa na watalii wengi kujionea maeneo ya kihistoria na majengo ya kale kama Kanisa la Anglikana lililojengwa mwaka 1873 Mkunazini, ambalo ni kichocheo cha kuondoshwa kwa biashara ya utumwa mwaka 1907.

Rais Jakaya Kikwete alifika katika Hospitali ya Aga Khan jana mchana, ambapo alikwenda moja kwa moja katika chumba walimolazwa wasichana hao na kuzungumza nao na kupata taarifa ya maendeleo yao.

Baada ya hapo, alipita katika chumba alimolazwa Mbunge wa Bariadi Mashariki, John Cheyo na kumjulia hali na kuzungumza naye.

Akizungumza na waandishi wa habari nje ya hospitali hiyo, Rais Kikwete alisema uvamizi huo ni wa kusikitisha na kushukuru uongozi wa hospitali hiyo kwa kuwahudumia vizuri wagonjwa hao.

Rais alisema ameagiza vyombo vya ulinzi na usalama, kusaka wahusika na kuwafikisha katika vyombo vya sheria.

Kiongozi wa Shirika la Art in Tanzania, lililoleta walimu hao nchini, Bashir Ismail, alisema inaonekana shambulio hilo lililenga walimu hao kutokana na aina ya mavazi waliyovaa.

Baada ya uvamizi huo, alisema waliwasiliana na Ubalozi wa Uingereza nchini, ambao ulipeleka ndege maalumu ikawasafirisha hadi Dar es Salaam ambako waliwasili hospitalini saa nne usiku.

Alisema katika eneo la tukio, kulikuwa na wageni wengi lakini waliomwagiwa tindikali hiyo ni walimu hao ambao walivaa suruali.

Kuhusu hali yao ya afya, Ismail alisema pamoja na majeraha, lakini wote wanazungumza na wakati wowote wakipata ndege, watasafirishwa kurejea kurudi nchini mwao Uingereza kwa matibabu zaidi.

Hivi karibuni mfanyabiashara maarufu na mmiliki wa maduka ya Home Shopping Center (HSC), Said Mohamed Saad, alimwagiwa tindikali maeneo ya Msasani City Mall, Dar es Salaam na sasa yuko Afrika Kusini kwa matibabu zaidi.

Alimwagiwa saa moja usiku, na mtu ambaye hakufahamika na mara baada ya tukio hilo, mhusika alikimbia huku mlinzi wa eneo hilo akijaribu kumkimbiza bila mafanikio baada ya kuteleza na kuanguka. Hatua hiyo ilitoa mwanya kwa mtuhumiwa kutoroka eneo la tukio kwa pikipiki.

Tukio hilo lilikuja takribani wiki mbili tangu Shekhe Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, mkoani Arusha, Said Makamba kujeruhiwa usoni kwa kumwagiwa tindikali usiku akiwa nyumbani kwake

Sunday, 21 July 2013

YALIYOJIRI MKUTANO WA LUDOVICK NA WAANDISHI WA HABARI LEO


*Aelezea uhusiano wake na Mwigulu, Lwakatare 
*Asema yeye bado ni mwanachama hai wa Chadema, amkwepa Kibanda
SIKU chache baada ya Mahakama kumuachia kwa dhamana mshitakiwa mwenza wa Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Wilfred Lwakatare, Joseph Ludovick, amefunguka na kuelezea tuhuma ambazo zimekuwa zikielekezwa kwake, ikiwamo uhusiano wake na Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mwigulu Nchemba. 

Ludovick, ambaye anadaiwa kurubuniwa na Nchemba na hivyo kumrekodi Lwakatare wakipanga mipango ya kumdhuru Mhariri Mtendaji wa gazeti la Mwananchi, Denis Msaky, alijitokeza juzi katika mtandao wa kijamii wa Mabadiliko na kuomba kuulizwa jambo lolote, kwa kile kilichoonekana kutaka kujibu tuhuma ambazo zimekuwa zikielekezwa dhidi yake.

Maswali na majibu yake ilikuwa ni kama ifuatavyo; 

KUHUSU UHUSIANO WAKE NA MWIGULU

Akielezea uhusiano wake na Mwigulu baada ya kuulizwa swali na mtu aliyejitambulisha kwa jina la Abdul Dello, Ludovick alisema ni wa kawaida na kwamba haufikii kama ule wa Lwakatare na Maggid Mjengwa.

“Tumejuana kwenye mitandao ya kijamii na tukadevelop ukaribu, ilitokana na mimi kukosoa mijadala yake na kumpinga.

“Ninayo mahusiano na watu wengi tu nje ya Chadema. Mfano ni huyo Mwigullu, Sixtus Mapunda, Mbunge Kangi Lugora, nk.na sidhani kama ni dhambi hii. Wapo wengi tu wenye uhusiano kama huu. Wote hawa katika nyakati tofauti tumesaidiana mengi.

Katika swali lake lingine, Abdul Dello alihoji: “Ludo, Mwigulu Nchemba alithibitika kukutumia m-pesa ya elfu 50 ilikuwa ya kazi gani?

