http://kariakoodsm.blogspot.com
KARIAKOO BLOG:Kwa Habari Kali Za Mjini | SIASA | BURUDANI | UCHUMI | FASHION | BLOGGER TRICKS | UDAKU | MICHEZO | WASILIANA NA MIMI|0713305567 |urassaombeni@yahoo.com|KWA| MATANGAZO| BABARI| USISITE PIA KUCOMMENT KWENYE HABARI ZETU | <div style='background-color: #de24de;'><a href='http://www.ikiloop.com/' title='link'></a></div>
Showing posts with label HOME. Show all posts
Showing posts with label HOME. Show all posts

Monday, 17 June 2013

MBOWE:Hata kama utaamua Mbowe au (Godbless) Lema, huwezi kuiua CHADEMA wanachama wengine wataendeleza harakati za chama kama kawaida,




MWENYEKITI wa CHADEMA Freeman Mbowe, amevituhumu vyombo vya dola kuwa vinawafahamu watu walioshiriki kwenye mlipuko wa bomu uliotokea juzi katika viwanja vya Soweto kwenye mkutano wa chama hicho.

Mbowe, alisema tukio hilo ni la kupangwa na wamegundua risasi za bunduki aina ya SMG na bastola zilitumika mara baada ya mlipuko huo jambo linalozusha hofu na kudidimiza demokrasia ya vyama vingi.

Wakati Mbowe akitoa tuhuma hizo kwa vyombo vya dola, Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Said Mwema ameunda timu itakayoongozwa na makamishna wawili (Paul Chagonja na Isaya Mungulu), kwenda mkoani Arusha kuongeza nguvu ya uchunguzi.

Akizungumza na waandishi wa habari jana mkoani hapa, Mbowe alisema uchunguzi wa awali walioufanya wamebaini tukio hilo ni la kisiasa na lilipangwa.

Alisema ni vema serikali ikatangaza kuachana na mfumo wa vyama vingi kuliko kuruhusu mauaji na vurugu katika mikutano ya vyama vya upinzani vinavyoonekana kutoa wakati mgumu kwa watawala.

Aliongeza kuwa uchunguzi wa awali katika eneo la tukio umebaini bomu lililolipuliwa ni la kiwandani na si la kutengenezwa.

Alisema katika eneo la tukio maganda ya risasi kutoka katika bunduki ya SMG na bastola yalikutwa hali inayowafanya waamini kuna watu waliamua kufanya tukio hilo kwa kupanga.

Mbowe alisema risasi hizo pia ni miongoni mwa zilizopigwa kwenye tanki la mafuta la gari la matangazo la CHADEMA ambapo zililitoboa.

Alibainisha kuwa inavyoonekana wahusika walitaka kuzalisha mlipuko mwingine mkubwa na kuleta maafa makubwa katika mkutano huo.

“Haihitaji uchunguzi wa kwenda mwezini katika suala hili, ni wazi walipanga kutuua lakini wakaua watu wasiohusika. Waliouawa hawakuwa katika mpango wao na wamekuwa wahanga kwa niaba yetu.

“Hata kama utaamua kumuua Mbowe au (Godbless) Lema, huwezi kuiua CHADEMA kwani chama kitabaki, na wanachama wengine wataendeleza harakati za chama kama kawaida,” alisema.

Wabunge kutohudhuria Bunge

Mbowe alisema kutokana na tukio hilo ambalo limeua watu zaidi ya watatu, CHADEMA imeamua kulifanya ni la kitaifa na wabunge wake watashiriki kwenye maombolezo.

Alisema kuanzia leo wabunge wote wa CHADEMA hawatahudhuria vikao vya Bunge na watajumuika mkoani Arusha hadi misiba yote itakapomalizika.

Alisema wanatarajia kufunga mahema katika eneo la tukio na marehemu wote wataagwa katika eneo hilo ambapo ibada zote za Kiislamu na Kikristu zitafanyikia hapo.

