http://kariakoodsm.blogspot.com
KARIAKOO BLOG:Kwa Habari Kali Za Mjini | SIASA | BURUDANI | UCHUMI | FASHION | BLOGGER TRICKS | UDAKU | MICHEZO | WASILIANA NA MIMI|0713305567 |urassaombeni@yahoo.com|KWA| MATANGAZO| BABARI| USISITE PIA KUCOMMENT KWENYE HABARI ZETU | <div style='background-color: #de24de;'><a href='http://www.ikiloop.com/' title='link'></a></div>
Showing posts with label AJALI. Show all posts
Showing posts with label AJALI. Show all posts

Sunday, 5 May 2013

PICHA NA MATUKIO MBALIMBALI KANISA LILILOLIPULIWA NA BOMU ARUSHA

eneo lenye utepe ndipo kinachohisiwa kuwa bomu ndipo kilipotua na kulipuka katika Kanisa la Mt Joseph Olasiti Arusha ambapo Balozi wa Papa alikuwa akihudhuria ibada ya Kuzindua Parokia kanisani hapoMungu uwe upande wetu
Umati wa wakazi wa Arusha wakielekea eneo la tukio kujua hali za ndugu zako

ARUSHA UPDATES: RPC- ARUSHA ATHIBITISHA KUWA KILICHOLIPUA KANISA NI BOMU



Mkuu wa Mkoa Mulongo naye  amefika  eneo  la  tukio  na  kuwafariji  wahanga  wa  tukio  la  bomu....

RPC  wa  mkoa  wa  Arusha  naye  aliambatana  na  mkuu  wa  mkoa  na  muda  huu  alikuwa  anatoa  nasaha  zake  kwa  wananchi....

RPC  ameeleza  kuwa  tukio  hili  ni  la kigaidi. Katika  maelezo  yake, RPC amesema kuwa  aliyehusika alijitokeza nyuma ya jengo kwa kujificha na kurusha bomu. ...

Amesema Polisi wanawasaka waliohusika  na  unyama  huu  na  ameomba yeyote  mwenye taarifa yoyote aisaide polisi. ..


Waliojeruhiwa ni 50 .Hao wana majeraha ya kawaida  na 3 wako  mahututi

Mpaka sasa  mtu mmoja anashikiliwa  na  polisi kwa mahojiano  zaid

ARUSHA UPDATES: MBUNGE LEMA ATEMBELEA ENEO LA KANISA LILILOLIPULIWA


Godbless  Lema ambaye  ni  mbunge  wa  arusha  ametembelea  eneo  la  kanisa  lililolipuliwa  na  kuwafariji  wahanga  wa  tukio  hilo.....

 Akiongea  kwa  jazba  na  hasira  na  wanachi  waliopo  eneo  la  tukio,Lema  ameitumu  serikali  kwa  mara  nyingine  na  kudai  kuwa  uzembe  wa  viongozi  ndo  chanzo  cha  matukio  kama  haya....

Hotuba  fupi  na  nasaha  zake  zilikuwa  zikisikika  moja  kwa  moja  kupitia  Radio  maria   kabla ya  kituo  hicho  kuamua  kukatisha  nasaha  zake.....

Haijafahamika  mara  moja  sababu  za  kukatishwa  kwa  hotuba  yake ...

Bado tunasubiri  taarifa  rasmi  ya  vyombo  vya  ulinzi  na  usalama  kuhusiana  na  tukio  hili

BREAKING NEWS: KANISA KATOLIKI LALIPULIWA NA BOMU JIJINI ARUSHA WAKATI MISA IKIENDELEA



Kanisa katoliki parokia ya Olasiti ambalo leo hii lilikuwa linapandishwa hadhi na kuwa Parokia limelipuliwa na kitu kinachosemekana kuwa ni bomu, watu wengi wamejeruhiwa na mtu mmoja inasemekana amefariki dunia.... ....



Tukio hilo limetokea wakati Misa ikiwa ndio inaanza .Ilikuwa ni saa 5 kamili...Kabla Askofu hajaanzisha sala , mlipuko mkubwa ulitokea ndani ya kanisa hilo......


Mgeni rasmi katika hafla hiyo alikuwa ni balozi wa Vatican nchini Tanzania. ...

Habari zaidi zinakuja

Saturday, 4 May 2013

MFANYABIASHARA AJIRUSHA TOKA GHOROFA YA TISA KARIAKOO



TAARIFA za awali zina arifu kuwa Mfanya Biashara, Costa Shirima anaedaiwa kujirusha kutoka gorofa ya tisa ya Hoteli ya Concord iliyopo Kariakoo Jijini Dar es Salaam inaelezwa kuwa alifariki  dunia  muda mfupi  baada  ya  kujirusha na  alikuwa asafiri na ndege ya saa 10 jioni kuelekea China kufuata bidhaa za maduka yake.