Ludovick alijibu akieleza kuwa: “Nilikuwa na tatizo binafsi la kifamilia, nilihitaji msaada.”

KUHUSISHWA NA USALAMA WA TAIFA
Mtu mwingine aliyejitambulisha kwa jina la Hamis Hamad alimuuliza akisema: 

“Ludo, unasemwa sana mtaani kuwa wewe ni TISS Agent (wakala wa usalama wa taifa) uliyepachikwa pale Chadema kwa ajili ya kuiua kifo cha kawaida na ndiyo maana unafanya kazi nyingi za kujitolea badala ya kwenda kufundisha kama taaluma yako ya ualimu inavyokuruhusu, kweli?

Majibu ya Ludovick yalikuwa hivi: “Nchi hii tunapenda majungu tuuu, na magazeti yetu yamebobea kusambaza majungu na kupakazia watu. Huwezi kuelewa dhana hii hadi ikukute. Juu ya kazi ni tofauti za kimtazamo, so wengine wanapenda kuajiriwa na wengine hawapendi, so haicount hii. Ni uamuzi tu. Niliijua Chadema 2006 na kujiunga rasmi 2009. Hakuna aliyenipachika huko. Ni by conviction, nakuhakikishia hata matatizo yote ninayoyapata ni kwa sababu ya Chadema.”

AELEZA ANAVYOMFAHAMU LWAKATARE

Boniface Magessa alimuuliza hivi: “Ludovick, elezea kidogo unavyomfahamu Lwakatare. Siku ya tukio la kurekodiwa ulikuwa wapi? Kama mlikuwa wote siku hiyo, ulikaa mbele yake au nyuma yake?

Ludovick: “Magessa, Lwakatare tumekutana Bukoba 2010 wakati wa kampeni. Tumefahamiana kwa sababu ya Chadema tu. Na ameendelea kuwa rafiki yangu na kiongozi wangu.

Siku ya tukio la kurekodiwa nilikuwa nyumbani kwake Lwakatare. Siyo muhimu juu ya location”.

MASWALI MENGINE 
Leila Sheikh alimuuliza hivi; “Ludo, eti uliwahi kuruka ukuta usiku fulani?

Ludovick: “Da Leilah umefunga wewe? Sasa haya ya kuruka ukuta usiku fulani ni nini tena? Teh teh, hebu fafanua? Marcois, siku hizi kibwagizo changu ni kuwa natazama yote haya nayo ni ubatili mtupu, ni sawa na kufukuza upepo”.

Swali lake lingine lilisomeka hivi: “Kama wewe ni mwanachama hai wa Chadema kwa nini umeitwa 'msaliti' na shabiki wa Chadema kuwa ile kanda ya Lwakatare ulitumwa na Mwigulu kuipiga? Je, ile kanda ni ya kweli?

Inadaiwa kuwa ile kanda inaonesha nia/mpango wa kumuumiza Msacky.

Katika majibu yake Ludovick naye alijibu “Leila, mimi ni Mwanachadema hai. Kuitwa msaliti ni hali halisi ya sasa. Lakini inawezekana kuwa mimi wanayeniita msaliti, siku moja wakaona kuwa ndiye mwokozi. Fikiria kama ningekuwa natumika kama mnavyosema, kwa nini kesi ya ugaidi imefutwa? Si ningesema tu kuwa kulikuwa na watu wengine kadhaa? Kama ninatumika, kwa nini nikamatwe Iringa na kusafirishwa usiku tena chini ya ulinzi mkali? Leila teh teh kwamba nilitumwa kurekodi ile kanda!!! Yaani na Lwakatare naye akatumwa ili aongee haya tunayotuhumiwa kuyapanga? Na je, suala hili ikionekana kuwa ni kweli Lwakatare alilifanya, nani atakuwa msaliti kwa Chadema? Je, chama chetu kinazo sera za kudhuru waandishi? Sasa msaliti ni yule anayechafua chama kwa kupanga mambo yasiyoendana na sera za chama? Au ni yule anaye kilinda chama? Haya si nyote mnajua concept ya whistle blowers? Hamtegemei wawemo ndani ya Chadema? 

Na je, kama Mahakama itaamua kuwa tuhuma zetu ni kweli bila chembe ya shaka, ninyi mtaendelea kusema nini, kuwa mimi msaliti au wote sasa tutakuwa wasaliti? Naomba tuachie mahakama suala hili. Kuitwa msaliti wakati unaumia kwa ajili ya hao wanaokuita wasaliti, kibinadamu inaumiza sana. Na hilo ndilo linanitokea.

Kuhusu kwa nini watu wote wananilaumu, si kweli. Wapo wasioona hivyo, ila in a great party propaganda chafu za CCM na za Chadema zimenifanya muhanga wa mambo haya. Uhusiano wangu na Lwakatare kwa sasa ni wa mashaka sana. 

Swali jingine la Sheila ni hili: “Je, wewe bado mwanachama wa Chadema? Kama ndiyo, mbona walikutema kwa muda ukakaa rumande bila dhamana? Kwa nini wewe ambaye ni volunteer wa Chadema ulikanwa pale baada ya kushikiliwa na polisi? Huo ndiyo u****wa kafara.

