http://kariakoodsm.blogspot.com
KARIAKOO BLOG:Kwa Habari Kali Za Mjini | SIASA | BURUDANI | UCHUMI | FASHION | BLOGGER TRICKS | UDAKU | MICHEZO | WASILIANA NA MIMI|0713305567 |urassaombeni@yahoo.com|KWA| MATANGAZO| BABARI| USISITE PIA KUCOMMENT KWENYE HABARI ZETU | <div style='background-color: #de24de;'><a href='http://www.ikiloop.com/' title='link'></a></div>

Monday, 21 October 2013

SIMBA WAPONEA CHUPUCHUPU KUTOKA KWA YANGA

Dar es Salaam. Bahati yao! Ndicho unachoweza kusema baada ya Simba kufanikiwa kulazimisha sare ya 3-3 dhidi ya Yanga jana kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Mabingwa watetezi Yanga, walianza kwa kasi mchezo na kupata mabao matatu katika kipindi cha kwanza kupitia Mrisho Ngassa na mawili ya Hamis Kiiza, lakini Simba waliamka kipindi cha pili na kusawazisha mabao hayo kupitia Betram Mwombeki, Joseph Owino na Gilbert Kaze.

Katika uchunguzi uliofanywa na Gazeti hili kabla ya mchezo huo ulibaini Simba wamekuwa wakifunga mabao mengi kipindi cha kwanza na Yanga wenyewe wameruhusu mabao mengi kipindi cha pili.


Yanga waliuanza mchezo kwa kasi na dakika ya nne, ambapo katika dakika ya 14 winga Ngassa aliwainua mashabiki wa Yanga baada ya kufunga bao akiunganisha krosi ya Kiiza iliyompita beki wa Simba, Kaze.


Katika dakika ya 35, mpira wa kurusha wa Mbuyu Twite uligongwa na Kavumbagu na kumkuta Kiiza aliyeusukumia wavuni mpira huo kirahisi.Pia katika dakika ya 45, Kavumbagu aliwatoka mabeki wa Yanga na kupitisha krosi fupi kwa Kiiza aliyefunga bao la tatu kirahisi.


Kocha wa Simba, Abdallah Kibaden atajutia uamuzi wake wa 4-4-2 kwa kuwaanzisha Chanongo, Singano, walioshindwa kurudi katikati kuwasaidia Humoud na Mkude kulinda kutokana na kuzoea kucheza kama winga.


Yanga walikuwa imara zaidi katikati ya uwanja wakiwa na viungo watatu Athuman Idd, Frank Domayo na Haruna Niyonzima pamoja na Kavumbagu aliyesaidia hivyo kuwafanya kuwa wanne na kuwafunika kabisa Mkude na Humoud.

Hata hivyo kipindi cha pili katika dakika ya 47 Kibaden aliwapumzisha Chanongo na Humoud na kuwaingiza Said Hamis Ndemla na William Lucian walioimarisha safu ya kiungo na kuirudisha Simba mchezoni.

Mshambuliaji Mwombeki aliipatia Simba bao la kwanza katika dakika ya 53, baada ya mabeki wa Yanga, Nadir na Yondani kufanya uzembe wa kumkaba Amis Tambwe na kutoa nafasi kwa mfungaji .


Dakika ya 57, Owino aliipatia Simba bao la pili akiunganisha kwa kichwa kona ya Singano kufanya matokeo kuwa 3-2.

Baada ya hali hiyo, kocha wa Yanga, Brandts alimtoa Kiiza na kumwingiza Simon Msuva, ambapo katika dakika ya 64 Ngassa alpiga shuti la karibu lililopanguliwa na kipa Abel Dhaira.

Yanga imeendeleza udhaifu wa kuruhusu mabao katika kipindi cha pili kwani kati ya mabao saba waliyofungwa msimu huu kabla ya jana, waliruhusu kuanzia katika dakika ya 49 mpaka 90, ndicho kilichotokea, baada ya Kaze kumalizia mpira wa adhabu uliopigwa na Cholo katika dakika ya 83 na kuiandikia Simba bao la kusawazisha. baada ya mechi kumalizika, kocha wa Simba, Abdalah Kibaden aliwasifu wachezaji wake kwa kucheza kwa kujituma na kufanikiwa kusawazisha.

Naye Brandts alisema wachezaji wake walicheza kizembe kipindi cha pili hasa sehemu ya kiungo.

Yanga iliwasili uwanjani saa 8:33, kupitia mlango wa kawaida, wakati watani zao Simba waliingia saa 8:35 kwa kupita geti lililopo upande Kaskazini walipo mashabiki wao.

Katika mchezo wa awali wa timu za vijana, Simba B na Yanga B zilimaliza kwa kutoka sare 1-1.


Vikosi

Simba: Abel Dhaira, Nassor ‘Cholo’ Masoud, Haruna Shamte, Kaze Gilbert, Joseph Owino, Jonas Mkude, Abdulhalim Humoud/ Lucian William, Ramadhani Singano, Amisi Tambwe, Betram Mwombeki/ Zahoro Pazi na Haruna Chanongo/ Said Hamisi.

Yanga: Ally Mustapha ‘Barthez’, Mbuyu Twite, David Luhende, Nadir Haroub, Kelvin Yondani, Athuman Idd, Mrisho Ngassa, Frank Domayo, Didier Kavumbagu, Hamis Kiiza/ Simon Msuva na Haruna Niyonzima

KAULI NZITO YA SOFIA SIMBA: SUGU ANA MAPEPO!!!