Shirima (47), ambaye amefikwa na umauti muda mfupi baada ya kudondoka chini ni mfanyabiashara aliyekuwa akimiliki maduka kadhaa ya urembo wa akina mama yaliyopo jirani na Hoteli hiyo ya Concord.

Aidha taarifa hizo za awali kutoka kwa mmoja wa wanafamilia ambaye alidai kuwa si msemaji wa familia ya Shirima ya Mwika Moshi mkoani Kilimanjaro, nikuwa Marehemu mara kwamara alikuwa akipendelea kula katika hoteli hiyo na siku ya tukio inadaiwa kuwa aliwaeleza watu kuwa anapanda juu ya Hoteli hiyo kupunga upepo baada ya kuhisi hewa nzito mahali alipokuwa.


Inadaiwa kuwa baada ya kupanda huko juu ghafla alianguka chini na kudondokea gari dogo aina ya Toyota Corola linalofanya biashara ya Taxi na kupoteza maisha yake na gari hilo kuharibika vibaya kutokana na kishindo hicho.

Marehemu Shirima mbali na kuwa Mfanya Biashara wa muda mrefu Kariakoo pia alikuwa akiendelea na Ujenzi wa Jengo la Gorofa maeneo ya Kariakoo.

Marehemu ameacha Mjane na watoto 5.

Wednesday, 3 April 2013

UNAJUA ALICHOKIANDIKA KIBANDA LEO FB????GONGA HAPA



Ufisadi mkubwa kampuni za simu


KWA UFUPI
“Misamaha kwa kampuni za mawasiliano ni miaka mitano na TIC inaweza kuongeza miaka mingine mitatu. Kutokana na hali hiyo tunahitaji marekebisho ya sheria ili tuweze kuzibana hizi kampuni ziweze kulipa kodi na kuchangia pato la ndani,” alisema Zitto.Hata hivyo, Mwenyekiti wa Kamati hiyo Zitto Kabwe hakuwa tayari kueleza maeneo ambayo Serikali imekuwa ikipunjwa kodi na kampuni hizo na badala yake amesema wameunda kamati ndogo ya watu watatu kwa ajili ya kuchunguza wizi huo.

Kamati hiyo ilibaini madudu hayo baada ya kukutana na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Mamlaka ya Mawasiliano (TCRA), Mamlaka ya Bandari (TPA) na Wakala wa Vipimo Tanzania (WMA).

Akizungumza na waandishi wa habari, Zitto alisema wameitaka TRA kuandika mapendekezo ya kufanyiwa marekebisho ya sheria ya fedha ya 2012, ili iwe na uwezo wa kuhakiki uwekezaji wa kampuni za simu na kufanya ukaguzi wa miradi husika ili kubaini kama inafanana na kodi inayotozwa.

Alisema kampuni hizo zina misamaha mikubwa ya kodi ambayo inatolewa na Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) bila kushirikisha wadau mbalimbali na kwamba hivi sasa Serikali inapata Sh300 bilioni tu kwa mwaka kama fedha za mapato ya kampuni hizo.

“Misamaha kwa kampuni za mawasiliano ni miaka mitano na TIC inaweza kuongeza miaka mingine mitatu. Kutokana na hali hiyo tunahitaji marekebisho ya sheria ili tuweze kuzibana hizi kampuni ziweze kulipa kodi na kuchangia pato la ndani,” alisema Zitto.

Zitto alisema mbali na mapendekezo hayo, pia wamemtaka Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kukagua misamaha yote ya kodi inayotolewa na TIC ili kujiridhisha kabla ya kutoa uamuzi wa kuendelea nayo ama vinginevyo.

Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa PAC, Deo Filikunjombe alisema: “Kuna fedha zinakatwa kienyeji tu na kampuni hizi, mfano kwa watu 5 milioni kwa siku wanapata Sh1.8 bilioni, sasa kama kampuni hii itakuwa na wateja zaidi inapata kiasi gani, fedha hizi hazipo katika mlolongo wa ukatwaji wa kodi.

“Pia tutahitaji maelezo ya jinsi mnavyodhibiti meseji za chuki ambazo tunaziona kila siku katika simu zetu, pia kampuni hizi zimekuwa zikibadili majina kila baada ya muda fulani jambo ambalo pia linakosesha nchi mapato.”