Alijibu hivi: “Mimi ni mwanachama wa Chadema na nakuhakikishia mateso yote ninayoyapata ni kwa sababu ya Chadema.

Masharti ya dhamana hayakuwa wadhamini wawekwe na Chadema, bali watu wawili. Sasa sidhani kama Chadema walikuwa na kesi mahakamani hadi watafute wadhamini. Kuhusu kuwa volunteer wa Chadema ni majungu niliyoyazungumza. Sijawahi kuwa volunteer wa Chadema. Mimi ni mwanachama wa kawaida.

Nyoni Magoha alimuuliza hivi: “Wewe bado una imani na Chadema? Utaendelea kuwa mwanachama hai au umeshajitoa/utajitoa?

Majibu ya Ludovick: “Ninayo imani kubwa sana na isiyotetereka kwa Chadema. Nitaendelea kuwa mwanachama hai”.

Hata hivyo, Ludovick ambaye anatajwa kuhusika na tukio la kutekwa na kujeruhiwa kwa Mhariri Mtendaji Mkuu wa New Habari (2006) Ltd, Absalom Kibanda, alikwepa kuzungumzia jambo hilo na hata alipoulizwa baadhi ya maswali yenye mwelekeo huo.

Kuhusishwa Ludovick na tukio la Kibanda kunatokana na utata wa kauli na mwenendo wake siku ambayo Mhariri Mtendaji huyo alijeruhiwa.

Saturday, 13 July 2013

HATUA KWA HATUA SAFARI YA NASSARI TOKA DAR NA MIZINGUO YA JESHI LA POLISI HADI HOME


Jana Julai 10, 2013 Mbumge wa Arumeru Mashariki (CHADEMA) alirudi Jimboni kwake tokea Dar es Salaam alikokuwa akipatiwa matibabu kufuatia kipigo alichopata wakati wa uchaguzi wa diwani Kata ya Makuyuni.
Ratiba ya kurejea kwake ilihusiha mapokezi ya ndugu, jamaa, marafiki na watu wa Chadema kuanzia uwanja wa mdogo wandege Arusha na baadae kufanya mkutano wa hadhara Jimboni kwake eneo la Liganga - Usa River.
Bahati mbaya raiba hiyo haikuweza kukamilika baada ya Jeshi la Polisi luweka zuio la kutokuwako mkutano wana shamrashamra za mapokezi kwa mtu yeyete kwasababu za kuwako kwa chaguzi za udiwani Arusha Mjini keshokutwa Jumapili Julai 14, 2013.
Maandalizi ya zuio la Jeshi la Polisi yalianza asubuhi kwa kuweka utepe kuzunguka eneo walilotenga katika uwanja wa ndege Arusha na skari wenye silaha wakilinda na pia kusambaza gari la majii ya kuwasha na askari wengi kulinda viwanja vya wazi Usa River wakiwa na mabomu, bunduki, mbwa na farasi.
Kwa kiasi kikubwa zuio hilo la Polisi lilipokelewa vyema na maelfu ya watu wa Chadema waliokuwa wameshajpanga kwa wingi kumpokea Mbunge Nassari na kuhudhuria mkutano wake wa Arumeru Mashariki.
Mh Nassari aliwasili uwanja wa ndege Arusha majira ya mchana na kupokelewa na watu walionea gari mbili tu zilizoruhusiwa na Jeshi la Polisi, saloon moja na Jeep ya wazi iliyombeba nassari.
Msafara wa gari hizo mbili za Nassari ulisindikizwa kwa ulinzi mkali na magari (Landcruiser) za Jeshi la Polisi kwa nyuma na mbele zikiwa zimesheheni askari wenye silaha kali hadi ofisi kuu za Chadema zilizopo Ngarenaro Arusha. Nassari akaingia ofisini askari wakapaki pembeni kuendelea kulinda walichoagizwa kulinda.
Njiani kulikuwa na wananchi baadhi wenye magari na bodaboda waliotaka kuunga msafara lakini kabali ya Polisi iliwafanya wasiweze kuunga msafara huo.
Katika ofisi za Chadema walikuwepo wanachama kiasi na viongozi wa Chama ngazi ya Mkoa na Kanda, sambamba na Mbunge wa Arusha Mjini Mh Lema na waandishi wa habari, wote wakimsubiri Nassari wampokelee ofisini hapo baada ya kuzuiwa uwanja wa ndege. Pia walikuwapo wagombea udiwani wa Kata za Kaloleni na Elerai ambao walitangazwa na watu wa CCM kuwa wamejitoa ili kuwahadaa.