IGP aunda timu

Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Mwema ameunda timu ya kuongeza nguvu ya uchunguzi itakayoongozwa na makamishna wawili ambao ni Paul Chagonja kutoka idara ya operesheni na Isaya Mngulu kutoka ofisi ya upelelezi makao makuu.

IGP Mwema alisema baada ya tukio hilo, jeshi hilo lilituma makamishna wawili kutoka makao makuu kwa ajili ya kuongeza nguvu ya uchunguzi wa tukio hilo na kwamba wameshaanza kukusanya taarifa mbalimbali zitakazoweza kusaidia kuwabaini watu waliohusika.

Alisema wameunganisha nguvu na vyombo vingine vya ulinzi na watawasaka wahalifu hao pamoja na walio nyuma yao kwa kile alichoeleza tukio hilo linaashiria kushamiri kwa matendo ya kigaidi nchini.

Akizungumzia tuhuma zinazotolewa na wananchi juu ya Jeshi la Polisi kuwajeruhi watu kwa risasi za moto, IGP Mwema alisema kila taarifa inafanyiwa kazi kwa umakini na kwamba baada ya uchunguzi watatoa taarifa kamili kwa umma juu ya kilichotokea jijini Arusha.

Aliwaomba wananchi wenye taarifa za kuweza kumtambua aliyerusha bomu pamoja na watu walio nyuma yake wajitokeze au wamtumie ujumbe kupitia simu yake ya mkononi namba 0754 78 55 57 na kwamba uhusika wao utafanywa kuwa siri.

IGP Mwema pia alisema watachunguza kauli ya Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) bara, Mwigulu Nchemba aliyowaambia wakazi wa Kimandolu kuwa wasipoichagua CCM katika uchaguzi wa madiwani wa Jiji la Arusha ulioahirishwa jana, watakufa.

Mwema alisema watachunguza kauli hiyo baada ya kuulizwa swali la hatua zilichochukuliwa kabla na baada ya mlipuko huo dhidi ya kauli ya Nchemba.

Juzi katika mkutano wa kufunga kampeni za udiwani kwa CHADEMA uliofanyika kwenye viwanja vya Soweto, kitu kinachodhaniwa ni bomu kilipuka na kuua watu watatu na wengine kujeruhiwa.

MBOWE ATEMBELEA ENEO LA MLIPUKO, PAMOJA NA KUTEMBELEA FAMILIA ZA WAFIWA NA MAJERUHI WA MABOMU NA RISASI ARUSHA


Mwenyekiti wa Chadema, Mh freeman Mbowe na Mbunge wa Arusha Mjini Mh Godbless Lema wakiwa katika uwanja wa Soweto mchana wa leo wakati zoezi la kuchukua vipimo mbalimbali likiendelea chini ya usimamizi wa wataalamu toka Jeshini.

Mbowe na Lema wakishauriana jambo..
Eneo la maafa. Inaelezwa kuwa wataalamu wa jeshi waligundua kuwako kwa kitu ndani ya tanki la mafuta na hivyo kuamua kulikata. Taarifa hizo zinadai kwamba kulikuwa na mabomu yametegwa chini ya gari na hivyo tank hilo lilishmabuliwa kwa risasi labda utokee mlipuko! Pia gari hii ya amatangazo ina majeraha mawili mlango wa kushoto yaliyotokana na kitu chenye ncha mabacho kinaweza kuwa risasi au vipande vya vyuma vya bomu.


Mh Mbowe akiwa nyumbani kwa wazazi wa mmoja wa marehemu (Ramadhani) eneo la Mianzini kuwapa pole kwa kuondokewa na mpendwa wao.
James Ole Millya na Mbunge Lema wakimjulia hali mmoja wa majeruhi walilazwa hospitali ya Seliani

Mtoto Sharifa nae amalazwa hospitalini hapo kwa majeraha ya mlipuko
Dereva wa mgombea wa Chadema Kata ya Themi, Bw beni akiwa majeruhi kitandani

Kamanda wa Chadema ambaye alikuwa ni mlinzi wa amani (Red Brigade) katika mkutano huo, Bw Kitumbwizi akiugulia maumivu katika hospitali ya Selian alikolazwa baada ya kujeruhiwa katika mlipuko huo. Huyu amaumizwa mguu mmoja, mkononi na sehemu ya kwapani ambapo imegundulika kuwa kuna chuma ama risasi ndani ambayo imekuwa ngumu kutolewa mapaka sasa.