Mbeya. Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania(UWT), Sofia Simba na Mbunge wa Viti Maalumu, Mkoa waMbeya, Dk Mary Mwanjelwa (CCM), juzi walitumia muda mwingi jukwaani kumnangaMbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ (Chadema) wakimfananisha na `pepo’ aliyekwenda bungeni kwa ajili ya kufanya vurugu.
Mbeya. Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania(UWT), Sofia Simba na Mbunge wa Viti Maalumu, Mkoa waMbeya, Dk Mary Mwanjelwa (CCM), juzi walitumia muda mwingi jukwaani kumnangaMbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ (Chadema) wakimfananisha na `pepo’ aliyekwenda bungeni kwa ajili ya kufanya vurugu.
Viongozi hao walisema kuwa wananchi wa jiji hilo wamepeleka ‘pepo’ bungeni ndio maana mbunge  huyo amekuwa kinara wa vurugu ndani ya Bunge, hivyo wananchi wa Mbeya Mjini wamempeleka mtu anayehitaji kuombewa.
Walitoa kauli hiyo juzi wakati wakihutubia mkutano wa hadhara uliofanyika katika eneo la wazi la Kata ya Manga
Mjini Mbeya.
Simba, ambaye pia ni Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, alisema hali hiyo ya ‘mapepo’ mara kadhaa imekuwa  ikimsababishia mbunge huyo kujiingiza kwenye vitendo vya vurugu, likiwemo tukio la hivi karibuni kupigana bungeni badala ya kuibua hoja za maendeleo. Juhudi za gazeti hili za kumtafuta Sugu zilikwama jana baada ya kuelezwa na watu wake wa karibu kuwa alikuwa safarini China.
Simba alisema tukio la mbunge huyo kupigana na askari wa bunge ndani ya ukumbi, lilitokea kwa kuwa hakukuwa na mtu wa kuombea ‘mapepo’ siku hiyo baada ya kumkumba ghafla mbunge huyo.
 “Siku ile tukio linatokea bahati mbaya sana  Mchungaji  Lwakakatare (Mbunge  wa Viti Maalumu Getrud Lwakatare) hakuwemo ukumbini maana angeweza kuyaombea na hivyo naomba wananchi wa Mbeya msituletee ‘mapepo,” alisema.
Viongozi hao walisema kuwa wananchi wa jiji hilo wamepeleka ‘pepo’ bungeni ndio maana mbunge huyo amekuwa kinara wa vurugu ndani ya Bunge, hivyo wananchi wa Mbeya Mjini wamempeleka mtu anayehitaji kuombewa.

Walitoa kauli hiyo juzi wakati wakihutubia mkutano wa hadhara uliofanyika katika eneo la wazi la Kata ya Manga

Mjini Mbeya.

Simba, ambaye pia ni Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, alisema hali hiyo ya ‘mapepo’ mara kadhaa imekuwa ikimsababishia mbunge huyo kujiingiza kwenye vitendo vya vurugu, likiwemo tukio la hivi karibuni kupigana bungeni badala ya kuibua hoja za maendeleo. Juhudi za gazeti hili za kumtafuta Sugu zilikwama jana baada ya kuelezwa na watu wake wa karibu kuwa alikuwa safarini China.

Simba alisema tukio la mbunge huyo kupigana na askari wa bunge ndani ya ukumbi, lilitokea kwa kuwa hakukuwa na mtu wa kuombea ‘mapepo’ siku hiyo baada ya kumkumba ghafla mbunge huyo.

“Siku ile tukio linatokea bahati mbaya sana Mchungaji Lwakakatare (Mbunge wa Viti Maalumu Getrud Lwakatare) hakuwemo ukumbini maana angeweza kuyaombea na hivyo naomba wananchi wa Mbeya msituletee ‘mapepo,” alisema.

Saturday, 19 October 2013

Thursday, 17 October 2013

KAULI YA ZITTO KABWE YAVIAMSHA VYAMA VYA SIASA: WENGINE WAANZA KUJISAFISHA


Dar es Salaam. Maelekezo yaliyotolewa na Mwenyekiti wa Kamati ya Hesabu za Serikali (PAC), Zitto Kabwe kutaka kusitishwa kwa ruzuku kwa vyama vya siasa nchini kutokana na kutowasilisha taarifa za ukaguzi wa matumizi yake, yamevivuruga baadhi ya vyama vilivyotajwa.


Vyama vya siasa vinaonekana kutoa matamshi yanayolenga kujinasua katika hoja hiyo, vikiwemo vilivyomshutumu Zitto, kuilaumu Serikali na hata vingine vimediriki kutaka ruzuku hiyo ifutwe kwa maelezo kwamba ni ubadhilifu wa fedha za umma.


Juzi Zitto alisema tangu 2009 Serikali ilitoa kiasi cha Sh67.7 bilioni kama ruzuku kwa vyama tisa vya siasa, lakini vyama hivyo havijawahi kuwasilisha taarifa za ukaguzi hesabu zake msajili kama sheria inavyoagiza. Kwa sababu hiyo, Zitto aliamuru Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, kusimamisha utoaji wa ruzuku hadi hapo vitakapowasilisha ripoti ya ukaguzi na makatibu wake wakuu kuhojiwa.


Kwa mujibu wa Sheria namba 5 ya 1992 ambayo ilifanyiwa marekebisho ya Sheria namba 7 ya 2009, Vyama vya Siasa vinawajibika kuwasilisha hesabu zake kwa CAG na ofisi hiyo inaweza kuamua kuzifanyia ukaguzi yenyewe au kuteua mkaguzi.


Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Ludovick Utouh aliwahi kusema kuwa utaratibu ambao umekuwa ukitumiwa na vyama hivyo kwa kuteua kampuni binafsi siyo sahihi na ni kinyume cha sheria.


“Kwa mujibu wa kifungu cha 14 cha Sheria ya Vyama vya Siasa, vyama vinatakiwa viwasilishe hesabu kwa CAG, ndipo tuzikague au tuamue kampuni ya kufanya ukaguzi huo, sasa wao walichagua kampuni binafsi moja kwa moja zikawafanyia ukaguzi,” alisema Utouh wakati akitangaza kuthibitisha ubora wa hesabu za vyama vitano vilivyoshiriki kwenye Uchaguzu Mkuu wa 2010.


Mwenyekiti wa Democratic Party (DP), Mchungaji Christopher Mtikila alipendekeza kufutwa kwa ruzuku hiyo kwa vyama vya maelezo kuwa ni inawanyonya wananchi.


“Badala ya kuvipa vyama vya siasa ruzuku, tuelekeze fedha hizo kwenye miradi mingine ya maendeleo,” alisema Mtikila huku akiahidi kwamba chama hicho kitawasilisha kwa Msajili wa Vyama vya Siasa taarifa yake ya fedha iliyokaguliwa katika kipindi cha wiki mbili kuanzia sasa.


CCM wang’aka


Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimemshambulia kiongozi huyo, huku kikisema kuwa Zitto ambaye ni Naibu Katibu Mkuu wa Chadema anapaswa kushughulikia matatizo yaliyopo katika chama chake kwanza kabla ya kuzungumzia matatizo katika vyama vingine vya siasa.


Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye alisema chama hicho hakihusiki na agizo la PAC la kusimaishiwa ruzuku ya kila mwezi, kwani hesabu zake zimekuwa zikifanyiwa ukaguzi. Alisema CCM ipo tayari kwenda mbele ya PAC kikiwa na hesabu zilizokaguliwa na wakaguzi wa nje, Shirika la Ukaguzi la Taifa (Tanzania Audit Corporation - TAC) kuanzia 1977/1978 hadi 2010/2011.


“Januari 29, mwaka huu niliandika barua yenye kumbukumbu namba CMM/F. 20/80/89 ili kuwasilisha rasimu ya hesabu za mwaka wa fedha 2011/2012 lengo likiwa CAG atupangie siku ya TAC kutukagua,” alisema Nape na kuongeza: “Hesabu zilizokaguliwa na wakaguzi wa nje TAC ambazo ni za 2009/2010 na 2010/2011 tayari ziliwasilishwa kwa CAG.”


Nape alifafanua kwamba hesabu za 2011/2012 bado ziko kwa wakaguzi wa nje, wakishakamilisha nazo zitawasilishwa kwenye vikao vya chama na hatimaye kwa CAG.


“Hesabu hizi zikikaguliwa kwa mujibu wa utaratibu, anapelekewa CAG ambaye ndiye anazipeleka kwa Msajili wa Vyama vya Siasa na sio vinginevyo,” alisema.


Alidai kuwa Zitto anapaswa kuanza kutoa ‘boriti kwenye jicho lake ndipo aone kibanzi kwenye jicho la mwenzake’ kwa sababu chama chake ndicho kimekuwa na matumizi mabaya ya ruzuku. Alisema Zitto kama Naibu Katibu Mkuu wa Chadema ni vyema akawajibika ndani ya chama chake ili kuonyesha mfano kwa wengine.


“Wote tunakumbuka kelele zilizopo mtaani kuhusu matumizi mabaya ya ruzuku zinazoelekezwa na Chadema na viongozi wake kutoka kwa wanachama wao, hivyo si ajabu wakawa wanakiuka sheria hii na ndiyo chanzo cha kelele hizo za wanachama wao,”alisema.


Vyama vingine


Kwa upande wake, Chadema kilieleza kwamba hakijapata barua inayowaarifu kuhusu kutaka kufungiwa ruzuku kutokana na kutowasilisha taarifa ya ukaguzi.


Ofisa Habari Mwandamizi wa Chadema, Tumaini Makene ilisema hata barua ya kuitwa kwenye Kamati ya PAC, iliwafikia kwa kuchelewa. “Tunasubiri barua rasmi ya suala hili ndio mamlaka zinazohusika na masuala ya fedha ndani ya chama, hususan, Baraza la Wadhamini wa Chama kuweza kutafakari hatua,” alisema Makene.


Hata hivyo, alisema angependa umma utambue kwamba “Chadema ndicho kilichokuwa mstari wa mbele tangu kabla na baada ya mwaka 2009 kutaka ukaguzi na wazi katika mapato na matumizi ya vyama vya siasa.”


Alifafanua kuwa msimamo wa Chadema kwenye mkakakati huo ulikuwa ni kuibana CCM kutokana na madai ya baadhi ya vigogo wake “kukwapua fedha Benki Kuu ( Akaunti ya Madeni ya Nje – EPA) na kuzitumia kwenye uchaguzi wa mwaka 2005.”


Alijigamba kuwa hesabu za chama chake zimekuwa zikikaguliwa kila mwaka na kwamba wanasubiri maelezo ya barua kuhusu kile kinacholalamikiwa.


Kwa upande wa Chama cha Wananchi (CUF) kimesema hesabu zake ziko safi, ila imeshindikana kukaguliwa kwa vile Serikali haijatoa fedha za kugharimia ukaguzi huo.


Naibu Katibu Mkuu wa CUF, Tanzania Bara, Julius Mtatiro alisema hesabu zao zimekwishakaguliwa na wakaguzi wa ndani.“Tunachosubiri ni Serikali kutuletea mkaguzi ambaye baada ya kufanya hivyo hesabu zetu zitakuwa zimekamilika na wananchi wataweza kuziona,” alisema.


Alisema chama hicho hakina fedha kwa ajili ya kugharimia mkaguzi wa nje na kwamba jukumu hilo ni la Serikali.


Naye Katibu Mkuu wa Chama cha NCCR-Mageuzi, Samwel Ruhuza alisema kuwa chama hicho kipo tayari kuwasilisha hesabu zake, kwani zipo tayari na kwamba walishindwa kuziwasilisha baada ya kuelezwa kuwa CAG ndiye anayepaswa kufanya ukaguzi.


Imeandaliwa na Aidan Mhando, Leon Bahati, Fidelis Butahe na Raymond Kaminyoge

Wednesday, 16 October 2013

TUBURUDIKE KIDOGO JAMANI

PICHA ZA RED KAPET BET AWARDS 2013

2 Chainz Kwenye Tuzo za BET Hiphop Music Awards jana, 
B.o.b
Eve 
CLICK READ MORE KUCHEK ZAIDI MTU WANGU
Kevin Hart

Nelly

Rick Ross

Snoop Dogg

Schoolboy Q, Kendrick Lamar, & Jay Rock

Bone Thugs-N-Harmony 

Future & Mike Will

Lee On The Beats, DJ Khaled, & Ace Hood



Lil Mama

NILIVYOTESWA NA NILIYEMPENDA NA HATIMAYE AKAPIGWA MTUNGO


Zamani nilikuwa nasikia tu stori za kisekondari juu ya haya mambo lakin kweli wahenga walisema kuwa uyaone.