Press Conference


Mh Nassari aliongea na waandishi wa habari ofisini hapo na kueleza kwa ufupi maumivu yake na kipigo alichopata na kudai kuwa aliumia zaidi uti wa mgongo.
Nassari akasema kwa sasa yuko salama na mzima wa faya na atashiriki kwa ukamilifu katika chaguzi za udiwani na ataongoza kikosi maalumu kwa Kata mojawapo kulinda kura za Chadema isiibiwe hata moja kama sheria zinavyoagiza ili haki itendeke.
Nassari alishangazwa na kulaani uamuzi wa Jeshi la Polisi kumfuatiliatangia uwanja wa ndege wa Dar es Salaam na kisha kumzuia kabisa asionane na watu wake ilhali wanajua Arumeru kwake ni Mamlaka tofauti na Arusha Mjini na yeye ni mbunge wa kuchaguliwa na watu hao na ametoka katika matibabu.
Baadae Mbunge wa Arusha Mjini akapewa nafasi ya kuzungumza na kuanika bayana mtego waliokuwa wameemtegea Mwigulu Nchemba kwa kili kilichoelezwa mnamo Juni 12, 2013 alifanya mpango wa kumrubuni mgombea wa Chadema Kata ya Elerai, Eng Mpinga kujitoa kwa kumdanganya kuwa yeye Mwigulu alikuwa ametumwa na Rais Kikwete na kwamba angekubali angepewa Ukuu wa Wilaya au cheo chochote ambacho angetaka. Lema anasema mtego huo ni kama Mwigulu aliushitukia na kwamba kama angeingia kwenye 18 angefanywa kitu mbaya.
Lema aksema Chadema kama chadema wanarudisha Kata zote nne na wamejipanga kwa kila hila kuhakkisha hakuna dhuluma itakayofanikiwa, ikiwemo zoezi alilodai linafanywa na maofisa wa Tume ya Uchaguzi walioko Jijini Arusha kujaribu kubadilisha majina ya daftari la wapiga kura.
Mh Lema alitanabaisha kuwa nae ataongoza kiksoi maalumu kwa usalama wa kura za chadema kwa Kata mojawapo na kwamba kuna baadhi ya wabunge wa Chadema watakuja Arusha kuapishwa kama mawakala na watashiriki uchaguzi huo kuhakikisha hakuna haki yao itakayodhulumiwa. Pia makamanda wao waliokuwa mikoani kama Ally Banaga na Alphonce Mawazo na wengine watarudi kuungana na wengine kuongeza nguvu ya ulinzi.Watakaofanya vurugu wapewe kichapo
Lema akatahadharisha kuwa kuna watu wameandaliwa kufanya vurugu wakivalishwa alama za Chadema ili ionekane ni Chadema. Lema akasema yeyote atakaefanya vurugu sio mtu wa Chadema na atashushiwa kipigo bila kujali amevaa magwanda ama kitu gani na kwamba watu wa Chadema watatambua na alama wanazozijua siku hiyo. Amewataka watu wote wa Chadema kuwa wapole lakini jasiri ili wasiwape mwanya CCM kutimiza hila zao.



Eng Mpinga akanusha kuhamia CCM, amdharau Mwigulu Nchemba


Mgombea wa Chadema Kata ya Elerai, Eng Jeremiah Mpinga akajitokeza mbele ya kamera za waandishi wa habari na kukanusha propaganda za Mwigulu Nchemba akimtumia kijana aliyefukuzwa Chadema, Mtela Mwampamba kupitia mitandao ya kijamii (facebook na Jamii Forum) wakidai yeye Mpinga amkubaliana nao kuhamia CCM.Eng Mpinga akasema amemdharau sana Mwigulu Nchemba na akasema hakuwahi dhani ni mpuuzi kiasi hicho kwasababu Mwigulu aliomba kuonana ane Mpinga mapema mwezi Juni, kwanza kwa kupitia viongozi wa Wilaya Arusha na baadae mawasiliano yalivyoendelea ndipo Mwigulu mwenyewe akajitokeza kwa namba yake 0714 008888 kuomba waonane akidai ana maagizo ya Kikwete. Mzee Mpinga akasema Mwigulu ni kama ndugu yake kwasababu wanatoka maeneo jirani huko Singida na wanafahamiana. Alipomuomba kuonana nae alimkubalia kama ndugu na alikataa kukutana maeneo mengine zaidi ya nyumbani kwake.Eng Mpinga akatanabaisha kuwa japo aliona ngumu kwenda nyumbani kwake, alilazimika kufika siku ya Juni 12, 2013 akiwa ameambatana na Mtela Mwampamba. Mzee Mpinga kwa kujihami kiusalama alibaki sebuleni kwake na red brigade mmoja na alikuwa nae sebuleni. Mwigulu alipofika akahoji huyo ni nani na kutaka aondolewe aliambiwa na mtoto wa familia na hapo ni kwake ahawezi kuondoka.Ndipo Mwigulu Nchemba akaanza kubembeeza kwa hadaa kwamba ametumwa na Rais Kikwete kumuomba Eng Mpinga ajitoe Chadema na atapatiwa cheo au kazi yeyeote ikiwemo ukuu wa Wilaya.Mzee Mpinga akamchomolea Mwigulu katakata na Mwigulu akaondoka na kusema "Kaa ujifikirie, ukipata jibu nijulishe... Sisi (CCM) ndio tuna Serikali tunaweza kufanya chochote..)Picha iliyowekwa Facebook na mtumishi wa Mwigulu ilipigwa kwa siri kwasababu Eng Mpinga anasema hakukuwa na tukio la wazi la kupiga picha.