TRA na TCRA
Mkurugenzi Mkuu wa TRA, Harry Kitilya alisema kinachowakwamisha ni sheria zilizopo, kwamba wanashindwa kukusanya mapato kwa kuwa kampuni hizo zina misamaha ya kodi.
“Misamaha hii ndiyo inatupa wakati mgumu kukusanya mapato, ila kama sheria hii ya misamaha ya kodi itafanyiwa marekebisho tutaweza kuingia kiasi kikubwa cha kodi,” alisema Kitilya.

Naye Profesa Nkoma alisema ili kuzibana zaidi kampuni za simu kuanzia mwezi Julai mwaka huu utafungwa mtambo maalumu wa kudhibiti mawasiliano (TTMS).
Kuhusu wizi wa mafuta bandarini, Zitto alisema kamati hiyo itafanya kazi kwa muda wa mwezi mmoja ikiwa ni pamoja na kuhoji wadau mbalimbali wanaohusika na suala hilo ili wahusika waweze kuchukuliwa hatua za kisheria.

Alisema wizi huo umekuwa ukifanywa kutokana na kuchezewa kwa mabomba (flow meters) ya kupakua mafuta kutoka kwenye meli na kwamba WMA pamoja na TRA wamethibitisha kwamba vipimo hivyo havifai kwani vinasoma tofauti na kiasi cha ujazo wa mafuta.

Aliongeza kuwa kitendo cha kuzuia mashine hiyo kutofanya kazi kumezidisha wizi wa mafuta bandarini, jambo ambalo limesababisha kuongezeka kwa malalamiko.

Alisema katika mazingira hayo mkakati wa Serikali wa kuongeza mapato kupitia vyanzo vya ndani hauwezi kufanikiwa, hivyo wabunge wana wajibu wa kuchukua hatua ili kuhakikisha hali hiyo inafanyiwa kazi.

Monday, 1 April 2013

Breaking News: Mgodi wafukia wachimbaji Arusha; zaidi ya watu 18 wanahofiwa kufariki.. Wanajeshi wafanaya uokozi sasa na tayari mtu mmoja ameokolewa hai na wengine watatu wakiwa wameshakufa!


KWA mujibu wa mashuhuda wa ajali iliyotokea leo asubuhi Jijini Arusha, inakadiriwa zaidi ya watu 18 wamepoteza maisha kufuatia kufukiwa na gema la mchanga/moram wakati wakichimba na kupakia kwenye malori.
Ajali hiyo mbaya imetokea katika machimbo ya moram nje kidogo ya Jiji eneo jirani na Moshono-Kiserian ambapo vijana hao wanaokadiriwa kufikia idadi hiyo walikuwa wakipakia moram kwenye magari mawili, moja ni Fuso na lingine kubwa zaidi (tani 18) na yote mawili yamefukiwa kabisa na kifusi.
Shuhuda mmoja wa ajali ambae pia ni mchimbaji ameieleza Blog hii kwamba kwa kawaida gari ndogo kama Fuso hupakiwa na watu 7, na hiyo kubwa huwa na watu 12 bila kuhesabu dereva na utingo.
Blog hii iliweza kushuhudia sehemu ndogo sana ya Fuso ikionekana lakini gari nyingine ilikua imefukiwa kabisa na kupondeka vibaya.
Miongoni wa waliofikwa na mauti ni pamoja na madereva wa magari hayo. taarifa za eneo la tukio zinaeleza utingo mmoja ameokolewa akiwa amejeruhiwa vibaya na kukimbizwa hospitali lakini dereva wake amefariki dunia.
Katika eneo la ajali hali ni ya simanzi na vilio toka kwa kina mama huku baadhi wa wababa na marafiki na ndugu wa jamaa waliofukiwa wakishindwa kujizuia na kuangua kilio.
Meya wa Manispaa Mh Gaudence Lyimo pamoja na Mbunge wa Arusha Mjini Mh Godbless Lema ni miongoni mwa viongozi wakubwa waliofika eneo la ajali kusaidiana na kikosi cha Jeshi la Wananchi kufanya uokozi.
Blogu hii ilishuhudia pia Wachina wakipeleka moja ya mashine zao (Excavator) kuongeza nguvu katika kusaidia kufukua miili ya watu hao iliyonaswa na kifusi hicho.
ajali (66)Mwili wa dereva wa lori moja kubwa lenye ujazo wa tani 18 ukiwa umeopolewa na askari jeshi, tayari kupelekwa mochwari ya Hospitali ya Mt Meru. Dereva huyu ametambulika kwa jina moja tu la Alex amefikwa na mauti akiwa ndani ya gari hilo wakati vijana wengine wakiendelea kupakia moram asubuhi ya leo
ajali (55)Mbunge wa Arusha Mjini, Mh Godbless Lema akiwasili eneo la ajali mapema asubuhi
ajali (44)Baadhi ya wananchi waliojitokeza kushuhudia ajali hiyo mbaya wakishangaa zoezi la uokoaji na wengine wakisubiri kutambua ndugu zao, jambo ambalo halikupata nafasi
ajali (56)Meya wa Manispaa ya Arusha, Mh Gaudence Lyimo akisaidiana na vikozi vya jeshi katika zoezi la uokozi
ajali (59)Mh Lema akiangalia namna vikosi vya Jeshi la Wananchi pamoja na askari Polisi wakiendelea na zoezi la uokozi
ajali (65)Mwananchi huyu aliishiwa nguvu baada ya kushuhudia mwili wa rafiki yake ukiopolewa kutoka kwenye kifusi
ajali (49)Hali ilivyo machimboni hapo
ajali (64)Kina mama wakilia kwa uchungu wakihofu kuondokewa na wapendwa wao
ajali (21)Vikosi vya Jeshi la Wananchi na Polisi vikiwa kazini
ajali (35)Sehemu ndogo ya Fuso ikionekana huku gari nyingine ikiwa haionekani kabisa
ajali (23)
ajali (2)Ambulance ya Jiji tayari tayari kwa lolote ikihitajika
ajali (3)
ajali (4)Wachina wakielekea eneo la jali na vifaa vyao kusaidia zaidi zoezi la uokozi
ajali (6)Wanajeshi zaidi wakielekea chini kwenye mgodi
ajali (21)
Tunaomba radhi kwa ubora hafifu wa picha hizi….