Nilikuwa na mchumba wangu ambaye alikuwa anasoma chuo fulani dodoma nilitokea kumpenda sana na hata kufikia hatua ya kupanga kufunga ndoa mwezi wa pili mwakani baada ya kutoa mahali mwaka huu.katika mahusiano yetu takribani miaka mitatu hatukuwai kukwaruzana kwa namna ya kutahadharisha mahusiano yetu.nilijitolea sana kumuhudumia vyema japo alikuwa na mkopo lakini pia nilikuwa ninamlipia mdogo wake wa kike ada ya diploma ktk chuo fulani par ambapo yeye anachukua diploma ya biashara.Mwaka jana mwezi wa pili nilipata safari ya kwenda nje ya nchi kufanya course ya mwaka mzima na kumuacha yeye nyumbani kwangu ambapo nilimuachia nyumba na gari yangu japo hili gari hata kabla ya sijaondoka alikuwa anatumia yy muda mwingi sababu mm nilikuwa natumia sana gari ya ofisini.mwezi wa tisa nilipewa mapumziko ya wiki mbili nikarudi na kumkuta kaleta rafiki zake watatu wanakaa pamoja mbaya zaidi hali ilinionesha kwamba walikuwa walevi wa kukubu na walikuwa wanadiliki pia kulala chumbani kwangu pindi wamelewa.niliporudi niliona nimfanyie suprise bila kumwabia kumbe nilijifanyia mwenyewe maana baada ya kuwasili tz nilikaa dar siku mbili ili kuripoti nipo tz then nikaanza safari ya dom nilipofika saa kumi na mbili jioni sikumkuta nami sikupiga simu nikawanasubiri nione matokeo yake.


Sasa ilipofika saa nne usiku bado alikuwa hajarudi nikaamua kumpigia simu yangu wakati nipo nje nilikuwa natumia roaming service kwaiyo namba haikuwa nabadilika hata nilipompigia akajua bado niko nje ya nchi.cha ajabu na alichonishtua akaniambia nipo nyumbani naangalia movie nikamwambia sawa na kaka yangu kanipigiaatapita kukusalimia anatoka mwanza akasema sawa then kama baada ya dk 20 nikaona anakuja akiwa na hao wadada huku wamelewa wote nahisi sababu ya pombe hakushtuka sana aliponiona ila asubuhi aliniomba sana nimsamahe.lakini tayari kichwa changu kilishagonga alerm baada ya kuona hata mazingira halisi jinsi walivyokuwa wanaishi pale.nikawa nimerudi kumalizia course yanguna mwezi watatu nikarudi tz hapa ndipo nilipoona kuna kitu kinaendelea sio sawa.hakuwa na uhuru tena na simu yake akawa hajiamini ndipo nikaanza ku track simu yake nikagundua kabadilika sana na ana mahusiano zaidi ya mmoja nje.kilichoniuma zaidi nilipokuwa zanzibar takriban mwezi mzima kkikazi tangu mwei wa nane kumbe alikuwa kaenda club na akalewa wakambeba na wakampiga mtungo nilipopata iyo habari ikabidi niwatafute wahusika kidiplomasia na wakanipa paka mkanda waliorekodi.ijumaa nikamwambia nataka tuende kwao nikwasalimie wazazi akafurahi sana nilipofika jioni nikawaomba wote na kuanza kuwasilimulia yote na kuwaonesha mkanda kwakweli mamake alilia sana hakuamini hata huyo mwanamke hakuamini kama nilikuwa na taarifa hizo zote nikawa nacheka nae hivi nimerudi jana wakuu na kuona nishare nanyi kwa mawali matatu

UTAFITI: WASIO NA ELIMU NDO WANAMUUNGA RAIS KIKWETE MKONO KWA UTENDAJI KAZI WAKE!!

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Kupunguza Umaskini (REPOA),Profesa Samuel Wangwe akizungumza jijini Dar es Salaam jana wakati wa kutoa matokeo ya utafiti uliongozwa na taasisi ya Afrobarometer. Picha na Silvan Kiwale.

Dar es Salaam. Ripoti mpya ya utafiti imebaini kuwa asilimia kubwa ya Watanzania wenye elimu ya darasa la saba na wale wasiosoma, ndiyo wanaokubaliana na utendaji kazi wa Rais Jakaya Kikwete.
Ripoti ya utafiti huo iliyopewa jina la ‘Namna Watanzania wanavyouangalia utendaji kazi wa Bunge na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania’ ilitolewa jana jijini Dar es Salaam na Asasi ya Afrobarometer, inaonyesha kuwa asilimia 77 ya waliokosa elimu ndiyo wanamuunga mkono Rais Kikwete.

Afrobarometa ni Asasi ya Kimataifa inayojumuisha taasisi tatu za Institute for Democracy ya Afrika Kusini, Ghana Centre for Democratic Development ya Ghana na Political Science Department ya Chuo Kikuu cha Michigan cha Marekani.

Mtafiti Msaidizi wa Afrobarometer, Stephen Mwombela akisoma ripoti hiyo mbele ya waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, alisema asilimia 72 ya wale walioishia darasa la saba ndiyo wanamuunga mkono Rais.

Wakati asilimia 23 ya watu wasiosoma ndiyo hawamkubali Rais na asilimia 28 ya wale walioishia darasa la saba, pia hawaridhishwi na utendaji wa kiongozi huyo.

Mwombela, hata hivyo, alisema utafiti huo uliohusisha watu 2,400 wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania unaonyesha kuwa idadi kubwa ya wasomi wa kiwango cha sekondari na kuendelea wanaunga pia mkono utendaji wa Rais, lakini siyo kwa kiwango cha juu kama wale ambao hawajasoma.

“Asilimia 60 ya waliosoma elimu ya sekondari na kuendelea wanaunga mkono utendaji wa Rais, lakini 40 hawakubaliani na utendaji wake,” ilisema taarifa ya matokeo ya utafiti huo uliofanyika kati ya Mei hadi Juni mwaka jana.

Matokeo ya utafiti huo yanatofautiana na yale ya mwaka 2008, ambayo yalionyesha kuwa wasomi walikuwa wanamuunga mkono Rais kwa asilimia 92.

Pia katika matokeo ya utafiti huo wa mwaka 2008, ulionyesha kuwa wasiosoma walimuunga mkono kiongozi huyo kwa asilimia 92.

Imani ya wananchi kwa Rais

Ripoti hiyo ilisema pia imani ya wananchi kwa utendaji wa Rais imeshuka hadi kufikia asilimia 74 kwa mwaka jana, tofauti na asilimia 94 ya mwaka 2005 wakati aliposhika wadhifa huo
Pia utafiti huo uliodhaminiwa na Taasisi ya Utafiti kuhusu Kuondoa Umaskini (Repoa) umebainisha kuwa imani ya wananchi kwa Rais imeshuka kutoka asilimia 88 mwaka 2008 hadi asilimia 74, huku idadi ya watu wasiokubaliana kabisa na Rais ikiongezeka kutoka asilimia 11 mwaka 2008 hadi asilimia 26 mwaka 2012.