Katibu wa Kanda awashukia Polisi


Nae Katibu wa Kanda ya Kaskazini Chadema, Mh Amani Golugwa amelitaka Jeshi la Polisi kutumia kiherehere kile kile walichokitumia kumkamata Mh Joseph Mbilinyi (Sugu) kwa kile alichoandika Facebook kuwa waziri mkuu ni -------- kuagiza wananchi wapigwe tu, basi wa wamkamate pia aliyesambaza picha na maelezo ya uongo huko Facebook na Jmii Forums kuwa mgombea wa Chadema amejitoa ilhali wanajua kampeni zimepigwa marufuku na Tume na taarifa yake sio ya kweli..



Safari ya Nassari kuelekea Arumeru


Baada ya kikao na waandishi wa habari Nassari na msafara wake wa gari mbili walondoka ofisini hapo kuelekea Arumeru. Defenda za Polisi zikawaunganishia tena kukaba msafara. Ilikuwa ni kama vile gaidi osama analindwa asitoroke.
Msafara ulikatiza Kilombero, Desemba, Seliani na hadi unafika mataa ya Mianzini tayari kundi kubwa la magari, boda boda n.k waliunga msafara na Polisi wasijue la kufanya. Wananchi waliokuwa pembezoni mwa barabara walishangilia sana kwa miluzi na makelele kila mahali Nassari alikopita pamoja na kukabwa na askari polisi.
Baadhi ya magari binafsi yaliyounga msafara kilazima yalianza kujiachia mojamojakuanzia Philips yakabaki magari kama manne hivi ambayo yalikuwa ni kutoka Arumeru. Polisi nao wakiwa nyuma, msafara ukikimbia nao wanakimbia..
Gari ya Polisi kutoka Arusha ilipokelewa na gari nyingine iliyokuwa imejiandaa kwa kazi hiyo, ya Arusha ikaishia maeneo ya Tengeru.
Maeneo ya Makumira kulikuwa na gari jingine landcruiser lenye askari walio tayari kwa mapambano na mabomu yao wametega mahali pembeni ya njia.
Nassari na watu wake wakafika Leganga Usa River na kushukia njia ya vumbi kulia kufuata ilikokuwa gari ya matangazo ya Chadema maeneo ya Ngaresero iliyokuwa ikiwatangazia watu kuwa mkutano wake umeahiriswa hadi watakapotangaziwa tena.
Hapo Leganga askari Polisi walikuwa wameziba kabisa njia inayoingia uwanja wa Shule ya Msingi Leganga, baada ya kuona Nassari ameingia njia ya vumbi nao wakaunganishia kwa nyuma kumfuata.. Baade kidogo landcruiser 2 zilizosheheni askari na silaha zao wakaunga msafara tena kumfukuzia Nassari.
skari wengine kwenye Landcruiser na silaha waliziba njia ya kuingilia uwanja mwingine wa Ngarasero pale Usa River, wananchi wakiwa wametanda barabarani washangaa..
Nassari akiwa kwenye gari ya wazi alikutana na barrier ya Polisi baada ya kuvuka daraja Fulani kama mita 150 hivi kabla ya kuingia Usa River halisi kupitia Old Moshi road (sasa Mandela Road). Barrier hii iliongozwa na Mkuu wa Kituo cha Polisi Usa River ..kama sijakosea ni Mussa Sindi Huya
Kufikia hapo hali ilianza kuwa mbaya, Polisi walikomaa Nassari waondoke nae bila mtu mwingine yeyote. Nassari nae hataki. Mabishano yakawa makali sana kiasi cha askari wote kushuka kwenye magari yao na kuwazingia Chadema huku silaha zao zikiwa tayari tayari kwa lolote. Punde kidogo gari 2nyingine 2 za Polisi zikaongezeka na kupaki mwanzo wa daraja, Nassari na Chadema wake wakawa wamewekwa Kati huku mabishano yanaendelea. Watu wa Chadema waliokuwa nje ya magari ni reed brigade peke waliokuwa kwenye gari ya wazi..wengine walikuwa ndani ya magari yao kama matatu wakisubiri hatma ya hali ile.
Wakati Mkuu wa Kituo yuko bize kuwasiliana na Nassari nae alikuwa busy pia kuwasiliana na wote wakimaliza kila mmoja anadai ameelekezwa hivi na ndicho kilicho sahihi. Kiongozi huyo wa Polisi alionekana kama anapokea maagizo fulani kila anapoambiwa taarifa mpya na Nassari kutoka mahali Fulani..
Nassari akawaambia kama ni vipi aende mwenyewe kwa mguu hadi Ofisini kwake na hao wenzake warudi. Polisi wakakataa, wanataka waondoke nae wao.
Baada ya mzozo kutokuwa na muafaka na dalili ya hali kuchafuka zaidi, magari yote yaliamriwa kugeuza kurudi yalikotoka. Madereva wakatii na kugeuza lakini kusogelea darajani wakakuta gari za Polisi zimeziba, wao wako kati na dalili ya Polisi kukinukisha iko wazi..
Nassari akapanda boda boda na kuondoka eneo hilo, hatua hiyo ikawalazimu Polisi kuwasha landcruiser zao na kuanza kumfukuzia na hapo kutoa mwanya kwa gari zilizokuwa ziimewekwa kati kugeuza tena kwa kasi ya ajabu na kupenya huku nyingine zikikatiza kwenye mahindi ya watu na kutimka lakini wakakutana na kizuizi kingine cha Polisi inapotokea Mandela road kuunga na barabara kuu ya Moshi Arusha.
Nassari alifika mahali huku anafukuzziwa na askari Polisi akaacha ile bodaboda akaingia kwenye Suzuki iliyokuwa na Katibu wake, Toti Ndonde akiwa na watu wengine wawili. Wale watu wengine walishatawanyika kila mtu na njia yake.
Askari Polisi waliendelea kuifukuzia Suzuki hiyo hadi ikafikia mahali Nassari akashuka na kuwaluliza wanamfuatilia nini hivyo? Askari wale wakajibu yeye aendelee na shuguli zake wao wanayao. Nassari akarudi garini safari ikaendelea. Sasa alikuwa anaelekea shambani kwake anakojenga nyumba yake. Polisi bado wanamfukuzia.
Nassari akafika restaurant fulani akaamua kushuka kwenye gari aende chooni kujisaidia, Polisi bado wamekaba.
Nassari akaenda hadi kwenye nyumba yake anayojenga, akakagua mambomambo hapo.. Polisi bado wamekaba na landcruiser lao. Kha!
Baada ya kutoka maendeleo ya kazi ya ujenzi na kuona hali ya kufuatwa inaendelea, ikabidi dereva akaimbize gari na kuwapotezea vichochoroni.HII NDIO KAZI YA JESHI LA POLISI KWA SASA… WAKATI WAHALIFU WANAKULA RAHA WAO WANAHANGAIKA NA WATU WEMA TENA VIONGOZI WAKUBWA KABISA!!