Sunday, 16 June 2013

PICHA: USHAHIDI WA SHOO YA MWANA FA ILIVYOBUMA


King Zilla kutoka Salasala alikuepo. 


Watu wakipata chakula na vinywaji kabla ya kuingia kwenye show 


Meneja wa Ommy Dimpoz, Muba, Salama na Ommy Dimpoz. 























Ilikua ni show inayohitaji watu 400 tu
Ben Pol kwenye stage. 
FA mwenyewe. 



Mandojo na Domokaya, Kilimanjaro Band, Fa na Linah pamoja na Maua. 



Mwigizaji Wema Sepetu akiingia. 


Reuben Ncha kali na Shadee. 
Vanessa Mdee na B12 

CHADEMA YAZIDI KUPENYA NGOME ZA CCM

Mashabiki wa CDM wakishangilia ushindi Iyela, Mbeya



HABARI MPYA: Hadi hivi inaonekana CHADEMA imeinyang’anya CCM viti kadhaa vya Udiwani na kutuma ujumbe kuwa ‘upepo umebadilika’. Baadhi ya Kata ambazo matokeo yake yameshajulikana ni kama hivi:

1. Makuyuni, Monduli (ARUSHA) – CCM
2. Minepa, Ulanga (MOROGORO) – CCM
3. Bashnet, Babati (MANYARA)- CHADEMA
4. Nyampulikano, Sengerema (MWANZA) – CHADEMA
5. Masanze, Kilosa (MOROGORO) – CCM
6. Ifakara, Ifakara (MOROGORO) – CCM
7. Tingeni, Muheza (TANGA) – CCM

8. Genge, Muheza (TANGA) – CCM

9. Iyela, Mbeya (MBEYA) – CHADEMA

10. Iseke, Singida (SINGIDA) – CCM

11. Manchira, Serengeti (MARA) – CCM

12.

ITAENDELEA..............

Sunday, 9 June 2013

Mbunge CCM mbaroni vurugu za gesi Mtwara


Dar es Salaam. Jeshi la Polisi mkoani Mtwara limemkamata mbunge wa Mtwara Mjini (CCM), Hasnain Murji likimtuhumu kuchochea vurugu za kupinga mradi wa bomba la gesi kutoka mkoani humo kwenda jijini Dar es Salaam.


Habari zilizopatikana na kuthibitishwa na Msemaji wa Jeshi la polisi nchini, Advera Senso zinaeleza kuwa Murji alikamatwa jana jioni nyumbani kwake maeneo ya Shangani mjini Mtwara.


Kukamatwa kwa mbunge huyo kunakuja ikiwa zimepita siku tano tangu viongozi wanne wa vyama vya upinzani mkoani Mtwara, kufikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Mtwara, Juni 4, mwaka huu wakikabiliwa na mashtaka matatu ikiwamo kula njama, kufanya uchochezi na kuamsha hisia mbaya kwa wakazi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.


Washtakiwa hao ni Katani Ahmed Katani (33) na Saidi Kulaga (45) wa CUF, Hassan Uledi (35) wa NCCR Mageuzi na Hamza Licheta (51) wa TLP, wote wakazi wa Mtwara. Taarifa zaidi zilieleza kuwa baada ya polisi kumkamata mbunge huyo, walifanya upekuzi katika nyumba yake kwa saa kadhaa na baada ya kujiridhisha walikwenda kupekua na ofisi yake.