Imani kwa Bunge
Wananchi wengi pia wameonyesha kutokuwa na imani na mwenendo wa Bunge, kwa kulipa asilimia 76 mwaka 2012, idadi yao ikishuka kutoka asilimia 83 ya mwaka 2008.

Imani ya wananchi kwa Bunge imeshuka katika kipindi hiki ambalo liko chini ya Spika Anne Makinda, ambaye alichukua uongozi mwaka 2010 wakati mwaka ule wa 2008 lilikuwa chini ya Samuel Sitta imani ilikuwa juu. Taarifa hiyo pia inaeleza kuwa watu wanaoishi vijijini ndiyo wanaoridhishwa zaidi na Bunge kwa kupata asilimia 63, ikilinganishwa na wakazi wa mijini ambao ni asilimia 60.

Pia imebainika kuwa wananchi wa Zanzibar wanaridhishwa zaidi na utendaji wa Bunge kwa asilimia 64, tofauti na wananchi wa Tanzania Bara ambao wanaridhishwa kwa asilimia 61.

“Watu waliokuwa wanakubaliana na utendaji wa Bunge mwaka 2003 walikuwa asilimia 31, lakini mwaka 2012 idadi iliongezeka hadi asilimia 61,” alisema Mwombela wakati akiwasilisha matokeo ya utafiti huo unaofanyika kwa mara ya tano nchini Tanzania.

Hata hivyo, Mwombela alisema kuwa wananchi wengi bado wanafurahishwa na utendaji wa Mahakama, lakini idadi yao imepanda kutoka asilimia 73 kwa mwaka 2008 na kuwa asilimia 74 mwaka 2012.
Akichangia baada ya ripoti hiyo kuwasilishwa, Dk Abel Kinyondo, alisema kuwa matokeo ya utafiti huo hayajaonyesha kuporomoka kwa imani kwa Rais badala yake yameonyesha uhalisia.

“Inawezekana imani kwa Rais haijashuka, badala yake imekaa katika hali yake, kwa sababu kitu gani alikifanya 2008 watu wakampenda sana, ambacho leo hii hajakifanya hadi wasimpende?” alihoji Kinyondo. Kinyondo alionekana kushangazwa na namna Rais alivyoweza kupata asilimia 71 wakati nchi inapita katika kipindi kigumu cha rushwa na ufisadi.

Mwakilishi kutoka Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Victor Kimesera alisema utafiti huo una kasoro kadhaa ikiwa ni pamoja na kumtaja Rais kuwa ndiye mwakilishi pekee wa Serikali wakati kuna viongozi wengine wengi. “Kwa upande wa Rais walitakiwa kuhoji viongozi wengi zaidi kwa sababu Rais siyo kiongozi pekee yake katika Serikali,” alisema.

Naye Naibu Katibu Mkuu wa zamani wa Wizara ya Fedha, Dk Jonas Kipokola alisema kama utafiti huo ungefanyika Mei hadi Juni mwaka huu, huenda matokeo yangekuwa tofauti. “Siwezi kusema yangekuwaje, lakini yasingekuwa hivyo yalivyo,” alisema Kipokola.

JK KIKWETE AKUTANA NA VYAMA VYA UPINZANI IKULU: TANZANIA KWANZA


Dar es Salaam. Rais Jakaya Kikwete na viongozi wa vyama vya siasa vya CCM, Chadema, CUF, NCCR- Mageuzi, TLP na UDP wamekubaliana mambo mawili makubwa baada ya kuweka pembeni tofauti za kiitikadi na kutanguliza masilahi ya taifa walipokutana jana Ikulu jijini Dar es Salaam.


Mkutano huo uliitishwa na Rais Kikwete ili kuondoa sintofahamu ya Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba uliopitishwa Septemba na Bunge lilipokutana mjini Dodoma.

Taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu jana jioni ilisema katika mkutano huo ilikubaliwa kwamba vyama vyote vya siasa nchini vyenye mawazo, maoni na mapendekezo ya kuboresha Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba viwasilishe mapendekezo yao haraka serikalini ili ifatutwe namna ya kuyashirikisha mapendekezo hayo katika marekebisho ya sheria hiyo.

Pia Rais na vyama hivyo walikubaliana kwamba vyama vya siasa nchini, kama wadau muhimu katika mchakato wa Katiba Mpya, viangalie namna ya kukutana na kujenga mfumo wa mawasiliano na maridhiano kwa lengo la kusukuma mbele mchakato huo kwa masilahi mapana ya nchi yao na mustakabali wa taifa.


“Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD) kimepewa jukumu la kuratibu jambo hilo ikiwa ni pamoja na kuandaa mkutano wa vyama hivyo na wadau wengine nchini,” iliongeza taarifa hiyo.


Viongozi wa vyama vyama vya siasa waliohudhuria mkutano huo ni Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba, Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia.

Wengine ni Makamu Mwenyekiti wa CCM, Philip Mangula, Isaack Cheyo ambaye alimwakilisha Mwenyekiti wa UDP, John Cheyo na Nancy Mrikaria ambaye alimwakilisha Mwenyekiti wa TLP, Augustine Mrema. Cheyo na Mrema wako nje ya nchi.
Wengine ambao waliambatana na wenyeviti wao ni Mohamed Mnyaa na Julius Mtatiro wa CUF, Tundu Lissu na John Mnyika wa Chadema na Martin Mng’ongo wa NCCR-Mageuzi.

Vicheko Ikulu
Vicheko na bashasha vyatawala Ikulu
Ilikuwa fursa kwa Rais Kikwete kukutana na viongozi hao baada ya kipindi cha miezi miwili cha kurushiana maneno baina ya viongozi wa Bunge, Serikali, CCM waliokuwa wakivutana na viongozi wa vyama vitatu vya Chadema, CUF na NCCR- Mageuzi.

Kama mtu yeyote angeulizwa kutabiri katika tukio lililotokea jana lingetokea basi angekuwa na wakati mgumu kutokana na ukali wa maneno na malumbano katika kipindi chote baada ya kumalizika kwa mkutano wa Bunge wa Septemba.Rais Kikwete alionekana mwenye furaha tele wakati alipokutana na viongozi wa vyama hivyo na kivutio zaidi ilikuwa pale alipokutana na Mnadhimu Mkuu wa Kambi rasmi ya Upinzani, Tundu Lissu.
Viongozi hao walisalimiana huku wote wakitabasamu na kuashiria kuwa waliamua kuweka tofauti zao pembeni na kuangalia masilahi ya nchi.