Sunday, 30 June 2013

OBAMA APOKELEWA AFRIKA KUSINI NA MABANGO: KESHO ZAMU YETU TUTAMPOKEA KWA NGOMA NA VIGELEGELE

HIVI NDIVYO MAMBO YALIVYOKUWA KATIKA VIUNGA VYA MKI WA CAPE TOWN.
Waandamanaji wakiwa tayali kuanza maandamano ya Amani
Akiwa na mwenyeji wake Rais Jacob Zuma kulia kwao ni wake zao.
Moja la bango la waandamanaji likiwa chini.

Kama unavyojionea mwenyewe.
kazi kweli kweli.
Wakiyaandaa mabango .

Uku ikiwa wanakumbuka kwamba kiongozi wao wa kwanza Mweusi Mzee Nelson Mandela yuko Hospitali akiendelea kupata matibabu kutokana na hali yake kuwa mbaya Baadhi ya wananchi wa Afrika kusini walijitokeza nje ya ukumbi wa Bunge mjini Cape Town kuandamana kupinga ziara ya Rais wa Marekeni Obama,uku wakiwa na Mabango yenye kuonyesha ujumbe mbalimbali kwa rais huyo

Friday, 28 June 2013

SUGU AMBWAGA PINDA

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Dodoma imetupilia mbali mashitaka yaliyokuwa yamefunguliwa na serikali dhidi ya Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi (CHADEMA) kwa madai ya kumtukana Waziri Mkuu Mizengo Pinda.

Akitoa hukumu hiyo, Hakimu Mfawidhi wa mahakama hiyo, Eliezel Luvanda alitupilia mbali mashitaka hayo kutokana na hati ya mashitaka dhidi ya mbunge huyo kuwa na upungufu.

Luvanda alisema kwa mujibu wa kifungu cha sheria cha 132 (20) hati hiyo haikuwa na maelezo ya kutosheleza kuonesha ni lugha gani iliyodaiwa kuwa ni ya matusi aliyotumia mshitakiwa huyo dhidi ya Pinda.

Awali akisoma hati hiyo, Mwendesha Mashitaka, Hariet Lopa alidai kuwa Juni 24 mwaka huu akiwa katika Manispaa ya Dodoma, Mbilinyi aliweka ujumbe wenye lugha ya matusi dhidi ya Waziri Mkuu Pinda kinyume cha sheria.

Kabla ya hakimu kutoa hukumu hiyo, wakili na mwanasheria wa CHADEMA, Tundu Lisu, aliwasilisha utetezi wake mbele ya mahakama hiyo akiitaka kuitupilia mbali kesi hiyo kwa vile hakuna matusi yanayotajwa yakidaiwa kutolewa na mbunge huyo dhidi ya Pinda.

Lissu alisema kuwa kwa mujibu wa kifungu cha sheria cha 132 (20), hati hiyo haikuwa na maelezo ya kutosheleza kuonesha ni lugha gani iliyotumika na ni matusi gani, hivyo haiwezi kuwa kesi ambayo inaweza kuendelea kusikilizwa.