“Amekamatwa kwenye saa 11:00 jioni, hata hati ya kukamatwa kwake imeeleza kuwa anatuhumiwa kuchochea vurugu za kupinga gesi inayopatikana mkoani Mtwara kwenda Dar es Salaam,” alisema Katibu wa Mbunge huyo, Meckland Millanzi.


Katika ufafanuzi wake Senso alisema kukamatwa kwa mbunge huyo ni jambo la kawaida na kwamba hivi sasa unaandaliwa utaratibu ili faili lake lipelekwe kwa Mwanasheria wa Serikali.


“Acheni polisi ifanye kazi yake kama kutakuwa na la ziada tutawaeleza ila kwa sasa tunaandaa utaratibu wa suala hili kwenda kwa mwanasheria wa Serikali,” alisema Senso. Murji amekamatwa ikiwa zimepita siku 16 tangu kutokea vurugu kubwa mkoani Mtwara zilizodumu kwa siku mbili, ambapo polisi walipambana na makundi ya vijana wanaopinga mradi wa bomba la gesi kujengwa.


Vurugu hizo zilizosababisha baadhi ya watu kupoteza maisha huku wengine wakiachwa majeruhi na mali nyingi kuharibiwa, ziliibuka baada ya hotuba ya bajeti ya wizara ya nishati na madini kusomwa bungeni .


Mvutano kuhusu mradi wa bomba la gesi ulianza Novemba 16, mwaka jana baada ya Serikali kutuma kamati inayoratibu maoni ya sera ya gesi “The Natural Gas Policy of Tanzania -2013” ambayo ilifika mkoani Mtwara kukusanya maoni ya wananchi.


Katika mikutano yake mjini Mtwara, wananchi wengi hawakukubaliana na wazo la kusafirishwa gesi nje ya Mtwara kwa njia ya bomba. Hali hiyo ndiyo iliyowasukuma viongozi wa vyama kuhamasisha wananchi

WASHINDI WA TUNZO(AWARDS)KILIMANJARO MUSIC AWARDS- KTMA 2013



Usiku wa tuzo za KTMA ulipambwa na burudani ya aina yake kutoka kwa wasanii mbalimbali wakiwemo Linah, Amini, Richie Mavoko, Mataluma, Hussein Jumbe, Zahir Zorro, Patricia Hillary na Barnaba. Wengine ni Snura, Godzilla, Mabeste, Madee na Afande Sele.


Host wa tuzo hizo mwaka huu alikuwa ni Zembwele na TJ.


Hii ni list nzima ya tuzo hizo.


Wimbo bora wa mwaka
Dear God – Kala Jeremiah

Msanii bora wa Kiume
Diamond


Msanii bora wa kike 
Lady Jaydee


Msanii bora wa kike Taarab
Isha Mashauzi


Msanii bora wa kiume Taarab
Mzee Yusuf


Msanii bora wa kiume Bongo Flava
Diamond

Msanii bora wa kike Bongo Flava 
Recho


Msanii bora wa Hip Hop
Kala Jeremiah


Msanii bora wa kiume Bendi
Chalz Baba


Msanii bora wa kike Bendi
Luiza Mbutu


Msanii bora anayechipukia
Ally Nipishe


Video bora ya mwaka
Baadaye – Ommy Dimpoz


Mtunzi bora wa mashairi Taarab
Mzee Yusuf


Mtunzi bora wa mashairi Bongo Flava
Ben Pol

Mtunzi bora wa mashairi hip hop 
Kala Jeremiah


Mtunzi bora wa mashairi Bendi
Chalz Baba


Mtayarishaji bora wa mashairi muziki wa kizazi kipya
Man Walter


Mtayarishaji wa wimbo wa mwaka – Taarab
Enrico


Mtayarishaji wa wimbo mwaka – Bendi
Amoroso


Mtayarishaji chipukizi wa mwaka
Mesen Selekta


Rapper bora wa bendi
Fagasoni


Wimbo bora wenye vionjo vya asili
Chocheeni Kuni – Mrisho Mpoto ft Ditto


Wimbo bora wa bendi
Risasi Kidole – Mashujaa Band


Wimbo bora wa Reggae
Kilimanjaro – Warriors from The East


Wimbo bora wa Afrika Mashariki
Valu Valu – Jose Chameleone


Wimbo bora wa Bongo Pop
Me an You – Ommy Dimpoz ft Vanessa Mdee


Wimbo bora wa kushirikiana/Kushirikishwa
Me and You – Ommy Dimpoz ft Vanessa Mdee