Kumbuka katika hotuba yake ya mwisho wa mwezi Septemba, Rais Kikwete alimshutumu Lissu kwa kusema kwamba katika uteuzi wa wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba kuwa yeye hakuheshimu mawazo ya Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) na Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT).

Rais Kikwete alikaririwa akisema kauli hiyo ya Lissu ni uzushi, uongo na uzandiki wa hali ya juu, huku akisisitiza kuwa mbunge huyo alitoa kauli hiyo ili kupotosha ukweli na pengine isaidie kujenga hoja yake ya kutaka Rais asiteue wajumbe 166 wa Bunge Maalum la Katiba.

Lissu, ambaye pia ni Mbunge wa Singida Mashariki, alipinga tuhuma hizo na kusisitiza Rais aliteua wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba kutoka Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC) na Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT) bila ya ridhaa yao.
Chikawe, Wassira na Lukuvi ndani
Mawaziri watatu, ambao walitetea kwa nguvu kupitishwa kwa muswada ule ndani na nje ya Bunge walihudhuria mazungumzo hayo.

Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Uratibu na Bunge, William Lukuvi, Waziri wa Sheria na Katiba, Mathias Chikawe na Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Rais anayeshughulikia Mahusiano na Uratibu, Stephen Wassira walikuwemo kwenye mazungumzo ya jana.

Mawaziri hawa kwa nyakati tofauti walitetea kuwa mchakato wa muswada ule haukuwa na matatizo yeyote na kushikilia kuwa lazima Rais lazima asaini muswada kwani ulikuwa umepitishwa kihalali na Bunge.

Pia walikuwa wameshikilia kuwa safari hii kulikuwa hakuna mambo ya mazungumzo kati ya Rais na upinzani.Chanzo cha sintofahamuWabunge wa vyama vya Chadema, CUF na NCCR-Mageuzi walisusia mjadala wa muswada huo wakipinga matayarisho yake kutoshirikisha upande wa Zanzibar na pia walikuwa hawakubaliani na baadhi ya vipengele vya muswada huo.

Katika hatua nyingine, taarifa kutoka Ikulu zilisema kwamba Rais Kikwete alisaini muswada huo tangu Oktoba 10 mwaka huu siku ambayo wapinzani walipanga kufanya maandamano nchi nzima.

Katika mahojiano na Mwananchi jana jioni, Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Salva Rweyemamu alisema muswada huo tayari ulikwishasainiwa na Rais na kama kuna marekebisho yatafanywa.

Mwananchi ilimtafuta Rweyemamu baada ya kusikia akithibitisha kusainiwa kwa muswada huo katika mahojiano na BBC Idhaa ya Kiswahili jana.

Akizungumza na Mwananchi Rweyemamu alisema, “Rais ameshasaini tangu Oktoba 10, unajua kulikuwa hakuna tatizo lolote kuhusu muswada huu kwa sababu ulifuata taratibu zote bungeni.”

Rweyemamu alisema kuwa awali Ikulu ilitoa taarifa kuwa Rais atakutana na wapinzani, pia atausaini muswada huo.

“Muswada umepitishwa bungeni na yeye amekamilisha kazi kwa kuusaini ili kuwa sheria. Alipokutana na wapinzani leo (jana) amewaeleza hilo na wameridhika” alisema Rweyemamu.
CHANZO: GAZETI LA MWANANCHI

Tuesday, 15 October 2013

RAIS KIKWETE AKUTANA NA WAPINZANI IKULU LEO:KATIBA MPYA


Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika mazungumzo na Viongozi wa Vyama vya Siasa nchini,waliofika ikulu jijini Dar es Salaam leo.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimkaribisha ikulu kiongozi wa kambi ya upinzani Bungeni Mh.Freeman Mbowe mara baada ya mazungumzo nao leo ikulu jijini Dar es Salaam.Nyuma kushoto ni Kiongozi wa NCCR Mageuzi,Mh. James Mbatia na Professa Ibrahim Lipumba wa CUF.

Rais Dkt.Jakaya Kikwete akisalimiana na Mhe.Tundu Lissu CHADEMA Nyuma ni Mhe.James Mbatia NCCR Mageuzi.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Mhe. John Mnyika.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya Pamoja na Viongozi wa Vyama vya upinzani muda mfupi kabla ya kuanza mazungumzo kuhusu rasimu ya katiba ikulu jijini Dar es Salaam.Wengine katika picha kutoka kushoto Isaack Cheyo UDP, James Mbatia NCCR Mageuzi, Professa Ibrahim Lipumba CUF, Freeman Mbowe CHADEMA, Philip Mangula CCM, na Bibi Nancy Mrikaria aliyemwakilisha Mwenyekiti wa TLP Mhe.Agustine Lyatonga Mrema.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Vyama vya upinzani na wasaidizi wao waandamizi muda mfupi kabla ya kuanza mazungumzo kuhusu rasimu ya katika ikulu jijini Dar es Salaam leo.Kutoka kushoto mbele Isaack Cheyo UDP, James Mbatia NCCR Mageuzi, Professa Ibrahim Lipumba CUF, Freeman Mbowe CHADEMA, Philip Mangula CCM, na Bibi Nancy Mrikaria aliyemwakilisha Mwenyekiti wa TLP Mhe.Agustine Lyatonga Mrema.Waliosimama Nyuma kutoka kushoto ni Naibu Katibu Mkuu CUF Bwana Julius Mtatiro,Mhe. Tundu Lissu CHADEMA, Bwana Martin Mng’ong’o NCCR Mageuzi ,Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Uratibu na Bunge William Lukuvi, Mhe.Habib Mnyaa CUF, Mbunge wa Ubungo Kwa tiketi ya CHADEMA Mhe.John Mnyika, Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Mahusiano na Uratibu Mhe.Steven Wassira na Waziri wa Katiba na Sheria Mhe.Mathias Chikawe.(picha na Freddy Maro).

JK KUJADILI MUSWADA NA MBOWE, LIPUMBA, MBATIA

RAIS Jakaya Kikwete leo anakutana Ikulu na viongozi wa vyama vya CHADEMA, CUF na NCCR-Mageuzi kwa ajili ya mazungumzo ya kuboresha kasoro zilizojitokeza kwenye muswada wa sheria ya marekebisho ya sheria ya mabadiliko ya Katiba ya mwaka 2013.