UPDATE ARUSHA: IDADI YA WALIOFARIKI DUNIA KWA KUFUKIWA NA KIFUSI IMEFIKIA 20




WATU zaidi ya 20 wamefariki dunia kwa kufukiwa na kifusi wakati wakichimba  mchanga aina ya Moramu katika machimbo  yaliyopo Moshono nje kidogo ya jiji la Arusha.


Tukio hilo ambalo limegubikwa na simanzi na vilio kwa ndugu jamaa na wananchi, limetokea leo majira ya saa 5 asubuhi wakati marehemu hao wakichimba na kupakia Moramu hiyo kwenye magari .


Pamoja na vifo hivyo magari mawili aina ya Fuso na Scania yameharibiwa vibaya baada ya kufukiwa na kifusi kilichoporomoka umbali unaofikia mita 50 kutoka usawa wa bahari.


Tayari kikosi cha uokoaji ambao ni  Jeshi la Wananchi Kambi ya Tanganyika Parkers kimefanikiwa kuopoa miili ya marehemu 16 waliofukiwa.


Baadhi ya miili ya marehemu  imetambulika kwa majina kuwa ni  Alex Maliaki, Gerald Hamis, Sauli Rafael (Mbu), Barick Loselian, Kababuu Lowasale, Mwenda Kibobori, Japhet Mjivaine na Garald Masai.


Taarifa za mashuhuda zimebainisha kwamba chanzo cha kuporomoka kwa kufusi hicho ni mvua kubwa zinazoendelea kunyesha jijini Arusha zilizosababisha kukatika kwa Ngema baada ya kuzidiwa na maji ya mvua.

ARUSHA:ZAIDI YA WATU 18 WAMEFARIKI DUNIA BAADA YA KUFUKIWA NA KIFUSI KATIKA MACHIMBO YA MORRUM



Majeruhi aliyeokolewa.
Mwili wa mmojawapo wa marehemu.
Wananchi wa eneo hilo wakiwa na simanzi baada ya ajali hiyo.
----------
Watu zaidi ya 18 wanahofiwa kuwa wamepoteza maisha baada ya kufukiwa na kifusi wakiwa ndani ya mgodi wa Morrum huko Moshono jijini Arusha. 

Kwa sasa wanajeshi wanaendelea na zoezi la uokoaji na tayari majeruhi mmoja ameokolewa na miili ya watu watatu. 

Tukio hili linatokea ikiwa ni siku siku tatu baada ya maafa mengine kutokea jijini Dar es Salaam ambapo watu zaidi ya 30 wamepoteza maisha baada ya jengo la ghorofa 16 kuporomoka.