Lissu alidai kuwa maneno yanayodaiwa yangesababisha uvunjifu wa amani hayakutajwa katika hati hiyo huku akihoji upande wa mashitaka unataka Sugu ajitetee kwa shitaka lipi.

Aliendelea kuieleza mahakama hiyo kuwa kama hati hiyo ya mashitaka iliyopelekwa mahakamani hapo itaendelea kutumika, itakuwa imekiuka sheria, hivyo akaitaka mahakama hiyo kuifuta kesi hiyo.

Hakimu Luvanda alipomtaka mwendesha mashitaka wa serikali kujibu hoja ya Lissu, alishikilia msimamo wake na kuiomba mahakama kuendelea kuisikiliza kesi hiyo kwa madai kuwa ni mpya, hivyo makosa ambayo yapo yatafanyiwa marekebisho wakati shauri likiendelea.

Hata hivyo Lissu alipinga kauli ya mwanasheria wa serikali kwa madai kuwa hati ya mashitaka ni chafu na imeandaliwa ovyo, hivyo mahakama kukubali kuendelea kusikiliza kesi hiyo ni kosa na hivyo ni vyema ikatupiliwa mbali.

“Mheshimiwa hakimu naomba kesi hii itupiliwe mbali kwa kuwa hati ya mashitaka ni chafu na ni ya ovyo. Naomba itupiliwe mbali na mtuhumiwa aachiwe huru,” alisema Lissu na kuongeza kuwa wapo tayari hata kesho kuendelea na kesi hiyo ikiwa serikali itaandaa hati sahihi.

Hata hivyo, baada ya hakimu huyo kutoa hukumu hiyo, mwendesha mashitaka alidai wataendelea na upelelezi na ukikamilika wataandaa hati mpya.

Akizungumza mara baada ya hukumu hiyo, Lissu alisema mahakama hiyo imetenda haki na kama upande wa mashitaka haukuwa umeridhika na hukumu hiyo, ujipange upya na kupeleka hati ya mashitaka.

Lissu ambaye pia ni Mbunge wa Singida Mashariki (CHADEMA) alisema hata hivyo kufutwa kwa kesi hiyo hakumaanishi mteja wake hawezi kushitakiwa tena, kwani bado Waziri Mkuu Pinda anaweza kwenda polisi kutoa maelezo kama anaona kweli ametendewa kosa hilo.

Kwa upande wake, Sugu baada ya kuachiwa huru alisema kuwa anachoshauri ni Pinda kujitafakari upya juu ya kauli zake anazozitoa hasa kuhamasisha watu kupigwa.

Awali, Sugu alikamatwa na Jeshi la Polisi mkoani hapa kwa tuhuma kuwa aliweka ujumbe mfupi katika mtandao wa kijamii ambao ulikuwa unamtusi Waziri Mkuu Pinda.

Hata hivyo, alikuwa akipelekwa katika kituo cha polisi cha kati kwa mahojiano na jana ilikuwa ni mara ya kwanza kufikishwa mahakamani

AFRIKA KUSINI:MAMIA YA WATU WAANDAMANA KUPINGA UJIO WA OBAMA

Waandamaji Nchini Afrika Kusini wakiwa wamebeba mabango yanayopinga kuja Kwa Raisi Obama nchini Humo wakati wa maandamano ya Amani ya Kupinga Kuja Kwa Obama Katika Jiji la Pretoria Nchini Afrika Jioni ya leo wakati Raisi Obama alipotua Katika Jiji Hilo leo Jioni Juni 28
Waandamaji Nchini Afrika Kusini Wakisali mbele ya Bango linalopinga Kuja kwa Raisi Obama Nchini Humo wakati Raisi Obama alipotua Nchini Afrika Kusini Jioni ya Leo Juni 28
Waandamaji wa Nchini Afrika Kusini wakiwa wanasali mbele ya Ubalozi wa Marekani wakati wa maandamano ya kupinga kuja kwa Raisi Obama Nchini Humo Mapema leo wakati Raisi Obama alipotua Nchini Humo Kwa Ziara ya Siku 2 ametokea Nchini Senegali na Kutua Nchini Afrika Kusini huku Akihitisha Ziara Yake Nchini Tanzania wiki ijayo.
Mmoja wa waandamaji nchini Afrika Kusini ambaye jina lake halikuweza kupatikana mara moja akiwa amebeba moja ya Bango ambalo Linamwita Raisi OBAMA kuwa ni Mpishi wa Ikulu ya Marekani kama linavyosomekana na kuendelea kuelezea kuwa sera za Marekani ni tatizo.Mwandamaji huyu amebeba bango leo Juni 28 wakati wa maandamo ya amani kuelekea mbele ya Ubalozi wa Marekani NChini humo kwa kupinga Kuja Kwa OBAMA Nchini Mwao.