Hatua hiyo inatokana na msimamo wa wabunge wa vyama hivyo kususia mjadala wa muswada huo uliopitishwa hivi karibuni na wabunge wachache wa CCM na Augustine Mrema wa TLP, wakidai umechakachuliwa, huku Zanzibar ikiwa haijashirikishwa.

Kufuatia kusigana huko, viongozi wa vyama hivyo; Freeman Mbowe (CHADEMA), Prof. Ibrahim Lipumba (CUF) na James Mbatia (NCCR-Mageuzi), walikutana na makundi mbalimbali ya wadau na kutangaza kufanya mikutano na maandamano nchi nzima kupinga rais asisaini muswada huo.

Uamuzi wa wapinzani hao uliwaibua mawaziri kadhaa, Stephen Wassira (Ofisi ya Rais-Mahusiano na Uratibu), William Lukuvi (Sera, Uratibu na Bunge), Mathias Chikawe (Katiba na Sheria) na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema wakiwabeza.

Mawaziri hao walidai wapinzani wanapoteza muda wa mchakato ili rais awaite Ikulu tena kwa mazungumzo waweze kunywa chai na juisi, jambo walilosisitiza kuwa haliwezekani, kwani milango hiyo imefungwa.

Hata Waziri Chikawe alifikia hatua ya kumtisha Rais Kikwete, akisema kuwa asipousaini muswada huo atakuwa ametangaza mgogoro na Bunge, kwani lilifanya kazi yake kwa kufuata Katiba.

Rais Kikwete alitilia maanani hoja za pande zote na kuamua kuwaita wapinzani mezani kuzungumza nao, akisema kuwa kama dhamira yao ni kutaka kupata Katiba mpya, anawashauri waachane na mipango ya maandamano na kufanya ghasia, bali watumie njia halali, kwamba serikali iko tayari kuwasikiliza.

Hoja zinazovutaniwa

Mbali na mambo mengine, wapinzani wanadai kuwa muswada huo ulichomekwa baadhi ya vipengele ambavyo vingeisaidia CCM kutawala mchakato mzima wa katiba.

Katika hoja ya mapendekezo ya kumpa rais mamlaka ya kuteua wajumbe wa Bunge Maalumu, wapinzani hao wanasema hayakubaliki, kwamba yanarudisha dhana kwamba wajumbe hawa watakuwa watu wa rais ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM.

“Sheria iweke wazi kwamba wajumbe hawa ‘watateuliwa’ na taasisi zilizotajwa. Hii itaondoa utata juu ya uwakilishi wao na juu ya mamlaka yao ya uteuzi.

“Sheria itaje kwamba idadi ya wajumbe wa Bunge Maalumu watakaotokana na kila taasisi iliyoorodheshwa katika kifungu cha 22(1)(c) itakuwa 354,” walisema wapinzani.

Katika suala la Zanzibar, wapinzani hao wanasema wananchi wa huko hawakushirikishwa wakati wa uandaaji wa muswada huo, hivyo kutaka mambo kadhaa yafanyike ili kuondoa mgongano.

Kwamba, ili kutimiza matakwa haya ya sheria na kwa kuzingatia mapendekezo ya Rasimu ya Katiba iliyotolewa na Tume, Bunge linahitaji kuangalia upya suala la uwakilishi wa Zanzibar katika Bunge Maalumu.

Kwa mujibu wa kifungu cha 22(2) cha Sheria, idadi ya wajumbe wa Zanzibar katika Bunge Maalumu watakaotokana na makundi yaliyoainishwa katika kifungu cha 22(1)(c) “... haitapungua theluthi moja ya wajumbe hao.”

Hii ina maana kwamba, kwa uchache kabisa, wajumbe hao wa Zanzibar hawatapungua 55.

Rasimu ya Katiba itakayojadiliwa na Bunge Maalumu inahusu Katiba ya Jamhuri ya Muungano peke yake. Rasimu hiyo imependekeza kwamba masuala yote yasiyo ya Muungano, ya washirika wa Muungano, yaani Tanzania Bara na Zanzibar, yashughulikiwe na Katiba za washirika hao.

Rais Kikwete katika kutambua hoja za wapinzani aliomba hekima ziwaongoze viongozi wa pande zote ili waweze kutumia utaratibu walioutumia mwaka 2012.

“Kulipotokea mazingira kama haya pande zote zilikaa pamoja na kuzungumzia hoja moja baada ya nyingine na kukubaliana nini kifanyike na kifanyike vipi. Baada ya kuridhiana hatua zipasazo za kisheria na kanuni zilichukuliwa na kumaliza mzozo,” alisema rais.

Aliongeza kuwa kufanya kinyume cha hayo hakutaleta ufumbuzi wa mzozo huu na kutaliingiza taifa kwenye matatizo yasiyokuwa ya lazima.

Rais Kikwete alisisitiza kuwa hawatengenezi katiba ya chama fulani bali katiba ya nchi, katiba ya watu wa vyama vyote na wasiokuwa na vyama ambao ndio wengi kuliko wote.

Kuhusu ushiriki wa Zanzibar, alisema kuwa alielezwa ni kwa kiasi gani Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ilivyoshirikishwa na kutoa maoni yake yaliyojumuishwa katika muswada.

“Kama ni hivyo, nashauri kuwa suala hili lirudishwe bungeni ili wabunge walizungumze na kulifanyia uamuzi muafaka. Vinginevyo watu wataendelea kulaumiana isivyostahili,” alisema.

Suala la Tume ya Mabadiliko ya Katiba nalo litakuwa sehemu ya mjadala huo, licha ya Rais Kikwete naye kuona umuhimu wake akitaka ihusike kwenye hatua ya Bunge Maalumu.

“Nimeulizia ilikuwaje? Nimeelezwa kuwa jambo hili halitokani na mapendekezo ya serikali wala ya Kamati ya Bunge ya Katiba, Sheria na Utawala. Limetokana na pendekezo la mbunge katika Bunge wakati wa kupitia vifungu na kuungwa mkono na wabunge wengi.