Wimbo bora wa Hip Hop
Nasema Nao – Nay wa Mitego


Wimbo bora wa rnb
Kuwa na Subira – Rama Dee ft. Mapacha


Wimbo bora wa ragga/ dancehall
Predator – Dabo

Wimbo bora wa Taarab 
Mjini Chuo Kikuu – Khadija Kopa


Wimbo bora wa zouk rhumba 
Ni wewe – Amini


Bendi bora ya mwaka
Mashujaa Band

Kikundi bora cha Taarab 
Jahazi Modern Taarab


Kikundi bora cha muziki wa Kizazi kipya
Jambo Squad


Hall of Fame – Institution
Kilimanjaro Band wana Njenje


Hall of Fame – Individual
Salum Abdallah

Saturday, 8 June 2013

TAIFA STARZ WAFANYIWA UMAFIA ,WATANZANIA WAPAMBANA NA ASKARI


Kocha wa Stars, Kim Poulsen kushoto akipambana na askari wa Uwanja wa Marakech
Na Mahmlud Zubeiry, Marakech, IMEWEKWA JUNI 8, 2013 SAA 8:00 USIKUTIMU ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars usiku huu imekiona cha moto mbele ya askari wa Uwanja wa Marakech, baada ya kufanyiwa vurugu na kuzimiwa taa ishindwe kufanya mazoezi kwenye Uwanja huo siku moja kabla ya mchezo wao na wenyeji wao Morocco kesho, kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Kombe la Dunia. Sheria za FIFA zinasema timu mgeni, itapewa fursa ya kufanya mazoezi katika Uwanja utakaotumika kwa mechi dhidi ya wenyeji katika muda ambao mechi itachezwa, lakini leo msafara wa Stars ulipofika Uwanja wa Marakech ulizuiwa kuingia ndani na askari wa uwanjani hapo. Juhudi za Kocha mkuu wa Stars, Kim Poulsen kuwaelewesha askari wa Uwanja huo sheria ili wairuhusu timu kuingia uwanjani hazikuzaa matunda na ikabidi viongozi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) waingilie kati, nao pia wakachemsha.
Thomas Ulimwengu kulia nje ya geti, askari kushoto



Dk Dau getini


Mtanzania anaruka geti ili kufungua mlango Stars ikafanye mazoezi


Baadhi ya wachezaji wa Stars, kutoka kulia Juma Kaseja, Amri Kiemba, Mrisho Ngassa na Salum Abubakar baada ya kuingia uwanjani


Kutoka kulia Mwinyi Kazimoto, Athumani Iddi 'Chuji' na Kevin Yondan


Crescentius Magori kushoto akishuhudia marefa wa mchezo huo wakikagua pasipoti za wachezaji wa Stars


Wasiwasi; Kutoka kulia DK Dau, Mh Zitto Kabwe, Mh Mohamed Dewji na Magori wakijadiliana uwanjani