PICHA ZA RAIS OBAMA ALIPOTEMBELEA BANDARI YA ZAMANI ILIYOKUWA IKITUMIKA KUSAFIRISHIA WATUMWA

Obamas at the 'Door of No Return': First Family makes emotional trip to former slaving port in Senegal from where captives were shipped to America 
President Obama said that the visit to the former slave trade hub was important to him as an African American and an African American President tasked with protecting human right.
The Obamas visited Goree Island's Door of No Return where the slaves would embark on their journeys across the Atlantic Ocean
Facing history: President Obama took a tour of Goree Island outside of Dakar, Senegal where slaves used to be depart on boats bound for America in the late 18th century
President Obama was accompanied to Goree Island by his wife Michelle, their eldest daughter Malia, Michelle's mother Marian Robinson and their niece Leslie
Obama peered out at the crashing waves through the island's 'Door of No Return,' at first by himself


Though the Maison des Esclaves has become a popular tourist destination, it was one of the more minor slave shipping ports in

Mrs Obama joined him at the poignant doorway, and he said that the visit helped remind them of the importance of protecting civil rights
President Obama has a sombre moment at the Door of No Return



JE UNAFAHAMU GARI YA OBAMA????ICHEKI HAPA NI HATAREEEE.










PICHA ZA MATUKIO YA KUSHANGAZA UJIO WA OBAMA TANZANIA:


BARABARA YA MOROGORO UBUNGO IKIWA INAPIGWA DEKI
Mgambo wa Jiji wakinyanganyana bidhaa na Wamachinga maeneo Ya Mwenge katika Operation ya Kuwahamisha kufuatia ujio wa Obama Tanzania

Baadhi ya wakazi na wafanyakazi wa  halmashauri wakifanya usafi wa motaro ya maji chafu.
[clip_image001%255B7%255D.jpg]
Akina mama wakifanya usafi wa kufagia barabara maeneo ya changombe.
[clip_image001%255B7%255D.jpg]

MAONI YANGU:
Kwanini usafi mpaka aje obama????
Wamachinga wamekuwapo mwenge, Ubungo, Kariakoo na maeneo mengine miaka na miaka kwanini Obama aje ndo waondolewe????

Thursday, 27 June 2013

PICHA MBALIMBALI MAPOKEZI YA OBAMA SENEGAL




CHUO KIKUU HURIA KUMTUNUKU OBAMA DEGREE YA UZAMIVU (PHD):

Makamu Mkuu wa Chuo Kukuu Huria Prof. Tolly Mbwete



Kufuatia ujio wa Rais wa Marekani Barrack Obama nchini Tanzania Chuo Kikuu Huria cha Tanzania kimeamua kumtunukia Rais huyo Shahada ya heshima Uzamivu (PHD). 

Hayo yamesemwa na Makamu Mkuu wa Chuo hicho Prof. Tolly Mbwete ambaye aliongeza na kusema kwamba tayari Mkuu wa Chuo hicho Dr. Asha Rose Migiro ameshapewa taarifa hiyo na kuikubali kwahiyo kinachofuata ni kusubiri ujio wa rais Barack Obama ili waweze kumtunukia Shahada hiyo ya Heshima kutokana na juhudi zake za kupigania maendeleo ya jamii.

BARABARA YA OCEAN ROAD KUITWA OBAMA ROAD:
Manispaa ya ya Kinondoni kwa kushirikiana na ya ilala wamesema wapo mbioni kuibadili barabara ya Ocean Road na kuwa Barak Obama Road.....

MAMBO YAMEIVA UJIO WA OBAMA: MANDEGE NA WALINZI WAANZA KUTUA

Baadhi ya Helkoper za kijeshi toka Marekani ambazo zinadaiwa Baadhi zimeanza kutua kwenye Air Port ya Zanzibar na Dar na KIA kwa ajili ya kuimarisha usalama wa Rais wa nchi hiyo.



AIRFORCE ONE YA RAIS WA MAREKANI IKISINDIKIZWA NA NDEGE MAALUM ZA JESHI

SECURITY RING(MZUNGUKO) WA WALINZI KUMLINDA RAISI
Ndege maalum ya kivita itasindikiza Air Force One ya Rais Barak Obama
Askari maalum (MARINES) wa kulinda ndege ya Rais
Helkoper zitasambaa jiji zima la Dar kuanzi wiki hii hadi tarehe 2 Julai atakapoondoka Rais
Sasa kazi imeaaza ndivyo tunavyoweza kusema kwa sasa. Ambapo ndege na Helkoper za kijeshi toka Jeshi la Marekani zimeanza kuwasili ikiwa ni maandalizi tu ya kuimarisha ulinzi na usalama kwenye ujio wa Rais Obama.

Wakiongea na Kariakoo blog, baadhi ya maofisa wa Aripot walisema kuwa " Ndege zimeanza kuingia hasa nyakati za usiku ambapo tayari kuna Helkopter kadhaa zimeshuka usiku wa jana hapa Airpot ya Zanzibar na Dar hivyo kweli hali ya usalama ni kubwa sana" Alisema ofisa huyo

Aidha watafiti wa mambo wanadai  kuwa ulinzi wa Obama umekuwa mkubwa kuliko wa Georg W.Bush ilivyokuwa miaka kadhaa iliyopita