“Nami naiona hoja ya wajumbe wa tume kuwa na wajibu wakati wa Bunge Maalumu, hasa wa kusaidia kufafanua mapendekezo ya tume,” alisema




MMILIKI WA KONTENA LILILO KAMATWA LIKIWA NA VIUNGO VYA BINADAMU VYA BANDIA VYA KUTISHA KENYA AJULIKANA

Hatimaye mmiliki wa kasha la mizigo lililonaswa katika bandari ya mombasa likiwa na sanamu za vibwengo vya kutisha, amejulikana
Kwa mujibu wa taarifa rasmi, kampuni ya 'Market Masters' wanaomiliki maduka ya Village Market hapa Nairobi wamekiri kuagiza shehena hiyo kwa sherehe zao za kila mwaka. Wakati huo huo, mwanasiasa Omingo Magara amekanusha kuagiza shehena hiyo na akaitaka halmashauri ya ushuru nchini KRA kumuomba msamaha mara moja.


Sunday, 13 October 2013

MWANDISHI WA HABARI UFOO SARO APIGWA RISASI:

Mama yake apigwa Risasi na kufariki hapo hapo!
Muuwaji nae ajipiga Risasi na Kufa hapo hapo!

Aidha mvamizi huyo alimuua mama yake Ufoo papo hapo na yeye mwenyewe kujiua kwa risasi, 

Aidha anayedhaniwa kufanya mauaji hoyo ya kutisha ni mume au mchumba wa mwandishi wa habari wa ITV na Radio One Ufoo Saro na yeye mwenyewe kujiua.
akizungumza na mtandao huu kamanda wa polisi wa mkoa wa kipolisi wa kinondoni kamanda Wambura amesema tukio hilo limetokea majira ya alfajiri ya leo.
Kamanda wambura ameongeza kuwa mwanaume huyo anafanya kazi umoja wa mataifa UN huko sudani ila bado haijafahamika kwamba anafanyia kitengo gani (japo kwa habari za mtaani zinasema mtu huyo ni mwanajeshi ila bado hazijathibitishwa)

Kamanda Wambura anasema inasemekana kulikua kuna ugomvi kati ya wawili hao ambapo walishindwa kuelewana na ndipo walipoamua kwenda kwa mama mzazi wa Ufoo Saro(mama mkwe) na ndipo mwanaume huyo alipomshutumu mama mkwe wake kwamba anamtetea mwanae ndipo alipotoa bastola na kumpiga mama yake na Ufoo Saro Risasi ya kichwa na kumuua papo hapo na kisha akampiga Ufoo Saro risasi ya mbili moja ya tumboni na ingine ya mguuni na kudhani kwamba amemuua kumbe amemjeruhi tu kisha kujipiga mwenyewe risasi ya kidevuni na kufariki dunia hapo hapo

Saturday, 12 October 2013

Wahamiaji haramu 16 wa Somalia wakamatwa ndani ya Lori Mkoani Morogoro

Wahamiaji haramu 16 kutoka nchini somalia wamekamatwa Mkoani morogoro wakiwa wamejificha katika lori la mizigo lililosheni chokaa likitokea jijini dar es salaam kuelekea mkoani mbeya

Kupatikana kwa wahamiaji haramu hao kunatokana na ushirikiano wa wananchi ambao umesaidia kukamatwa kwa wahamiaji hao huku wakidai kuwa baadhi yao walikosa hewa kufuatia kujificha katika mizigo hiyo
Gari lilokuwa limebeba wahamiaji haramu hao likiwa katika kituo cha polisi mkaoni morogoro
Wahamiaji haramu kutoka somalia wamekamatwa Mkoani Morogoro leo .Wahamiaji hao waliokuwa wakisafirishwa katika gari la mizigo lilokuwa limebeba shehena ya chokaaa..

Kwa upande wake afisa uhamiaji mkoa wa Morogoro Hamprey Minja amesema kuwa dereva wa gari hilo amekamatwa na kufikishwa kituo cha polisi ambapo amesema kuwa vyombo vya ulinzi na usalama vimedhibiti kwa kiasi kikubwa maeneo ya mipaka kwa ajili ya kudhibiti matukio ya wahamiaji haramu hali inayopelekea wahamiaji hao kutumia njia nyingine ikiwemo ya kujificha katika magari ya mizigo

Jeshi la polisi mkoa wa Morogoro limewaweka chini ya ulinzi wahamiaji hao ikifanya taratibu za kuwafikisha mahakamani kujibu mashtaka ya kuingia nchini bila kibali Mmoja ya wahamiaji haramu akishushwa katika gari hilo akiwa katika hali mbaya

Friday, 11 October 2013

SHEHENA YA VIUNGO VYA BINADAMU YAKAMATWA KENYA: YASADIKIKA VILIKUWA VIKATUMIKE KWENYE DINI YA KISHETANI



Wengi walioipata hii taarifa wanashangaa imekuaje ni viungo tu vya binadamu vimepatikana kwenye kontena zima vikiwa vinaingizwa Kenya? vinakwenda wapi? kazi yake ni nini?

Taarifa iliyoripotiwa na Citizen TV Kenya inasema Shehena hii iliyokamatwa baada ya kupitishwa kwenye bandari ya Mombasa inasemekana imesafirishwa na Mwanasiasa maarufu ambae kabla ya kukamatwa alisema ilikua na bidhaa za nyumbani ambapo ilipofika kwenye kituo cha ukaguzi wa mashehena cha Changamwe ilipatikana na vikaragosi vya mafuvu na mifupa ya binadamu ndipo amri ikatoka kontena likamatwe.

Baadhi ya mifupa ya binadamu iliyopatikana ni pamoja na mafuvu, miguu na mikono pamoja bidhaa za nyumba ambapo vyote kwa pamoja vilikua vinasafirishwa ambapo Afisa wa maswala ya Uhusiano mwema wa KRA Fatuma Yusuf alithibitisha kwamba hii shehena iliingia kutoka China siku ya pili ya October 2013 kabla ya kugundulika ilikua na vikaragosi vya kutisha ikiwemo mifupa ya binadamu.

Mpaka sasa uchunguzi wa shehena hili unaendelea lakini baadhi ya wakazi wa Mombasa wameonyesha wasiwasi wao na kusema kuna haja ya Serikali kutoa ripoti ya ibada za kishetani ambayo inasemekana kubuniwa na Rais Mstaafu Daniel Arap Moi miaka kadhaa iliyopita.















credit: millad ayo.com