Ikawadia zamu ya viongozi wa Kamati ya Ushindi ya Stars, inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premum Lager, ambao nao walichemsha- ndipo baadhi wa Watanzania waishio hapa na wachache waliosafiri kutoka Dar es Salaam walipoongeza nguvu. Walikwenda kufungua geti kwa nguvu, wakawaweka kando askari waliokuwa wanawazuia na kuiingiza timu uwanjani kufanya mazoezi. Hata hivyo, Stars ilipofika uwanjani ililazimika kusubiri tena, kwani wenyeji Simba wa Atlasi walikuwa wakiendelea na mazoezi. Baada ya nusu saa, Morocco walimaliza awamu yao na Stars wakaanza kupasha misuli moto. Hata hivyo, baada ya dakika 34, taa za Uwanja huo zilizimwa na uwanjani kuwa giza totoro, lakini viongozi wa TFF wakaenda kuomba, zikawashwa na timu ikafanya mazoezi kwa dakika 10 zaidi. Naibu Waziri wa Habari Utamaduni na Michezo, Mh. Amos Makalla aliyekuwapo wakati wa vurumai zote hizo, alisikitishwa mno na kitendo hicho akisema si cha kiungwana na si cha kiunamichezo.
Makipa mazoezini; Juma Kaseja amedaka, Ally Mustafa 'Barthez' anamshuhudia kushoto



Shomary Kapombe anayeteleza, Erasto Nyoni akipitisha mpira


Mtanzania amemdhibiti askari wachezaji waingie uwanjani


Wachezaji wakiingia uwanjani kufanya mazoezi


Watanzania wamefanikiwa kufungua geti


Ahmad Mgoyi wa TFF akipambana na askari kufungua geti 


Mpambano, Kim Poulsen na askari, nyuma ni Mgoyi 

Makamu wa Rais wa TFF, Athumani Nyamlani alisema Morocco walikuja kucheza Dar es Salaam walipokewa vizuri na wakahudumiwa vizuri hadi wanaondoka, ajabu leo wanaifanyia ‘unyama’ Tanzania. Mkuu wa Msafara wa Stars hapa, Crescentius John Magori alisema watapeleka malalamiko FIFA, waandaji wa michuano ya kufuzu kwa Kombe la Dunia na kwa kuwa ushahidi upo, anaamini Morocco watachukuliwa hatua. Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba SC, Zacharia Hans Poppe alishauri Stars icheze chini ya angalizo kwa kuwasilisha barua FIFA mapema ili wakae wanajua kuhusu hali halisi Morocco. Kwa ujumla kilichotokea leo kimewatia woga Watanzania wengi waliopo hapa kuelekea mchezo wa kesho, ambao Stars inahitaji ushindi ili kujiimarisha katika mbio za kuelekea Brazil 2014. Hata ulinzi wa msafara wa Stars kutoka hotelini hadi uwanjani hakuwa wa kutosha na ilishuhuidiwa mara kadhaa ukiingiliwa na magari mengine barabarani wakati timu ikienda uwanjani kwa mazoezi. Wenyeji nchini Morocco wanasema inapowadia mechi, huwa wanaogopa kwa sababu mara nyingi hutokea vurugu ya damu kumwagika. Kwa ujumla Stars inaingia katika mchezo wa kesho katika hali ya wasiwasi na woga mkubwa. Stars itashuka dimbani saa 3:00 usiku kesho kwa saa za hapa sawa na saa 5:00 za Tanzania kucheza na Morocco. Stars inashika nafasi ya pili katika Kundi C, ikiwa na pointi sita nyuma ya Ivory Coast yenye pointi saba, ambayo kesho itakuwa ugenini ikimenyana na Gambia katika mchezo mwingine wa kundi hilo.
Mrisho Ngassa anamiliki mpira



Thomas Ulimwengu anakwenda


Mbwana Samatta kulia na mpira


Wachezaji Stars Uwanja wa Marekch

Stars ilitua hapa Jumatatu ikitokea Ethiopia ambako iliweka kambi ya wiki moja na kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Sudan, ulioisha kwa sare ya bila mabao.Kabla ya kuja hapa, Stars iliweka kambi ya wiki moja katika hoteli ya Tansoma, Dar es Salaam ikijifua Uwanja wa Karume na siku chache kabla ya kuondoka ilialikwa Ikulu na Rais Jakaya Kikwete, aliyewapa hamasa kwa hotuba nzuri
Credit to bin zubery