Sunday, 31 March 2013

Ajali; Simulizi ya aliyenusurika kifo kutoka ghorofa ya 15


Rais Kikwete na Mkewe, Mama Salma Kikwete wakimpa pole Yusuph Abdallah katika Hospitali ya Muhimbili walipotembelea majeruhi wa ajali ya kuporomoka jengo la ghorofa 16. Picha na Muhidin Michuzi 

Dar es Salaam. Fundi ujenzi, Yusuph Abdallah ambaye amelazwa katika Taasisi ya Mifupa (Moi), ameeleza jinsi alivyonusurika kifo baada ya jengo la ghorofa 16 kuporomoka Ijumaa iliyopita.

Yusuph aliliambia Mwananchi akiwa wodini kwamba kilichomponya ni neema za Mungu kwani kabla jengo hilo kuporomoka yeye alikuwa ghorofa ya 15 kwenye jengo hilo katika Mtaa wa Indira Gandhi akiendelea na ujenzi.
Alieleza kuwa hakuwa anafahamu kinachoendelea, bali aliona ghafla jengo linaaanza kuporomoka, na baada ya hapo hakufahamu zaidi kilichotokea hadi alipojikuta yuko hospitalini.
“Kweli jengo lilipoanza kuporomoka sikutambua nini kinachoendelea kwani nilipoteza fahamu na kujikuta nipo hapa Muhimbili,” anasimulia Abdallah.
Alisema anahisi alipoanguka alifunikwa na kifusi kilichomponda na kuvunja miguu yote.
Fundi huyo ambaye amefungwa plasta gumu (P.O.P) miguu yote, alisema hakuweza kuona watu waliomwokoa.

Mwingine aokolewa na mkewe

Mkazi wa Ubungo, Ally Mlela ambaye ni fundi madirisha anasimulia jinsi mke wake alivyomwokoa katika ajali hiyo baada ya kumtaka asiende kufanya kazi siku hiyo.
Akisimulia jinsi ilivyokuwa Mlela anasema siku ya tukio aliwasiliana na rafiki yake ambaye amepoteza maisha katika ajali hiyo na kumtaka aende akaonane na mkandarasi wa jengo hilo, ili ampe kazi ya kuweka madirisha.
“Majira ya asubuhi kati ya saa mbili na saa tatu hivi nilipokea simu kutoka kwa rafiki yangu jina maarufu anajulikana kama Tafu, ambapo alinitaka niende nikaonane na mkandarasi wa jengo hilo ili anipe kazi ya kuweka madirisha,” anasema Mlela.
Anasema wakati akijiandaa kutoka mke wake alimwambia siku hiyo apumzike asiende kufanya kazi naye akakubali, lakini haikupita muda mrefu mke wake alimfuata na kumuuliza amesikia taarifa kwamba kuna jengo limedondoka?
“Niliamua kwenda katika eneo la tukio na ndipo alipogundua kwamba eneo hilo ndiyo alipotakiwa kwenda kufanya kazi. Wakati juhudi za uokoaji zikiendelea nilijaribu tena kumpigia simu rafiki yangu.Nikiwa bado kwenye eneo la tukio ghafla nikaona mguu ukitolewa kwenye mchanga na nilitambua ulikuwa mguu wa rafiki yangu baada ya kuona kiatu chake.”

JK awatembelea majeruhi

Rais Jakaya Kikwete jana aliwatembelea majeruhi wa ajali hiyo ambao wamelazwa Hospitali ya Taifa Muhimbili na kuwapa pole.
Akizungumza na waandishi wa habari, Mkurugenzi wa Tiba wa Taasisi ya Mifupa (Moi), Dk Cuthbert Mcharo alisema walipokea majeruhi sita na hadi jana walikuwa wamebakia wanne.

Miili zaidi yapatikana

Katika hatua nyingine kikosi cha uokoaji jana kilipata miili ya watu saba iliyopatikana. Mmoja kati ya miili hiyo baada ya kuuchunguza, ulikutwa na kitambulisho cha kupigia kura kinachomtambulisha kwa jina la Salumu Mwaliko kutoka Kijiji cha Kwadeboma, Handeni mkoani Tanga.
Hatua hiyo inafanya idadi ya watu waliopoteza maisha katika maafa hayo kufikia 31.

NHC kugharimia majeruhi, mazishi

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadick alisema amepokea taarifa kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Nehemia Mchechu kwamba kuna majengo matatu ya ghorofa ambayo yanatakiwa kubomolewa kutokana na kuchakaa. Mbali na hilo, Mkuu wa Mkoa amesema Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) linatakiwa kulipa gharama zote za watu walioathirika na ajali ya Ijumaa iliyopita.
Alisema NHC wanapaswa kuwahudumia majeruhi wote pamoja na kugharimia mazishi ya watu waliopoteza maisha.